Mkuu Mkandara,sincerely the chances these people( Zitto and other leaders)getting together is really slim.this is because Zitto haonekani kama anataka kutafuta suluhisho bali anaonekana kama mtu ambaye anajaribu kuonyesha nani zaidi kati yake na viongozi wengine wenye mawazo tofauti na yake ndani ya chama.
Big lie, Soon baada ya Zitto kukubali kujitoa akaanza kufocus ni jinsi gani ya kuweza kufanya kazi na Mbowe. Whata happen wapambe wa Mbowe wakaona kujito kwake ni sign ya weakness na wakajikusanya wote kutumi resources zilizolengwa kujenga chama kuanza kumattack Msaidizi wa Zitto eti kumuonyesha siasa lakini pia kuonyesha kuwa Zitto hana base ndani ya chama. Ndipo Zitto alipopata taarifa hizo na kuzithibitisha akaamua kuanza kumfanyia kameni ya wazi Kafulila btn 11pm hadi mchana wa siku inayofuata na kumhakikishia ushindi Kafulila dhidi ya mgombea ambaye wanaoijiona ni maadui wa Zitto walikuwa wakimfanyia kampeni.
Mfano,toka kuanza kwa malumbano yake na viongozi wengine ni Zito pekeyake amekuwa akiongealea tofauti zao kwenye vyombo vya habari.sijamsikia kiongozi mwingine wa CHADEMA akiongelea matatizo ya ndani ya chama kwenye vyombo vya habari,kuanzia mbowe,dr.slaa,mnyika na viongozi wengine.
Haikutosha sio tu kulazimisha matokeo kutolewa lakini pia siku ya pili viongozi wenzake wakiongozwa na Slaa ambaye alilishwa majungu wakaanza na kwa kutumia vyombo vya habari kusema kuwa kuna vijana wanatumiwa na mafisadi na kutoa rushwa katika uchaguzi huo wa vijana wakimlenga Zitto.
Haikutosha, wakaanza kumzodoa mama yake mzazi ambaye ni mwanchama mwanzilishi wa CHADEMA tangia enzi 1992 wakati ambao wengi wa hao wanaomzushia ama walikuwa nyumbani kwao CCM ama bado wanalazimishwa kwenda shule (nachelea kutumia neno vinuka.....). Hapo ndipo Zitto akaamua kuwatumia ujumbe kuwa hayuko tayari kuona wanamfanya kama ambavyo waliwafanyia viongozi wengine ambao walitofautiana nao.
nimekuwa nikimwamini Zitto kwa muda mrefu sasa ila kwasasa am highly conviced kwamba kuna watu ambao wanamtumia ili kuua CHADEMA.Ukijaribu kukaa chini na kufikiria kwa undani utagundua kwamba Zitto is not himself,kwa mambo ambayo amekuwa akiongelea na ku-support within these few months utagundua kwamba huyu Zitto wa sasa sio yule tuliyemjua kipindi cha nyuma.Mfano,kwanini amekuwa yuko againsnt na viongozi wenzake kwenye kila jambo recently?haiwezekani kwamba Zitto yuko smart kuliko viongozi wengine ambao wamemzidi kielimu,kiumri,upeo wa siasa,na mambo mengine mengi tuu.
Kama ulimwamini Zitto pale tu alipokuwa akifanya yale unayoyaona wewe tu kuwa ni muhimu na sio anayoyaona yeye then kweli ulikosea pa kuweka imani yako.
Na pia kama kutofautiana na viongozi (chama) chake ndio ushahidi wako wa kukuhakikishia kuwa Zitto anatumika then nakushauri pia uache kuwashabikia kina Sitta, Mwakyembe na wengineo ambao wanatofautiana na viongozi na wenzao wa CCM.
Zitto ni kiongozi ambaye anafikiri siasa kwa upeo tofauti na tuliouzoea ama tunaolazimishwa kuuzoe. Siasa za ukasuku na upigaji kelele hata kama taarifa za kitaalamu zinasema tofauti. Zitto ni smart ndio maana anaamini kuwa ili kushinda CHADEMA hakipaswi kuendelea na taswira ya VYAMA PINGA ambavyo kwao ni kukosoa kila kitu na kukaa pembeni kutofanya any constructive politics hadi hapo watakapopewa madaraka. Kwa hulka ya watanzania itabidi msubiri sana kwa vyama vyenye muonekano huo kuchukua madaraka. Zitto amethbutu kutumia style tofauti na ndiyo ambayo wenzake wengi wazee kwa vijana wanashindwa kumuelewa na kuanza kujenga fikira potofu dhidi yake kama mlivyo wengi wenu hapa.
Zitto ni mchanga sana kisiasa,hana upeo wa kuona mbali japokuwa ana elimu ya chuo kikuu,ni mtu asiye changanua kwa undani jambo kabla ya kutoa uamuzi,
Kama una maana ya kuwa mchanga na asiye na upeo wa siasa majitaka, hovyohovyo na fisadi tulizo na tunazolazimishwa kuzizoea then ur right 100%. Lakini kama ni kwa muono mwa siasa endelevu zenye vision ya kujenga siasa makini na effective then ur wrong 100% kumuona kuwa ni mchanga na asiye na upeo. I bet he reads, learn and strategies 100% more than u.
mpenda sifa,mtu asiye na shukrani,mtu asiyekumbuka alikotoka na watu waliomfikisha hapa alipo leo, mbinafsi ambaye anajifikiria yeye mwenyewe na maslahi yake pasipo kuangalia yana madhara gani kwa chama chake na wananchi wa tanzania kwa ujumla.
