Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

This is bigger than Zitto, this whole saga exposes how disorganized the entire party is.
 
Huyo mama kiherehere tu. Mbona hatumsikii mama yake mbowe. Waswahili kudandia hitma balaa!
 
This is bigger than Zitto, this whole saga exposes how disorganized the entire party is.

A party is organized by individuals, if it is disorganized it is due to these people and in this case one of them is Zito. His bigheaddness is a root-cause to this saga. Being called Obama of Tanzania made him think he had reached the helm of Bongo politics. He may get sympathizers but the dude is done. Luck for him he is not like Mrema by that at least he is schooled , though at this pace his education may not be useful.
 
Duh...kumbe Zitto ndani ya Chadema yupo na Mama yake pia.
Sio yupo na mama yake,ikiwa wewe mama yako amekufa hilo ni suala jingine lakini ikiwa yupo hai basi anakutazama kama mwanawe na kwa jambo lolote lile anayohaki ya kusema au kukulinda kwa muda wote wa uhai wake kama mama.

Kama mzazi kwa mwanawe ,anazo hisia na yapo anayoyasikia kutokana na mambo ya siasa na pengine ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania na vituko vyake, mama huyo hakukosea kabisa na ameonyesha umahiri wa mzazi.
 
He may get sympathizers but the dude is done.
Uuuuugh! that's Heavy...Mkuu, I don't think this healthy for both of us..it's not the right dose we need right now.. We gonna walk through this both of us. Ain't worried any of this will tarnish Zittos political legacy as long he acknowledge errors/ mistake, whatever U may call in his judgment.
On the other hand Chadema as a party they should come together, correct all mistake of letting every big mouth scumbag talk on their behalf.. All public anouncement, addresses must go through approval and mister Katibu should stand firm on his ground..Wazee wakae pembeni kabisa esp. when issue relating their family members..
As I said it before, Sneetch is the liability to hte party...he should never build confidence over that..repeating his assertion that there isn't nothing wrong or sinister in backing the purchase of Dowans generators or promote political rivals within the party for what he call one man war against the elites...this is bad judgement! It won't get him anywhere but crush him Politically....
Only doing big things for the party and the Country is what really counts, it makes your legacy worth to be remembered for...Hope he got the message, Chadema regroup and Inshaallah will come through all this..
 
akiendeleza sera za madaraka na kugombania madaraka atakuwa hana tofauti na viongozi waliopo kwenye government yetu kwa sasa....amenidisappoint sana..hana tofauti na wale..

Hivi ni lini na wapi ambapo Zitto ameonyesha kugombania madaraka? Hata siku moja Zitto hajawahi kulazimisha wala kuomba madaraka CHADEMA isipokuwa nafasi za kuteuliwa. Leo hii ameamua kutumia njia ya kidemokrasia kuomba apewe nafasi ya kuomba kutumika kama mwenyekiti mmemzuia na akakubali bila ya ubishi wowote. Tena mara tu aliposhauriwa/shinikizwa hajachukua hata masaa 24 kukubalia matakwa ya Wazee wa busara.

Lakini still wale wanamuona adui wao wakaona bado haitoshi na wakaendelea na mpango wao kumuua kisiasa na ndipo naye akaamua kujitokeza wazi kumpigia kampeni msaidizi wake wa karibu ambao anaonekana kama adui wa wanaojiona wana haki zaidi ya wengine kuwepo CHADEMA wakati wengi wao ni Zitto ndiyo alikuwa mwenyeji wao wakati wanajiunga huko. Wengine wakitoka CCM lakini wanaishia kujiona wao ni wana CHADEMA haswa na Zitto ni pandikizi. Yaani pandikizi lilopandikizwa likiwa miaka kumi na sita?.Amejiunga na CHADEMA wakati ambako hao wanaomuita pandikizi walikuwa hata ofisi za CHADEMA hawazijui zilipo.

Propaganda kama hizi ndio zilezile cut and paste za CCM ninazosema. WApo tayari kuuwa chama na hata kuangamiza nchi kwa ajili ya kulinda nafasi zao za uheshimiwa halafu wanakimbilia kuwaita wale ambao wanatumia njia halali kabisa za kuomba ridhaa ya wanachama/wananchi kuomba kura zao kama wenye kugombania madaraka.

Zitto amechukua hata hatua ya kuwasihi wafuasi wa marehemu Chacha na wengineo waliokereka na shinikizo la yeye kujito kuacha mpango wao wa kupiga kura za maruhani dhidi ya Mbowe kwa manufaa ya chama kwa kuhakikisha Mwenyekiti wake anapata uhalali wa kutosha kuongoza chama lakini still wanakuja watu wasio na soni wala hiyana kumshutumu kuwa anagombea madaraka.

