Je, Zanzibar inasonga mbele au nyuma?

Je, Zanzibar inasonga mbele au nyuma?

PAKACHA NA WENGINE,
Maneno KUSONGA NYUMA yasiwape taabu.
Maana ya neno SONGA kwa Kiingereza ni MOVE.
Hivyo nlimaanisha "MOVE BACKWARDS".
Unajua tena upungufu wa kiswahili.

Tuendelee na mada wakuu.

Kuhusu ZANZIBAR, Watu wengi walidhani kuwa, Muungano wake na TANGANYIKA ungezidisha maendeleo kwa kasi.
Nadhani walwaza vibaya.
Au siyo wakuu?

Kwa bahati mbaya hao wananchi hawakuulizwa wala kushauriwa bali walilazimishwa tu si ndio mapinduzi, mchafukoge!
 
Zanzibar ilikuwa na maendeleo wakati karafuu ina soko duniani baada ya soko la karafuu kushuka na uchumi wa Zanzibar ukashuka. Zanzibar ni nchi yenye rasilimali chache kulinganisha na bara kuanzia population na hata natural resources. Uchumi wa Zanzibar una sukumwa na utalii tu kwa sasa. Sasa jamani nchi kama U.A.E. ambao ni matajiri wa kufaa wana panua wigo wa soko lao leo hii Wazanzibar wali tegemea kuendelea na karafuu na utalii tu? Kama uchumi ulikuwa una tegemea karafuu na utali basi it was bound to fail Muungano or not. Blame it on a lack of vision kama Zanzibar imeshindwa kudevelop other industries na kama kweli Tanganyika ndiyo tatizo blame it on Zanzibar leaders who lack the courage. Ni rahisi sana kulaumu wengine hata kama unajua ufumbuzi ni nini. Complaining never got anyone anywhere na hata kwenye maisha ni vigumu kukutana na mtu yoyote mlalamishi mwenye maendeleo.

La msingi na kubwa ni kuwa Wazanzibari si walalamishi hata kidogo isipokuwa ni kuwa ukweli unakuandameni na hamtaki kuukubali.
Zanzibar ilitegemea Karafuu kwa maendeleo yake na kiasi kikubwa cha utajiri huo kilitumiwa vibaya katika mambo yasiyokuwa ya msingi yaliyohusisha Muungano likiwamo la kuunganisha vyama na vita vya Kagera.
Kuanzia hapo mambo yaligeuka na baada ya kushuka bei ya Karafuu viongozi wa Zanzibar walitafuta njia mbadala ya kuinua uchumi wa Zanzibar lakini kuwepo kwa hatamu za chama kushika hatamu chini ya CCM Zanzibar ilianza kupata vikwazo vya makusudi ili izidi kuangamia kiuchumi.
Kila jambo lilofanywa na Zanzibar kujinasua kiuchumi lilipigwa vita na ndugu zao wa Bara kwa kisingizio cha Muungano.
- Zanzibar ilitaka kuanzisha bandari huru ikapigwa chini na ndugu zao
- Zanzibar kwa kupitia soko huria ilianza kunawiri kibiashara kwa kupunguza sehemu ya kodi na watu kutoka sehemu zote Afrika Mashariki na kati walikuja kununua bidhaa ndugu zao wa Bara ikawachoma wakawafisidi
- Zanzibar ilpotaka kupokea misaada kwa maendeleo "serikali" ya Muungano itaweka vikwazo
- Zanzibar ikitegemea malipo ya visa kwa watalii wanaokuja Zanzibar "serikali" ya Muungano inakinga visa hizo hukohuko wanakotoka watalii
- Kwa kutumia bandari Zanzibar ikipokea bidhaa na kupata ushuru ndugu zao weakaingia chibni kwa chini ili kuhakikisha kuwa makontena yote yanaingia Bara.
Hiyo ni mifano michache ya jitihada zisizofanikiwa za Zanzibar kujiendeleza kiuchumi ambazo "ndugu zao" wamekuwa mbele kuzifisadi kwa kisingizio cha Muungano. SASA ipo haja ya kuuliza iwapo Zanzibar inaendelea au inarudi nyuma? NAHISI HII NI KEJELI YA MAKUSUDI.
 
zanzibar ingeangalia visiwa vingine vimefanyaje kupata maendeleo. Waangalie sehemu kama Monte Carlo, nk. Tafuta njia za kuvutia watalii, kama tax free zone, legalising gambling, nk


Zanzibar inahitaji kitu kimoja kikubwa nacho ni uhuru wa kujiamulia lipi linalowafaa, maendeleo kwa Zanzibar ni kitu cha muda mfupi hata hakuhitajiki matendo machafu kwani hapo Zanzibar ilipokuwa na maendeleo ilikuwa na mamlaka yake.
 
