Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?


Haya yote nimeyasikia na ndio maana mimi huwapiga nondo kali sana wale wote wenye chuki za kidini na kikabila hapa jamvini. Kuna sehemu hapo pwani huwezi kununua kiwanja kama wewe ni mkiristo au kabila fulani.

Watu inabidi sasa wanatumia wakazi wa Pwani kuwanunulia viwanja maana wao pekee hawawezi kupewa (kutokana na maagizo ya kijinga toka kwa watu wasioitakia mema Tanzania).

Kazi kweli kweli
 
U need to find a hoby badala ya kuwa mropokaji kiasi hiki!

 
Just delete that "mchagga thing" inatugawa na haina mantiki katika undugu wetu wa kitaifa!!

What if is true?? jamani kunya anye CCM akinya CHADEMA karanga? wote tunapige kelele ili kusiwa na ukabila, kama Zito angeruhusiwa huoni kuwa wangeondoa hilo wingu maana lipo na lilikuwepo! kama CHADEMA tunakiamini kwa nini tusikionye leo?
 


..mkubwa wao alitoa maagizo juzi akiwa lindi akizindua barabara inayolipiwa mkopo wake kwa kodi zetu wote ...aliwaambia """ sasa barabara hiyo msimuuzie mtu yeyeto ardhi..."....nikajiuliza kama ni barabara imeanza kujengwa tangu enzi ya nyerere,mwinyi,mkapa,na sasa wanaendelea ...sikupata kumsikia mkapa mfano pamoja na kutokea huko pwani ya mtwara na kujenga sehemu kubwa ya barabara akiwaagiza wakazi wasikaribishe watanzania wenzao....ujinga kabisa..kukaribisha wasomali sawa ..lakini watanzania wenzenu tatizo....

juzi waziri mmoja akiwa bagamoyo ...akawaambia kuwa wanapeleka pale bandari ;;;na EPZ na akawataka watu pale wasimkaribishe mtu kufaidi hayo matunda.....kwa kuuza ardhi...,sasa tunaenda wapi????...hiyo EPZ na BANDARI si inajengwa kwa kodi za wote...kwa nini wazuie watanzania wenye nia ya kutega uchumi pale wasichukue fursa kwa usawa....???.... afteral bandari hiyo na epz hazikuwa na sababu badala yake wangejenga EPZ mtwara au tanga...waunganishe na uganda kwa tanga na malawi na zambia kwa mtwara...hakuna sababu ya kujenga bandari mpya bagamoyo just 30km away the dar es salaam port....
 

Mara nyingine hutokea mtoto akawa maarufu kuliko baba aliyemzaa ..... sishangai hali hiyo ikitokea kwa Zitto na Chadema!!
Ni mtazamo tu
 
Kunya, kulawiti, ujinga, upumbavu etc halafdu Zitto akijibu anatoa siri!
 

Eric,

Acha kupayuka ovyo, Zitto kakosa uhalai wa kuwa kiongozi kwa mujibu wa kifungu gani cha katiba yenu? acha blah blah umemwaga pumba tupu, kajipange uje upya au mwambieni baba mkwe amvue uanachama kabisa.

Philemon,

Eric Ongara mwanachadema (sijui ana cheo gani huko ) amekuja na shutuma na kumwaga matusi ya nguoni kwa Zitto. Huu ni muendelezo wa mashambulizi ya viongozi wa kada mbalimbali wa Chadema kwa Zitto.

Katika hali kama hii Zitto akijibu anaambiwa anavujisha siri! kakosa uhalali wa uongzozi nk.

Doule standards!
 
Shida Salum, maarufu kama First Lady ameshukia Dr Slaa na kumtuhumu kwamba amemuita mwanae kuwa ni fisadi. Shida Salum ambaye ni mama mzazi wa Zitto Kabwe aliyesama hayo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA(BAWACHA).

Akifungua mkutano huo, Dr Slaa alisema kwamba wanawake wa CHADEMA wawe mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi na kuhakikisha kwamba mafisadi hawasambaratishi CHADEMA.

Dr Slaa akatoa mfano wa jinsi ambavyo mafisadi walitaka kuichafua CHADEMA wakati wa kifo cha Wangwe na kufikia hatua ya kupika habari kwamba Mbowe alifukuzwa na mapanga Tarime.

