kocha Nabi
JF-Expert Member
- Feb 1, 2022
- 834
- 2,410
kwa uelewa wangu naona asilimia kubwa walikuwa wanafariki watu wazima na huanza kwanza kufika taarifa za ugonjwa.Zamani miaka ya nyuma Msiba ulikuwa unatumia Mwezi mzima .
Ila jambo ambalo huwa nalitafakari ni kuhusu "the power of connectivity"
Yaani kuna wale ndugu zetu walikuwa wakitoka Bukoba na kwenda kutafuta Maisha mikoa mbali mbali na wengine nje ya nchi .
Ila ilikuwa ikitokea Msiba ndani ya huo mwezi unaona wanarudi Pasipokuandikiwa barua , kupigiwa simu wala kutumiwa E-mail
Hili jambo binafsi nimelishuhudia Sana miaka ya nyuma.
Mwaka jana nilimuuliza hili jambo mzee wangu nikamuuliza ulijuaje kuwa Mama yako amefariki na wakati hakuna mtu alikupa taarifa na ndani ya huo mwezi ulikuja msibani akasema alikuwa anasikia sauti ya ndani ikimwambia something is wrong unabidi kufanya ufanyavyo kuwasiliana na watu wa nyumbani na alikuwa akijaribu kucheki anakuta kweli msiba.
Na zamani ilikuwa sio rahisi mtu kufia ndani pasipo watu wake wa karibu kujua.
Ila Leo hii watu tupo disconnected na universe .
Ni rahisi Sana kumsikia MTU kafia ndani na maiti yake imejulikana baada ya mwaka mmoja.
Na ni rahisi sana mtu kufiwa na mtu wake wa karibu Ila asitambue chochote hadi ajulishwe either kwa simu n.k
ikumbukwe zamani mtu akitoka kwao kijijini kurudi tena hadi imchukue miaka na mikaka. hivyo wengi wao zilikuwa zinafika taarifa za ugonjwa ndipo maamuzi ya kurudi kijijini kuuguza hufatwa.
na mara nyingi wagonjwa walikuwa wakifika hali ya kuumwa sana hawaishi kwani hakukuwa na huduma nzuri za afya kipindi hiko.
so watu wengi walijikuta wanafikia msiba ama wakifika kijijini ndani ya siku chache mgonjwa hufariki.