Je, zawadi inalipiwa ushuru?

Je, zawadi inalipiwa ushuru?

Konzogwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
434
Reaction score
156
Nawasalimu wanajamvi?
nimepewa zawadi ya gari na inatumwa tokea Japan. naomba mwenye kujua,.. je zawadi nayo hulipiwa ushuru kama ilivyo kwa magari mengine yaliyonunuliwa?
 
kwani hiyo Zawadi haina thamani
 
Waambie wakutumie pesa za ushuru, vinginevyo litapigwa mnada
 
Mara nyingi zawadi hasa gari ni kitu cha thamani.
Usishangae ikawa zawadi ya kukutia umaskini.
Halafu ukiangalia hiyo pia sio kama zawadi kivile,maana mwisho wa siku wewe mwenyewe unalipia karibia robo ya bei walionunua kama kodi.
 
Aisee... Isingekuwa inalipiwa Ushuru kila mtu anayeagiza gari angeweza kudai amepewa zawadi....!
 
Nawasalimu wanajamvi?
nimepewa zawadi ya gari na inatumwa tokea Japan. naomba mwenye kujua,.. je zawadi nayo hulipiwa ushuru kama ilivyo kwa magari mengine yaliyonunuliwa?

Kuwa zawadi hiyo ni private issue.....mi nafkiri ushuru utabaki palepale japo sina ujuzi mkuubwa na importation..!
 
nawashukuru wanajamvi. sasa nimeshajua kuwa nahitajika kulipa ushuru ila nabaki kujiuliza sijui itakuwaje kuhusu calculation zao maana unakuta wanacalculate ushuru kulingana na fob/cif price kutoka kwenye invoice. sasa invoice hamna miongoni mwa documents zilizotumwa. anyway ngoja nijipange tu kukabiliana na kitakachoibuka. asanteni sana.
 
Kuhusu invoice wala hakuna tatizo uwa wana makisio yao ambayo yaweza kuwa juu au chini ya actual cost.
 
nawashukuru wanajamvi. sasa nimeshajua kuwa nahitajika kulipa ushuru ila nabaki kujiuliza sijui itakuwaje kuhusu calculation zao maana unakuta wanacalculate ushuru kulingana na fob/cif price kutoka kwenye invoice. sasa invoice hamna miongoni mwa documents zilizotumwa. anyway ngoja nijipange tu kukabiliana na kitakachoibuka. asanteni sana.

Mkuu watakupa custom value yao kulingana na kumbukumbu zilizopita.
Kuna vitu wanaita HS CODE ...nadhani mule mule...
 
Back
Top Bottom