Visiwani wamebaki tu walalamishi hata kazi wameacha..wapo vijuweni tu wanalalamika!

Nidhamu tu ya kazi ..wandugu! Kama Opportunities ni kidogo..kwa bara si mnakaribishwa??

Hamna mandeleo yanayoletwa kwa kulalamika tu saa zote! Kazi kwanza!!!
 
It is easier to blame one's failures on another person. Instead of talking the talk they should walk the walk.


It is funny that we do not ask about Mwanza or Kigoma aren't they of the same status in regard with sovereignity or we do apply double standard?
To some issues Zanzibar is a part of Tanzania and in some issues that are unpleasant we distant ourselves with Zanzibar.
 
1. Kodi gani Mkuu bara inakusanya Visiwani kwa Uchumi mdogo hivyo??

2. Mwansfalsafa1 amesema vema: vision, hardwok and diversification! Sasa kunaguka kwa bei ya Karafuu utalaumu Bara?

Hata hivyo ndugu zetu wa Viswani wanakribishwa Bara kama Bakresa na wale Wapemba kule kariakoo kuna opportunities nyingi..na soko kubwa!! Sioni haja ya kuendelea kulalamika!

High time tukapunguza kulalamika!

1.Kwani fisadi anajali udogo wa alichonacho mwenziwe? Unahitaji somo bwana mdogo kuuelewa ukweli. Kwani wale waliokuwa wajija kwa boti ya asubuhi na kurudi na mapato kwa boti ya jioni hujawasikia?
2.Kuanguka kwa bei ya karafuu ni sawa na kuanguka kwa bei ya Pamba au kahawa lakini wenzetu mko huru kutekeleza shughuli nyengine za kiuchumi lakini kwa Zanzibar choyo chenu kinazuia kila jitihada.
Kuhusu Baharesa na Wapemba mmewakaribisha kwa kuwa walikuwa na pesa zilizotokana na hiyo Karafuu na mnawaona ni chachu ya maendeleo yenu kwani wanalipa kodi nyingio na kuwapatia ajira.
 
mbaazi ikikosa maua usingizia jua. Wazanzibar wengi tunalalamika hata kwa yale yasiyopaswa kulalamikiwa. Ebu angalia kwa uchache tu.... Tanganyika ina mali nyingi sana kama dhahabu, almasi, kahawa, katani, pamba, gas asilia n.k ... wakati kisiwani kwangu zanzibar tulitegemea sana zao la karafuu na bandari kwa uchumi. Hivi vyote vimekosa soko la kimataifa na mitaji ya uendelezwaji wa bandari. Ukiangalia kwa undani ukwepaji mwingi wa ushuru ufanywa zanzibar ... sasa mtaendeleaje? Soma taarifa ya CAG ya kuanzia 2006 utaona matatizo yenu. Jamani tusilaum wengine kwa matatizo yetu wenyewe

Naamini hu Mzanzibari au pengine hu muelewa wa mambo. Hiyo bandari na kipato mbona kilinawiri hadi pale zoezi lilipopigwa STOP na hao wafadhili wako?
Naamini wewe si mzanzibari kwani CAG ni kitu gani kwa Zanzibar? Hiyo ilkuwa janja yao kwa kutumia TRA ili kuiangamiza Zanzibar. Inashangaza kuwa kulikuwepo kukwepa ushuru lakini Biashara ilinawiri na sasa pasipo na kukwepa ushuru Wafanyabiashara wote wamehamia Bara, Jee huko ndiko kwenye kukwepa ushuru kwa sasa?
UKIAMBIWA UJIAMBIE
 
Zanzibar -wazanzibar ni WAVIVU...Period!!!wapi ulishaona nchi ya wavivu ikaendelea???Angalia hii takwimu:::asilimia 95% ya wazanzibar waishio UK wanaishi kwa benefits,asilimia 90% ya wazanzibar wote waishio Europe wanaishi kutegemea benefits.
Sasa mlishaona wapi nchi ya wa benefits ikaendelea????Na wakibahatika kupata vijisent wanajenga bongo sio kwao madongo kuinama Pemba.
Habar ndo hio......

Jee unao uelewa kuwa Wabara wanamiminika Zanzibar na kwa bahati mbaya si wawekezaji? Sasa jiulize Taifa la watu hodari wanakwenda kwa wavivu wanakwenda kufanya nini?
Jee umuelewa kuwa hakujawahi kufa mtu kwa njaa kule Zanzibar kwenye wavivu na huko kwenu mlio mahodari hadi hii sasa hivi kuna tishio la njaa baadhi ya sehemu?
Ama kwa utafiti wako sijui una ukweli kiasi gani lakini bahati mbaya kuwa wewe mwenyewe huaminiki kwa vile ni MUONGO.
 