Kuna kiongozi mmoja hivi karibuni aliniambia hivi, ninanukuu.."Zamani enzi za ujamaa viongozi walikuwa wanajengwa, siku hizi (enzi za unyang'au) viongozi wanabomolewa"

Tuyafanyao leo kufurajisha mioyo yetu na maslahi ya wachache mnaodhani kuwa ndio viongozi wema kwenu tutayakumbuka very soon na kuyajutia....

omarilyas
 
Hii ni heshima gani mnayoonyesha hapa JF kuhusu mama yake Zitto maana ikiwa mengine yatachambuliwa basi ni matusi ,sijui moderator yupo na kama anaweza kufuta basi hii topik nzima imepoteza uhalali wa kuwepo hapa JF.Na pengine hawa ndio wanachama wa Chadema walivyo ,kwa kweli hata heshima ya Chama hapa haipo na kinachoonekana ni ukosefu wa adabu tu,hivi wa Chadema ndivyo mlivyo ?
 
Erick Ongara,thanx for your post.umefafanua kwa undani hali halisi na natumaini kila mwana JF ambaye anaakili timamu za kufkiria jambo kwa undani atakuwa amekupata.kuna watu hapa ambao wataoa mawazo yao wakilalia zaidi kwenye ushabiki wa mtu mmoja mmoja.

Hii tabia ya kutuma post halafu unarudi na sura kivuli kuisifia? Mhh


mfano kuna watu ambao wanamshabikia zito as a person na sio zito kama CHADEMA.zito kama zito is nothing,he is who he is now kwasababu ya CHADEMA.Mambo yote ambayo amefanya na kumletea umaarufu aliyafanya kichama,i mean CHADEMA walikaa kama chama,wakapanga mikakati then wakagawanya majukumu na vitu vya kuongea public na bungeni kwa wabunge wao(this include slaa,zito,the late chacha wangwe,na wengineo).kwahiyo wakuu lazima muelewe wazi kwamba issue zote ambazo zito alikuwa akizitoa bungeni zilitoka kwenye chama chake na yeye alipewa aziwakilishe bungeni.

First,unapaswa kujua kuna mamilioni ya watanzaniaambao wapo nyuma ya Zitto wakati sio wanachama wala mashabiki wa CHADEMA. Hivyo wakitokea watu kumshabikia as a person haiwezi kuwa kosa. Tusilete udikteta wa kivyama hapa na wala tuache unafiki wa kuwalazimisha watu kushabikia chama kwa kazi za Zitto wakati kila kukicha chama (uongozi) hichohicho kinaonyesha taswira ya kumuona kama sio mwenzao.

Pili, si kweli kuwa yote anayoyafanya Zitto ambayo yamemjengea umuhimu katika jamii yametoka katika chama. Zitto amekuw akifanya mengi ambayo ndio yanayojenga jina la chama nje ya mitandao ya chama. Hata Buzwagi ni Zitto ndio alilipeleka chamani na sio vinginevyo. Na hata Buzwagi ilipompa umaarufu Zitto kwa makusudi kabisa alikaa kwa nyuma na kuwaacha wakubwa zake Mbowe, Slaa, Hamad Rashid hadi Mrema kujijenga huku yeye akitoa msaada wa karibu.

Ni personal network ya Zitto ambayo wengi chamani hawakubaliani nayo na hadi kufikia kuitumia kama kithibitisho kuwa Zitto anatumiwa na maadui zao ndio inayomuwezesha Zitto ama kupata habari ama kuhakiki taarifa nyingi ambazo ndizo huja kutumiwa na wakubwa zake kujijengea jina wao na chama kwa ujumla. Ni uongo, uzandiki na ujinga mkubwa kutaka kudanganya umma kuwa eti mambo yote anayoyasimamia Zitto yanatoka ndani ya chama. Yapo baadhi lakini sio kweli kuwa yote huwa anapewa Zitto wakati yeye ndiye huw anaypeleka chamani. Yapo mengine hata chama hicho hicho huamua kuyafunika halafu mnakuja hapa kuleta uongo kwa nia ya kumfitinisha.

adala ya kutumia nguvu zetu kumfunika Zitto nawashauri kuwa makini kutumia umaarufu wake, ujanja wake na haswa network yake kuendelea kuandaa ushindi wa 2010. tofauti na hilo ni ninyi ndio mtaishia kuwa wasaliti wa chachu na matumaini ya watanzania walioanza kuwajengea....

Zitakini kama ataanza mapema hii kujidai mjuaji zaidi na kulewa umaarufu ni dhahiri kuwa hatafika mbali kisiasa.atajiua mwenyewe kisiasa na pia kukiuwa chama chake. lazima ajifunze kuheshimu wakubwa zake kama kina mbowe,slaa na wengineo hata pale ambapo hakubaliani nao kimawazo.

Unanikumbusha baadhi ya mila na desturi za utamaduni wa kikandamizaji uliojijenga katika Tanzania yetu. M unapokuwa pro-active unaambiwa mjuaji. Mtu unapokuwa tayari kujitoa muda wote kwa faida ya wengi unaambiwa unajipendekeza. Mtu unapoamua kusimamia haki yake anaambiwa ana kiburi. Ni wapi Zitto hakuheshimu wakubwa zake. Yaani kutaka ridhaa yao ya kushindana na mwenyekiti wake tayari imeshakuwa ukosefu wa heshima? Si Zitto huyuhuyu ambaye alipoombwa/shinikizwa na wazee hao hao akakubali kujitoa?