Hii ya mpenda sifa inanifanya nijiulize kama wewe sio CCM maana this is typical them. Kila kukicha kila anayesema machafu yao huitwa mpenda sifa nad so is Zitto, Slaa na wengineo.
Mtu asiyekumbuka anakotoka, hii inaonyesha kuwa humjui Zitto na ni mmoja wa wale wanaojenga mitizamo yao kwa kutumia taarifa hovyohovyo za wahandisi wetu wa habari. Mbinafsi, as i said b4, ask even his worst enemy atakuambia ni vipi Zitto mtu wa kujitoa kwa wengine.
Kama unadhani kutaka kubadilishana uongozi wa chama na Mbowe kunamfanya awe anajifikiria mwenyewe na maslahi yake zaidi ya chama na nchi hata hata aliojiweka katika hali mbaya kisiasa kwa kukubali kujitoa na kuonyesha kuwa hana msimamo, then subiri time will tell....
Actually maamuzi yake mengi yanalenga na kuona mbali zaidi ya hao wenzake walio tayari kuvunja chama ili mradi waendelee kulinda nafai zao za uheshimiwa.
..kama kweli alikuwa na nia njema ni kwanini asiwataaritu viongozi walioko juu yake kuhusu kusudio lake la kugombea nafasi ya uenyekiti?ok,kama kulikuwa na kutokuelewana baina yake na viongozi walioko juu yake basi atleast kabla ya kugombea angewafuata wazee wa chama ili wamshauri.
Kwa mtazamo huu ndio maana nasema wengi wetu ni wachukia CCM tu na sio wanademokrasia, wapenda maendeleo wala wataka mabadiliko.
wana JF lazima tukubali kuwa baraza la wazee la CHADEMA limeundwa na watu wasomi na wenye upeo mkubwa kisiasa na kiuchumi ukilinganisha na Zito ambaye ameanza juzi.
Tehetehe....sitasema mengi hapa ila tu nakuambia kuwa hata hao wachche wenye vyeti vingi haviwezi kuwafanya kuwa wana upeo mwingi kama wanapoingia katika siasa ama nafasi za uongozi wanaacha utamaduni wa kujisomea. fanya utafiti wako kuhus Zitto na suala la kujisomea ujue kama kweli hana upeo na wenzake wengie wamemzidi....
yeye akiwa kama naibu katibu mkuu kwanini aunde kundi lake la upinzani ndani ya chama badala ya kukemea na kutokomeza mambo kama haya ndani ya chama ili kukiimarisha chama?Najua hapa JF kuna wapenzi wengi wa Zitto,lakiniwengi wao ni washabiki tu ambao hawachukulii mambo kimaanani na kwa uzito unaotakiwa..wanaongea mambo ambayo hayana msingi na kulaumu mambo wasiyoyaelewa kiundani.
Moja, Zitto hajawahi kuunda kundi lake na kama kuna makundi ndani ya CHADEMA sio kundi la Zitto Vs Mbowe ali ni kundi la Mbowe Vs kundi la wanaompinga Mbowe abalo limeanza muda mrefu na kukuzwa wakati wa saga la Chacha na sasa kumshurutisha Zitto kujitoa.
Pia, angalia isije ikawa wewe ndio mshabiki tu ambaye hachukulii mambo kimaanani na uzito unaotwakiwa...
k
abla hujashabikia mtu fulani tafadhali tafakari kwa makini hali halisi ya mambo yanayojiri nchini kwetu halafu tafakari ni kwa kiasi gani wananchi wameamka kimawazo.utagundua ni kwa kiasi gani watu wamechoka na uongozi wa serekali yetu na kiu yao ya mageuzi.Sasachama tawala wanaona hatari iliyoko mbele yao kama hawatabadilisha mambo haraka.Njia yao kubwa ya kurudisha imani na matumaini ya wananchi juu ya chama tawala sio kuwajibika na kurekebisha makosa yao bali kudhoofisha vyama vingine vilivyoanza kujenga imani kwa wananchi.Kwahiyo mpango wa CCM sio kuondoa mafisadi bali ni kuondoa wale wote wanaopinga mafisadi.CCM wana nguvu na pesa ya kukamilisha madhumuni yao hivyo wanaingia kwenye vyama vya upinzani na kujaribu kuwasifia na kuwaweka karibu wale viongozi wa upinzani ambao ni tishio kwao.wanawapa vyeo,mishahara na marupurupu mengi na kujidai kuwa-support.hii yote ni kujaribu kuwa mastermind ili kuwamaliza.sasa kwa viongozi wa upinzani ambao ni wana tamaa na walafi wa madaraka na umaarufu wanategwa kirahisi tuu kwa mitego kama hii.wanakufa na kuua vyama vyao kisiasa.. sasa ni lazima tujiepushe sana na viongozi wa aina hii manake watatupeleka pabaya..kila unapoona kiongozi mmoja anakuwa always against majority kwenye issues ambazo ni sensitive lazima ukae chini ujiulize ni kwasababu gani.
Acha kutumia CCM kuficha makosa yako. CHADEMA walipewa chance ya mwaka kujijenga lakini wao wakaitumia kujiharibia.
tukumbuke usemi wa Mwalimu Nyerere,"UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU".GOD BLESS US ALL!
Masikini mwalimu. hata maadui na wasaliti wake wanamtumia kuhalalisha maovu yao.....
omarilyas