Dr Slaa alisema kuwa huo ni mkakati wao kwa kuwa hata wakati wa hoja ya BOT walifikia hatua hata ya kuutumia usalama wa taifa kutimiza azma hiyo kwa kunukuu barua yao ya kuzuia hoja hiyo.

Dr Slaa alisema kuwa CHADEMA ndio mbadala wa CCM hivyo inatazamwa kwa matumaini na watanzania wote na kuwataka wanawake wawe mstari wa mbele kulea chama.

Mara baada ya Hotuba hiyo, Mama Shida ambaye alikuwa ni mgeni waalikwa kwenye ufunguzi wa mkutano huo kama Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Ulemavu(CHAWATA) alinyoosha kidole kusema neno.

Moja kwa moja akamlaumu Dr Slaa kwa kumuita mwanae kuwa ni fisadi. Akamtaka afahamu kuwa makao makuu ya chama hicho yamejaa uchafu.

Hata hivyo, Dr Slaa ambaye katika hotuba yake hiyo hakusema popote kuwa Zitto ni fisadi alimshukuru Mama Zitto kwa swali lake, na kumweleza kuwa kama ofisi ya katibu Mkuu inauchafu basi ni jukumu la yeye na Naibu Wake ambae ni mwanae Zitto Kabwe kuundoa ama kuwajibika.


..........ndiyohiyo
 
Asante, kaka wewe nawe umetoa hoja! hobby(sio hoby) yangu ni kuropoka!

Ni lugha yangu ya tatu hiyo ila nashukuru kwamba nimeeleweka na ujumbe umefika. Tujaribu o gea mambo ya msingi badala ya kukazana kuvamia watu wa nasaba fulani waliotoka maeneo flani. Pia tujaribu kuelewa ni nini kinajadiliwa kabla ya kukurupuka na kuanza kumvamia mwandishi badala ya kujibu hoja kwa kujenga hoja... Ukitaka mpanda Eric personally mfuate PM kama ambavyo umenifata mimi..!
 


Kumbe ulivyoandika muda ule, ulijenga hoja kwa kusema unaropoka? au unaona kuna mtu anatishika na lugha hizo humu? wengine tushatukanwa sana tu, sasa ukitokea wewe unaadika unaropoka haugusi kitu.

Ebu angalia post yako hii ya pili ilivyojaa utu na hekima, jribu kufikiri kama ingekuwa ndiyo umendika muda ule!

wengine wanavyofanya wanaread btn lines na kukosoa na kujenga hoja kila mstari, ukichukua post ya mtu nzima na kusema unaropoka, huwi tofauti na huyo aliyeropoka, tena inakuwa aibu mtu wa heshima kama wewe kumwambia kichaa kama mimi unaropoka, maana kuropoka inaweza ndio ikawa mimi na kila mtu ananijua kwa hivyo!

Ebu tauche hayo naona umekuja kikubwa inaweza ukawa hukunielewa, lakini nimemjibu kwa mawazo yangu, si unajua JF, we dare talk openly! kuna watu tuna matatizo ya ubongo na maisha , ninapofanya kosa jaribu kunielekeza kama ulivyofanya hapa! mkuu ndio maana linaitwa jamvi

Thank though, you are good man to me!
 
 
We can not under estimate nguvu ya mafisadi. Naamini maneno ya Mzee Mtei kuwa mafisadi wamepenyeza rupia Chadema. Kuna uwezekano kuwa haya tunayoyaona ni matokeo ya operesheni hiyo. Kama Chadema wakionesha maturity kwenye ku-deal na hili litakuwa jambo la maana na itaweka mazingira mazuri ya chama kujijenga. Lakini kama kesho wakifanya fyongo watawapa CCM a big greenlight.

Uzuri wa CCM ni chama ambacho popularity yake haijajengeka kwa individual personalities, imejengeka kwenye collective personality ya chama. Hata JK akiondoka leo bado CCM ni CCM tu, lakini inatia shaka kiasi kwa upande wa upinzani na CHADEMA as well. Inatia shaka zaidi kwa kitendo alichokionesha Zitto na kimezusha maswali Mengi kama kweli Zitto Kabwe. Is this Zitto Kabwe we know, the one we call him a hero, a camouflaged Zitto?? Is Zitto Kabwe we have seen in the past two weeks, a selfish one, the one who needed elders to tell him that personal rift will cause cancer in the party, a real Zitto ?? sijui kama ni kweli tatizo ni ugomvi binafsi kati yake na Mnyika na Mrema, au na yeye amelambishwa asali chafu na kusahau umuhimu wake kwa Tanzania hasa kwenye kipindi hiki tunapoendelea 2010. Who knows, ni yeye mwenyewe anayejua ukweli.