Hii mijiwazo inatufanya wengine kuchoka kabisa. Kama mbadala wenyewe ni huu uligubikwa na mawazo ya ki-CCM why should we bother with it wakati kuna JINAMIZI tulijualo (CCM) ambalo tunajua kuwa tukiliabudu halitatula likatumaliza....

omarilyas


Zito lazima aache ubinafsi na afanye mambo kwa manufaa ya watanzania wote wenye mapenzi na CHADEMA.

Jarbu hata kuwauliza hao maadui zake wanaompiga vita na kumuendeshea kampeni chafu dhidi yake kama walakubaliana nawe kuwa UBINAFSI ni sehemu ya hulka ya Zitto?

kwa yeye kama naibu katibu mkuu kuanika mambo ya ndani ya chama sio kwamba ana saidia kukijenga chama bali anakibomoa na anajibomoa mwenyewe kisiasa.

Na wale wanaoamua kuvunja misingi mikuu ya demokrasia katika nyakati kama hizi ambazo watanzania wote wanapaswa kuamini kuwa chama chao ndio nuru ya demokrasia nchini haswa tukieleke katika uchaguzi 2010, hawakibomoi chama chao?

Na vipi wale wanaopita mitaani, majukwaani, mitandaoni na magazetini kumsema na kumuandika vibaya Zitto ambaye wanajuwa wazi kuwa uongozi wake na imani ya watanzania kwake ni msingi muhimu kwa mafanikio ya chama chao, jee hawabomoi chama chao?

omarilyas
 
Mkuu Mkandara,sincerely the chances these people( Zitto and other leaders)getting together is really slim.this is because Zitto haonekani kama anataka kutafuta suluhisho bali anaonekana kama mtu ambaye anajaribu kuonyesha nani zaidi kati yake na viongozi wengine wenye mawazo tofauti na yake ndani ya chama.Mfano,toka kuanza kwa malumbano yake na viongozi wengine ni Zito pekeyake amekuwa akiongealea tofauti zao kwenye vyombo vya habari.sijamsikia kiongozi mwingine wa CHADEMA akiongelea matatizo ya ndani ya chama kwenye vyombo vya habari,kuanzia mbowe,dr.slaa,mnyika na viongozi wengine.nimekuwa nikimwamini Zitto kwa muda mrefu sasa ila kwasasa am highly conviced kwamba kuna watu ambao wanamtumia ili kuua CHADEMA.Ukijaribu kukaa chini na kufikiria kwa undani utagundua kwamba Zitto is not himself,kwa mambo ambayo amekuwa akiongelea na ku-support within these few months utagundua kwamba huyu Zitto wa sasa sio yule tuliyemjua kipindi cha nyuma.Mfano,kwanini amekuwa yuko againsnt na viongozi wenzake kwenye kila jambo recently?haiwezekani kwamba Zitto yuko smart kuliko viongozi wengine ambao wamemzidi kielimu,kiumri,upeo wa siasa,na mambo mengine mengi tuu.Zitto ni mchanga sana kisiasa,hana upeo wa kuona mbali japokuwa ana elimu ya chuo kikuu,ni mtu asiye changanua kwa undani jambo kabla ya kutoa uamuzi,mpenda sifa,mtu asiye na shukrani,mtu asiyekumbuka alikotoka na watu waliomfikisha hapa alipo leo, mbinafsi ambaye anajifikiria yeye mwenyewe na maslahi yake pasipo kuangalia yana madhara gani kwa chama chake na wananchi wa tanzania kwa ujumla.Zitto amekuwa against na viongozi wenzake na amekuwa anafanya maamuzi pekeyake bila kuwashirikisha viongozi wenzake.mfano suala la Dowans na suala la kugombea uenyekiti..kama kweli alikuwa na nia njema ni kwanini asiwataaritu viongozi walioko juu yake kuhusu kusudio lake la kugombea nafasi ya uenyekiti?ok,kama kulikuwa na kutokuelewana baina yake na viongozi walioko juu yake basi atleast kabla ya kugombea angewafuata wazee wa chama ili wamshauri.wana JF lazima tukubali kuwa baraza la wazee la CHADEMA limeundwa na watu wasomi na wenye upeo mkubwa kisiasa na kiuchumi ukilinganisha na Zito ambaye ameanza juzi.yeye akiwa kama naibu katibu mkuu kwanini aunde kundi lake la upinzani ndani ya chama badala ya kukemea na kutokomeza mambo kama haya ndani ya chama ili kukiimarisha chama?Najua hapa JF kuna wapenzi wengi wa Zitto,lakiniwengi wao ni washabiki tu ambao hawachukulii mambo kimaanani na kwa uzito unaotakiwa..wanaongea mambo ambayo hayana msingi na kulaumu mambo wasiyoyaelewa kiundani.kabla hujashabikia mtu fulani tafadhali tafakari kwa makini hali halisi ya mambo yanayojiri nchini kwetu halafu tafakari ni kwa kiasi gani wananchi wameamka kimawazo.utagundua ni kwa kiasi gani watu wamechoka na uongozi wa serekali yetu na kiu yao ya mageuzi.Sasachama tawala wanaona hatari iliyoko mbele yao kama hawatabadilisha mambo haraka.Njia yao kubwa ya kurudisha imani na matumaini ya wananchi juu ya chama tawala sio kuwajibika na kurekebisha makosa yao bali kudhoofisha vyama vingine vilivyoanza kujenga imani kwa wananchi.Kwahiyo mpango wa CCM sio kuondoa mafisadi bali ni kuondoa wale wote wanaopinga mafisadi.CCM wana nguvu na pesa ya kukamilisha madhumuni yao hivyo wanaingia kwenye vyama vya upinzani na kujaribu kuwasifia na kuwaweka karibu wale viongozi wa upinzani ambao ni tishio kwao.wanawapa vyeo,mishahara na marupurupu mengi na kujidai kuwa-support.hii yote ni kujaribu kuwa mastermind ili kuwamaliza.sasa kwa viongozi wa upinzani ambao ni wana tamaa na walafi wa madaraka na umaarufu wanategwa kirahisi tuu kwa mitego kama hii.wanakufa na kuua vyama vyao kisiasa.. sasa ni lazima tujiepushe sana na viongozi wa aina hii manake watatupeleka pabaya..kila unapoona kiongozi mmoja anakuwa always against majority kwenye issues ambazo ni sensitive lazima ukae chini ujiulize ni kwasababu gani.tukumbuke usemi wa Mwalimu Nyerere,"UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU".GOD BLESS US ALL!
 