Wajameni siasa nzuri na ipendeza kama unakuwa na wasiasa walio committed lakini kwa siasa zetu za bongo hizi bado tuna wasiasa wanaopenda umaarufu kwa kuzungumza kwa vinywa vyao bila kujali maslahi ya taifa/ wananchi. Hawa wenzetu wa zanzibari wana wanasiasa wadanganyifu!!!
 
Sasa unabisha au unatukana????jaribu shuka kidogo hapo london,UK....elekea Barking mahala wanapoishi wengi then chukua sample ya wazanzibar 10,NAKUHAKIKISHIA 9 WANAISHI KWA BENEFITS.Bado wabisha!!!!!!!

Sasa tuwaite nyie wazungu wa unga? Kwani ukienda Pakistani asilimia 99 ya Watanzania wanaojushughulisha na unga ni Wabongo.
Nafikiri wewe na hao mlio nje sikigezo cha Mtanzania au Mzanzibari kwa vile hamko pamoja nasi bali nyie ni mlioshindwa kuukabili Utanzania wenu
 
Mkuu lakini Zanziba si ina forodha yake yenyewe ya ushuru? Zanzibar pia si ina serikali yake? Sasa kweli kama serikali ya Zanzibar imeshindwa kusimamia mambo yake ilaumiwa Tanganyika? Na hata kama unacho sema ni kweli basi viongozi wa Zanzibar ni wazembe. Mwizi akiiba wakati mlinzi kalala utamlaumu nani? Huku kuilalamikia Tanganyika kila kitu ndiyo kutafanya Zanzibar isi tafakari nini haswa chanzo cha matatizo yake. If you come down to it Tanganyika is not the problem.


Yaani inaonyesha hutaki kuuelewa ukweli. Ukweli ni kuwa Zanzibar haina nafasi ya kujiamulia mambo yake.

Nakushangaa kuilaumu Serikali ya Zanzibar, hebu nikupe mtihani mdogo tu. Jee unasemaje na uamuzi wa Serikali ya Zanzibar kutaka Mafuta yasiwe ya Muungano?
 
GoZ slams donors

Zanzibar government called upon the donor community to go to Pemba and witness the real condition there instead of depending on hearsay and issuing statement that might aggravate the situation. It said such statement can precipitate trouble at a time when CCM and CUF have already reached an agreement on issuance of Zanzibar ID and registration of voters. The government said this following a statement by embassies of EU countries plus the USA, Canada, Japan and Norway, urging the government to make sure that all citizens, including those from Zanzibar, are given the right to vote.

Speaking over a phone, the Director of Zanzibar ID, Mohamed Juma Ame, said he was surprised by the EU statement given that the situation is already under control. “My office does not work under pressure from anyone or any party; we are guided by 2005 Act. These EU countries should watch what they are saying otherwise they might make the volatile situation worse. In any case I got only four appeals from people who feel aggrieved,” Ame claimed.

Wete DC, Omar Khamis Othman said the EU statement hampers attempts made by his office, ID department, political parties and other stakeholders. “What they want to see is disorder in Pemba. Journalists should tell them the truth so that they are not misled into creating unrest. Alternatively, they can ask for clearance to come to Pemba to see for themselves instead of depending on unreliable reports,” Othman said.

Director of Zanzibar Electoral Commission (ZEC), Salim Hamis Ali said they were expected to meet yesterday to discuss the current situation, including the statement by donors. If necessary a reply might be issued, he said. “So far we have not cleared the donors to come to Pemba, so it is surprising that they complain about something they haven’t seen. It would have been better for them to come or send their diplomatic staff to Pemba and then talk. The fact is that on Monday we are to meet CCM and CUF leaders in Wete to discuss the stage reached so far and the way forward,” Ali said.

Minister of State in Chief Minister’s Office, Hamza Hassan Juma said: “We would like the heads of diplomatic missions and their officers to go to Pemba and see the real situation. Instead of sitting in their offices in Dar es Salaam, let them come and see how we resume registration on Monday” Talking to reporters in his office yesterday, the Minister said: “Diplomatic missions should not interfere in internal matters as Zanzibar government follows the law and constitution. It is surprising that government has not received any statement from them. They should have contacted us to get the truth instead of listening to the other side. Let me emphasis that we will always respect the rule of law and good governance but we shall never be pushed around by EU or AU.”
He accused the opposition leaders of creating an atmosphere that led to suspension of registration. The Minister named Secretary General of CUF, Seif Sharif Hamad, saying he uttered provocative statements at CUF rallies.

Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Seif Idd told reporters: “We are disappointed by the donors’ statement since we already warned them against meddling in internal matters. They still persist. We shall continue urging them to stick to their job and do what they are supposed to do. Of course they provide us with funding but that doesn’t allow them to cross the line. If they see anything untoward they can always approach us at the Ministry instead of rushing to the press. We are not entirely amused by this type of behaviour”.