Mkuu Mkandara,sincerely the chances these people( Zitto and other leaders)getting together is really slim.this is because Zitto haonekani kama anataka kutafuta suluhisho bali anaonekana kama mtu ambaye anajaribu kuonyesha nani zaidi kati yake na viongozi wengine wenye mawazo tofauti na yake ndani ya chama.

Big lie, Soon baada ya Zitto kukubali kujitoa akaanza kufocus ni jinsi gani ya kuweza kufanya kazi na Mbowe. Whata happen wapambe wa Mbowe wakaona kujito kwake ni sign ya weakness na wakajikusanya wote kutumi resources zilizolengwa kujenga chama kuanza kumattack Msaidizi wa Zitto eti kumuonyesha siasa lakini pia kuonyesha kuwa Zitto hana base ndani ya chama. Ndipo Zitto alipopata taarifa hizo na kuzithibitisha akaamua kuanza kumfanyia kameni ya wazi Kafulila btn 11pm hadi mchana wa siku inayofuata na kumhakikishia ushindi Kafulila dhidi ya mgombea ambaye wanaoijiona ni maadui wa Zitto walikuwa wakimfanyia kampeni.



Mfano,toka kuanza kwa malumbano yake na viongozi wengine ni Zito pekeyake amekuwa akiongealea tofauti zao kwenye vyombo vya habari.sijamsikia kiongozi mwingine wa CHADEMA akiongelea matatizo ya ndani ya chama kwenye vyombo vya habari,kuanzia mbowe,dr.slaa,mnyika na viongozi wengine.

Haikutosha sio tu kulazimisha matokeo kutolewa lakini pia siku ya pili viongozi wenzake wakiongozwa na Slaa ambaye alilishwa majungu wakaanza na kwa kutumia vyombo vya habari kusema kuwa kuna vijana wanatumiwa na mafisadi na kutoa rushwa katika uchaguzi huo wa vijana wakimlenga Zitto.

Haikutosha, wakaanza kumzodoa mama yake mzazi ambaye ni mwanchama mwanzilishi wa CHADEMA tangia enzi 1992 wakati ambao wengi wa hao wanaomzushia ama walikuwa nyumbani kwao CCM ama bado wanalazimishwa kwenda shule (nachelea kutumia neno vinuka.....). Hapo ndipo Zitto akaamua kuwatumia ujumbe kuwa hayuko tayari kuona wanamfanya kama ambavyo waliwafanyia viongozi wengine ambao walitofautiana nao.

nimekuwa nikimwamini Zitto kwa muda mrefu sasa ila kwasasa am highly conviced kwamba kuna watu ambao wanamtumia ili kuua CHADEMA.Ukijaribu kukaa chini na kufikiria kwa undani utagundua kwamba Zitto is not himself,kwa mambo ambayo amekuwa akiongelea na ku-support within these few months utagundua kwamba huyu Zitto wa sasa sio yule tuliyemjua kipindi cha nyuma.Mfano,kwanini amekuwa yuko againsnt na viongozi wenzake kwenye kila jambo recently?haiwezekani kwamba Zitto yuko smart kuliko viongozi wengine ambao wamemzidi kielimu,kiumri,upeo wa siasa,na mambo mengine mengi tuu.

Kama ulimwamini Zitto pale tu alipokuwa akifanya yale unayoyaona wewe tu kuwa ni muhimu na sio anayoyaona yeye then kweli ulikosea pa kuweka imani yako.

Na pia kama kutofautiana na viongozi (chama) chake ndio ushahidi wako wa kukuhakikishia kuwa Zitto anatumika then nakushauri pia uache kuwashabikia kina Sitta, Mwakyembe na wengineo ambao wanatofautiana na viongozi na wenzao wa CCM.

Zitto ni kiongozi ambaye anafikiri siasa kwa upeo tofauti na tuliouzoea ama tunaolazimishwa kuuzoe. Siasa za ukasuku na upigaji kelele hata kama taarifa za kitaalamu zinasema tofauti. Zitto ni smart ndio maana anaamini kuwa ili kushinda CHADEMA hakipaswi kuendelea na taswira ya VYAMA PINGA ambavyo kwao ni kukosoa kila kitu na kukaa pembeni kutofanya any constructive politics hadi hapo watakapopewa madaraka. Kwa hulka ya watanzania itabidi msubiri sana kwa vyama vyenye muonekano huo kuchukua madaraka. Zitto amethbutu kutumia style tofauti na ndiyo ambayo wenzake wengi wazee kwa vijana wanashindwa kumuelewa na kuanza kujenga fikira potofu dhidi yake kama mlivyo wengi wenu hapa.



Zitto ni mchanga sana kisiasa,hana upeo wa kuona mbali japokuwa ana elimu ya chuo kikuu,ni mtu asiye changanua kwa undani jambo kabla ya kutoa uamuzi,

Kama una maana ya kuwa mchanga na asiye na upeo wa siasa majitaka, hovyohovyo na fisadi tulizo na tunazolazimishwa kuzizoea then ur right 100%. Lakini kama ni kwa muono mwa siasa endelevu zenye vision ya kujenga siasa makini na effective then ur wrong 100% kumuona kuwa ni mchanga na asiye na upeo. I bet he reads, learn and strategies 100% more than u.

mpenda sifa,mtu asiye na shukrani,mtu asiyekumbuka alikotoka na watu waliomfikisha hapa alipo leo, mbinafsi ambaye anajifikiria yeye mwenyewe na maslahi yake pasipo kuangalia yana madhara gani kwa chama chake na wananchi wa tanzania kwa ujumla.

Hii ya mpenda sifa inanifanya nijiulize kama wewe sio CCM maana this is typical them. Kila kukicha kila anayesema machafu yao huitwa mpenda sifa nad so is Zitto, Slaa na wengineo.

Mtu asiyekumbuka anakotoka, hii inaonyesha kuwa humjui Zitto na ni mmoja wa wale wanaojenga mitizamo yao kwa kutumia taarifa hovyohovyo za wahandisi wetu wa habari. Mbinafsi, as i said b4, ask even his worst enemy atakuambia ni vipi Zitto mtu wa kujitoa kwa wengine.

Kama unadhani kutaka kubadilishana uongozi wa chama na Mbowe kunamfanya awe anajifikiria mwenyewe na maslahi yake zaidi ya chama na nchi hata hata aliojiweka katika hali mbaya kisiasa kwa kukubali kujitoa na kuonyesha kuwa hana msimamo, then subiri time will tell....

Actually maamuzi yake mengi yanalenga na kuona mbali zaidi ya hao wenzake walio tayari kuvunja chama ili mradi waendelee kulinda nafai zao za uheshimiwa.



..kama kweli alikuwa na nia njema ni kwanini asiwataaritu viongozi walioko juu yake kuhusu kusudio lake la kugombea nafasi ya uenyekiti?ok,kama kulikuwa na kutokuelewana baina yake na viongozi walioko juu yake basi atleast kabla ya kugombea angewafuata wazee wa chama ili wamshauri.

Kwa mtazamo huu ndio maana nasema wengi wetu ni wachukia CCM tu na sio wanademokrasia, wapenda maendeleo wala wataka mabadiliko.


wana JF lazima tukubali kuwa baraza la wazee la CHADEMA limeundwa na watu wasomi na wenye upeo mkubwa kisiasa na kiuchumi ukilinganisha na Zito ambaye ameanza juzi.

Tehetehe....sitasema mengi hapa ila tu nakuambia kuwa hata hao wachche wenye vyeti vingi haviwezi kuwafanya kuwa wana upeo mwingi kama wanapoingia katika siasa ama nafasi za uongozi wanaacha utamaduni wa kujisomea. fanya utafiti wako kuhus Zitto na suala la kujisomea ujue kama kweli hana upeo na wenzake wengie wamemzidi....



yeye akiwa kama naibu katibu mkuu kwanini aunde kundi lake la upinzani ndani ya chama badala ya kukemea na kutokomeza mambo kama haya ndani ya chama ili kukiimarisha chama?Najua hapa JF kuna wapenzi wengi wa Zitto,lakiniwengi wao ni washabiki tu ambao hawachukulii mambo kimaanani na kwa uzito unaotakiwa..wanaongea mambo ambayo hayana msingi na kulaumu mambo wasiyoyaelewa kiundani.

Moja, Zitto hajawahi kuunda kundi lake na kama kuna makundi ndani ya CHADEMA sio kundi la Zitto Vs Mbowe ali ni kundi la Mbowe Vs kundi la wanaompinga Mbowe abalo limeanza muda mrefu na kukuzwa wakati wa saga la Chacha na sasa kumshurutisha Zitto kujitoa.