Meanwhile, Chairman of the CCM youth wing (UVCCM), Hamad Masauni told the donors to stop meddling in matters that “don’t concern them” and investigate before speaking out. He also told CUF to stop feeding wrong information to the donors ‘as they always do’. Talking to reporters in Dar es Salaam, Masauni said: “UVCCM condemns the act by some embassies issuing a statement without investigating, an act that is likely to cause breach of peace. They have to know that colonial era is over so UVCCM will not tolerate such behaviours by these white foreigners. Our parents fought for independence so that we can exercise our national sovereignty. Now they want to take us back to colonialism. They sit in their offices and listen to what CUF tells them and then come out with a statement” (Majira, Mtanzania, Habari Leo, Mwananchi, Tanzania Daima, Kulikoni, Nipashe)
 
Junius,
Mkuu nimekuelewa ila mie nimechukulia majority yao huko Uk/Europe kwa hivyo basi unavyosema na wabara wako vile kwangu mie hao ni Minority.Wabongo (Bara) wanajulikana na wanasfika na waafrika wengine kuwa ni wachapa kazi.Suala la uvivu hilo halina mjadala....angalia maendeleo tulio nayo bara then linganisha na Unguja/Pemba kwa ujumla wao.
Nawakilisha mkuu.


Kuna suala umeliacha na hilo ndio hoja kubwa. Jee tunawahukumu wazazi na ndugu walioko huku kwetu kwa matendo yenu huko?
 
Hatima na mustakabari wa Zanzibar hipo mikononi mwa Wazanzibar wenyewe...!
Enzi ya M'Mungu kuleta mitume imeshakwisha. Akili wanayo, siasa wanazijuwa, niya wanayo, sababu wanazo, uwezo wanao.

Swali linakuja... Wapo tayari kukaa pamoja na ndugu zao wa upande wa pili wa visiwani? Maana tumeshuhudia mengi sana jinsi wanavyo watetendea ndugu, jamaa na marafiki kutoka upande wa pili wa Zanzibari.

Hilo mnalikuza kwa sababu zenu lakini ukweli ni kuwa Zanzibar, Pemba na Unguja ni kitu kimoja.
Mnachokiona ni jitihada zinazotakiwa za kuwekana sawa katika kugawana mapato na hilo mbona hata bara lipo si tunasikia minongono ya uchaga, uhaya ukusini ,upwani na kadhalika.
 
Hizi habari za CUF zimepitwa na wakti......kwa kifupi Zanzibar hawaendi mbele wala hawarudi nyuma na pia hawako pale pale, bali wanaruka ruka mbele na nyuma kutafuta sababu pa kutokea lakini ndo hivyo tena wameshindwa.HATOKI MTU HAPA WALISHASAINI PAPERS KWA HIO LAZIMA KIELEWEKE HAKUNA PA KUTOKEA IMEBAKI KELELE ZA WAPANGAJI.........

Ulipofika huko UK ulikaribishwa nyumbani kwao na wakaku..., walikuibia mpenzi wako nini, walikuwekea kauzibe nini, au ,au,...... Kwa kweli bora ungeweka tatizo lako pahala pengine na sio hapa.
 
Visiwani wamebaki tu walalamishi hata kazi wameacha..wapo vijuweni tu wanalalamika!

Nidhamu tu ya kazi ..wandugu! Kama Opportunities ni kidogo..kwa bara si mnakaribishwa??

Hamna mandeleo yanayoletwa kwa kulalamika tu saa zote! Kazi kwanza!!!

DUH Mzee unanitisha sana Yaani hata chakula chao kinatolewa bure kutoka bara?
Nakubaliana nawe kwani pale mnapongangania vita juu ya ufisadi wakati Chenge, Lowasa,Manji, Rostam na wengine wanaendelea na nyie mnapiga domo tu au sivyo?
 
Zanzibar haiwezi kushindana na Tanganyika kwani hata matumizi yao yanatokana na Bajeti zinazopitishwa na nchi za ulaya ,marekani na Asia kwa ajili ya maendeleo yao.
 
Zanzibar haiwezi kushindana na Tanganyika kwani hata matumizi yao yanatokana na Bajeti zinazopitishwa na nchi za ulaya ,marekani na Asia kwa ajili ya maendeleo yao.
Astaghfirullah. hivi ni nani wanaotegemea zaidi kutoka (sadaka, ruzuku au hisani za Nje) Ni Zanzibar kweli? na siyo Tanganyika ilivyofanya mbinu na hila za kuchukua kilicho-kingi kupindukia kati ya kile Tunachogaiwa Tanzania?
 
Back
Top Bottom