Pia, angalia isije ikawa wewe ndio mshabiki tu ambaye hachukulii mambo kimaanani na uzito unaotwakiwa...

k
abla hujashabikia mtu fulani tafadhali tafakari kwa makini hali halisi ya mambo yanayojiri nchini kwetu halafu tafakari ni kwa kiasi gani wananchi wameamka kimawazo.utagundua ni kwa kiasi gani watu wamechoka na uongozi wa serekali yetu na kiu yao ya mageuzi.Sasachama tawala wanaona hatari iliyoko mbele yao kama hawatabadilisha mambo haraka.Njia yao kubwa ya kurudisha imani na matumaini ya wananchi juu ya chama tawala sio kuwajibika na kurekebisha makosa yao bali kudhoofisha vyama vingine vilivyoanza kujenga imani kwa wananchi.Kwahiyo mpango wa CCM sio kuondoa mafisadi bali ni kuondoa wale wote wanaopinga mafisadi.CCM wana nguvu na pesa ya kukamilisha madhumuni yao hivyo wanaingia kwenye vyama vya upinzani na kujaribu kuwasifia na kuwaweka karibu wale viongozi wa upinzani ambao ni tishio kwao.wanawapa vyeo,mishahara na marupurupu mengi na kujidai kuwa-support.hii yote ni kujaribu kuwa mastermind ili kuwamaliza.sasa kwa viongozi wa upinzani ambao ni wana tamaa na walafi wa madaraka na umaarufu wanategwa kirahisi tuu kwa mitego kama hii.wanakufa na kuua vyama vyao kisiasa.. sasa ni lazima tujiepushe sana na viongozi wa aina hii manake watatupeleka pabaya..kila unapoona kiongozi mmoja anakuwa always against majority kwenye issues ambazo ni sensitive lazima ukae chini ujiulize ni kwasababu gani.

Acha kutumia CCM kuficha makosa yako. CHADEMA walipewa chance ya mwaka kujijenga lakini wao wakaitumia kujiharibia.



tukumbuke usemi wa Mwalimu Nyerere,"UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU".GOD BLESS US ALL!

Masikini mwalimu. hata maadui na wasaliti wake wanamtumia kuhalalisha maovu yao.....

omarilyas
 
SIRI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe kuondoa jina lake katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa chama chake imejulikana.

Taarifa zinasema Kamati ya Wazee ya CHADEMA ilikuwa inahofia Zitto angeendeleza matakwa yake, “angetokomea kisiasa.”

Naye Mwanzilishi wa CHADEMA, Edwin Mtei, akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi Jumatatu alisema, “Zitto bado mchanga.”

Chanzo cha habari kimemnukuu mmoja wa wazee akisema, “Kijana huyu bado ana muda. Hana haja ya kuwa na papara. Tumemlea na bado anahitaji malezi na maelekezo; lakini angekaidi angekuwa anajitokomeza mwenyewe.”

Zitto, mbunge wa CHADEMA, Kigoma Kaskazini, alichukua fomu za kuomba kuwania uenyekiti wa chama chake ili apambane na mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe.

Taarifa zinasema, Kamati tayari ililetewa “dozi” (taarifa nyingi za siri) juu ya Zitto, lakini kabla hajasomewa “mabaya” yake, walimueleza kistaarabu kwamba ni vema akaondoa jina lake.

“Alipofika ndani ya Kamati, hakushinikizwa kama inavyoelezwa. Alielezwa juu ya hali ya chama na baadaye kutakiwa kutoa kauli yake kuhusu kugombea uenyekiti au kutogombea. Alisema anaondoa jina lake,” kimeeleza chanzo cha habari.

Hata hivyo, tuhuma mbili kubwa zilikuwa zikimsubiri Zitto katika Kamati Kuu (CC) ya chama chake.

Ya kwanza ni ile ya kushambulia mwenyekiti wake, Mbowe kuwa amekuwa baba wa migogoro badala ya suluhu katika chama.

Shutuma za Zitto zilitangazwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchi, likiwamo gazeti la Mwananchi na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW).

Zitto alinukuliwa akisema, ndani ya CHADEMA kuna harufu ya ukabila; akitoa mfano wa mchakato wa kuwapata wabunge wa Viti Maalum mwaka 2005, ambapo alisema wengi walitoka mkoa wa Kilimanjaro.

“Unajua hizi tuhuma ni nzito. Zingefikishwa CC, Zitto angejimaliza. Kwanza, ni yeye aliyekuwa Katibu wa Kamati ya kutafuta wabunge wa Viti Maalum. Sasa kuna makosa yamefanyika, na yeye ndiye mhusika mkuu. Asingeweza kukwepa,” zimeeleza taarifa za ndani ya chama.

“Zitto asingeweza kuthibitisha madai kwamba mwenyekiti anahusika. Kama kuna upendeleo, basi naye angehusishwa kwa kuhakikisha anampitisha dada yake, Mheshimiwa Mhonga Saidi,” ameeleza mtoa taarifa.

Tuhuma ya pili kubwa ilikuwa ujumbe wa simu aliomtumia Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Taarifa zinasema Zitto alimweleza Dk. Slaa kuwa hana “msaada wowote katika chama;” na kwamba kama kuna kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa CHADEMA, basi ni yeye na Mbowe.

“Huyu dogo, nadhani ameanza kulewa sifa. Kweli ana ubavu wa kujilinganisha na Padri huyu (Dk.Slaa)? Jambo hili lingefikishwa Kamati Kuu, hakika angekutana na cha moto,” mbunge mmoja wa CHADEMA alilimbia gazeti hili.

Imeelezwa kwamba tuhuma za Zitto ndizo zilifanya hata pendekezo lake la awali kuwa Dk. Slaa agombee uenyekiti likataliwe.

“Lakini Dk. Slaa alikataa kugombe uenyekiti, akisema hataki nafasi hiyo. Sababu kubwa ni kule kushambuliwa na Zitto. Sasa kufika hapo kukawa hakuna njia nyingine, bali Zitto kukubaliana na ushauri wa wazee wa kuondoa jina lake,” ameeleza mjumbe wa kikao cha wazee.

“Unajua wazee waliona mbali, kwamba Zitto asingweza kushinda uchaguzi. Angekuwa kama Profesa Safari (Abdallah Safari, aliyeshindwa vibaya na Profesa Lipumba katika uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF), jambo ambal lingemdhoofisha,” ameeleza.

Ndani ya CHADEMA taarifa zinasema Zitto hakuwa na mtandao mkubwa ambao ungemwezesha kushinda uchaguzi. Wabunge wote kumi na moja, ukimwondoa yeye na Mhonga, hawakuwa pamoja na Zitto katika uchaguzi huo.

Nguvu kubwa ya Zitto ilionekana kutoka nje ya CHADEMA, jambo ambalo lilianza kutia mashaka baadhi ya wanachama wenzake wakiwamo viongozi wakuu.

Watu pekee wanaofahamika kuwa ni wana-CHADEMA ambao walikuwa nyuma ya Zitto, ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa, Afisa wa Habari, Devid Kafulila na mwanachama maarufu wa Dar es Salaam, Mkumbwa Kitilya.

Mtemelwa ambaye kabla ya kujiunga na CHADEMA, alikuwa amepitia vyama mbalimbali ikiwamo CCM, NCCR- Mageuzi, Tanzania Labour Party (TLP) na CUF, ndiye aliyerudisha fomu za Zitto na meneja wake wa kampeni.

Ni Mtemelwa ambaye wakati wa mtafaruku wa uongozi ndani ya chama cha NCCR- Mageuzi, alipachikwa jina la “Black Mamba” kutokana na kuandaa makundi ya vurugu na ghasia yaliyoshabikia Agustine Mrema.

Wakati huo alikuwa mwenyekiti wa taifa wa vijana na aliapa kutetea Mrema hadi kaburini. Alikaripia na kutishia kila aliyetofautiana na Mrema.

Katika uchaguzi wa CHADEMA, Mtemelwa alibwaga katika harakati zake za kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa kupitia mkoa wa Temeke.

Taarifa zinasema karibu viongozi wa mikoa ya Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Morogoro, Manyara, Singida na Zanzibar, bado walikuwa na imani kubwa na uongozi wa Mbowe.

“Unajua hata hoja yake ya kuondoa jina ilipofika CC, hakuna mtu aliyehoji maamuzi yake. Hapa panathibitisha kuwa wazee waliona mbali, maana kama Zitto angefika mkutano mkuu angeshindwa vibaya kwa vile hakuwa na mashiko,” anasema mwanachama mmoja wa siku nyingi wa CHADEMA.

Naye mwandishi wetu, Steve Mwasubila anaripoti kuwa Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha CHADEMA, Edwin Mtei amewakata vijana kujihadhari na mbinu chafu za mafisadi na wala rushwa ili kulinusuru taifa.

Matei alitoa kauli hiyo juzi, Jumatatu jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mkutano wa uchaguzi wa vijana wa chama hicho, ambapo aliwataka vijana kuwa imara na kuepuka mitego ya mafisadi ya kutaka kukizorotesha chama kwa kuwapaka matope viongozi wake wakuu.

Alisema wakati wote amekuwa na masikitiko kwa kuwa vitendo vya kifisadi na ulaji rushwa vimekithiri nchini, wakati watoto wa masikini wakifa kwa utapiamlo.

“Kama watoto wa masikini wanakufa kwa utapiamulo, basi hiyo ni njaa, hivyo kauli ya rais kuwa hakuna mtu atakayekufa kwa njaa ni ya kusikitisha sana,” alisema.

Alisema mara kwa mara rais amekuwa akitoa kauli zenye kuacha maswali mengi kwa Watanzania wengi walio masikini.

Aidha, Mtei aliwataka vijana kujihadhari na Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo alisema imekuwa ikivifadhili baadhi ya vyama vya upinzani kwa maslahi ya chama tawala. Hakutaja vyama hivyo.

Alisema hali hiyo ni moja ya vituvi vinavyochangia kuua demokrasia ya kweli nchini na kuendelea kukilinda chama tawala kizidi kuteketeza raslimali za nchi.

Alisema kwa miaka 48 CCM imekuwa madarakani, imeshindwa kukidhi matarajio ya Watanzania. Alisema chama hicho kimedumaa kimawazo na kimetekwa na mafisadi, huku akiwataka wana CCM wenye kukerwa na ufisadi kujiengua katika chama na kujiunga na CHADEMA.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe aliwaasa waandishi wa habari kuacha kutumiwa na baadhi ya mafisadi kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kushiriki “kuibaka nchi.”

Akizungumzia kuenguliwa kwa Zitto katika kuwania nafasi ya uwenyekiti, Mbowe alisema maneno yasiyostahili na yenye kuonyesha kuwepo kwa mgogoro ndani ya CHADEMA, yamekuwa yakikuzwa na vyombo vya habari wakati hali ndani ya chama hicho ni utulivu.


Chanzo: Gazeti la MwanaHalisi
 
hao chadema waache propaganda zao, watoe ukabila ndani ya chama, hakiko tayari kuongoza nchi...wewe eti mbowe ndiye awe rais wa nchi wapi na wapi...
 
hao chadema waache propaganda zao, watoe ukabila ndani ya chama, hakiko tayari kuongoza nchi...wewe eti mbowe ndiye awe rais wa nchi wapi na wapi...


Karibi JF
naona umetumwa nawe umekuja ukiwa akili umeacha nyumbani ama chumbani .Soma uelewe kinacho sema kabla ya kurukia Urais na Mbowe .Pia taja Ukabila wa Chadema ambao unamnyima Mwananchi kupata huduma hosp katika Nchi ama kukosa uniform za shule .Usikurupuke kaka . Taja ukabila na uonyeshe wapi kuna semwa Mbowe anakuwa Rais .Chadema kuchukua Nchi si lazima Mbowe agombee .
 
Ya kwanza ni ile ya kushambulia mwenyekiti wake, Mbowe kuwa amekuwa baba wa migogoro badala ya suluhu katika chama.

Shutuma za Zitto zilitangazwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchi, likiwamo gazeti la Mwananchi na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW).

Zitto alinukuliwa akisema, ndani ya CHADEMA kuna harufu ya ukabila; akitoa mfano wa mchakato wa kuwapata wabunge wa Viti Maalum mwaka 2005, ambapo alisema wengi walitoka mkoa wa Kilimanjaro.

Hii ni shutma nzito dhidi ya Mbowe. Binafsi nilikuwa nimeridhishwa na maelezo ya CHADEMA namna uteuzi wa wabunge maalumu ulivyofanyika kwamba taratibu za NEC ndiyo zenye matatizo. Lakini kwa malalamiko ya Zitto inaleta maswali zaidi.

CHADEMA wanapaswa kuwa makini sana ktk uchaguzi ujao ili kuhakikisha kwamba makosa hayajirudii.

Tuhuma ya pili kubwa ilikuwa ujumbe wa simu aliomtumia Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Taarifa zinasema Zitto alimweleza Dk. Slaa kuwa hana “msaada wowote katika chama;” na kwamba kama kuna kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa CHADEMA, basi ni yeye na Mbowe.

Hii kama ni kweli basi Mhe. Zitto atakuwa amemkosea heshma huyu mzee. Ni dhahiri kwamba Dr. Slaa ndiye mhimili imara wa CHADEMA. Hata umaarufu ambao chama kinapata unachangiwa kwa sehemu kubwa na Dr. Slaa kuliko kiongozi mwingine yeyote ktk chama. In fact, tunategemea kumwona Dr. akikimbiza bendera ya upinzani dhidi ya Kikwete mwakani.

Kama ni kweli Mhe. Zitto anapaswa kumwomba radhi huyu Mzee wetu, mpiganaji imara na shujaa. Hivi jamani kuna Mzee gani anayeweza ku-copy na vijana kama Dr. Slaa? Nani jasiri dhidi ya ufisadi kama Dr. Slaa? Ninaamini hata nafasi ya ukatibu mkuu anaifanya vizuri ndo maana ameteuliwa tena. Huyu mzee alikuwa katinu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki! Hilo baraza limejaa wasomi, werevu, watu wenye uzoefu wa uongozi na exposure kubwa.

atu pekee wanaofahamika kuwa ni wana-CHADEMA ambao walikuwa nyuma ya Zitto, ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa, Afisa wa Habari, Devid Kafulila na mwanachama maarufu wa Dar es Salaam, Mkumbwa Kitilya.

Mtemelwa ambaye kabla ya kujiunga na CHADEMA, alikuwa amepitia vyama mbalimbali ikiwamo CCM, NCCR- Mageuzi, Tanzania Labour Party (TLP) na CUF, ndiye aliyerudisha fomu za Zitto na meneja wake wa kampeni.

Sasa makundi mwisho, wakae wajenge chama, imani ya watanzania bado ipo juu yao.
 
Yani hii ndio siri????????????????hivi nyinyi mnajua maana ya neno siri??????????????????
 
Engineer,

Hii ndiyo point muhimu sana na nukuu ya leo.
Mtumishi,

Ha haaaa!! unamwibia mtu ng'ombe wake halafu kesho unasema tukae chini tupatane?

Hapo sahau umoja maana hata mkimwagia maji chini kutakuwa na moto tu.

Dawa ilikuwa kuwaruhusu wote wagombee na mmoja abwagwe chini na wanachama.
 
Back
Top Bottom