Lakini kusikia ushauri wa wazee ni credit kwa Zitto, na wazee kuplay role ndani ya Chadema ni credit pia na ni utamaduni wetu watanzania, na inaonesha kuwa kuna effective internal mechanism inayoweza kufanya kazi ya kukilinda chama. Kwa hiyo the whole thing ni kuwa imeonesha wekaness na strength ya Chadema. Lakini blow aliyotoa Zitto kwa Chadema ni kubwa na itakuwa na madhara makubwa sana kwa Chama 2010.
Zitto naona upo online hapa, do not take it personal. Najua umewafurahisha baadhi na umetusikikisha baadhi pia.
 
 
Dude appears arrogant, self-righteous, ego-tripping and not least has a tendency to draw (and relish in) attention to himself.

I bet in the back of his conceited mind he believes himself to be some kind of charismatic, young, uniquely ambitious, next generation political animal in the local political scene.

All the hype he receives on a daily basis in the tabloids as some sort of an up-and-coming political stalwart and stud (among the usually grey-haired CCM geezers and rest of the aging, tired-looking and boring political talking-heads) no doubt contributes to his big-headedness (or inflated sense of self-importance if you will)

But one thing I know for sure (and you can all agree with me - more or less), ni kwamba jamaa ana sura mbaya kama kiatu cha Baniani! Damn!
 

Well Mkuu, Zitto is no devil. Nakumbuka kauli ya FMES, "viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe" kwa hiyo ukumbuke kuwa unapomsema Zitto maana yake nini. Hii ni Tanzania ndugu.
 
Mkuu Eric,
Shukran sana kwa mwenye kusoma between the line ataelewa ni mambo gani yamekuudhi. Na hakika umeeleza kama mpenzi na mwanachama wa Chadema ambaye unatazama mbalii na nje ya kabati hili la Udini na ukabila kwani haya yote na matokeo ya hasira za watu wote humu..

Kitu kimoja tu, umeeleza mengi kuhusu Zitto na tumekuelewa lakini umeshindwa kuelezea pia Ukweli wa lawama za Zitto pamoja na hasira zake. Je, kuna ukweli gani?...hapa nikiwa na maana wazee wa Chadema na washabiki woote waliokuwa against Zitto nao wana makosa makubwa tu ambayo tunayafukia fukia na visigino nya miguu yetu.. Ubaya wa kinyesi hakiwezi fichika kwa mchanga kwani ni harufu yake inayowaudhi watu.

Yawezekana wazee wa chama walifanya hayo kwa nia nzuri kama Zitto lakini kama utakuwa makini utagundua kwamba ni WAPAMBE wa pande hizi mbili walomwagia Petrol cheche za Uchaguzi huu ambao nina hakika Zitto na wazee walishafikia muafaka...Sisi ndio tulomhukumu Zitto na wazee kama Yesu na waumini wake walivyohukumiwa na Wayahudi.

Kama mtakumbuka mwaka 2006 baada ya Uchaguzi mkuu nilikuuliza wewe kuhusu Uchaguzi ndani ya Chadema ktk viti vya wawakilishi wake ikiwa ni pamoja na Secretariet. Sikuona ushindani mkubwa zaidi ya kuwa uchaguzi ule ulipangwa watu wakagawana vyeo. Nilipinga mfumo mzima wa chama Chadema na hakika niliwakalia kooni vibaya sana..
Nilihoji pia kwa nini ktk kugombea kiti cha rais Mbowe hakupata mshindani wa kweli na tulizungumzia hoja hizi kwa mapana kiasi kwamba nilikuwa mchungu kwenu. hakika mwaka huu nilitegemea ushindani na mambo mengi kurekebishwa kwani hizi tuhuma za Uchagga na Udini zimekuwepo sii leo. Zipo miaka kibao na wala sii Zitto kiongozi wa kwanza ndani ya chama kulalamikia haya. Sisi sote tulitegema kutakuwa na mabadiliko mwaka huu na pengine kila mgombea kuanza kuipanga vizuri zaidi.

Mara zote uchochezi wa Demokrasia ktk chama na ushindani wake una malengo ya kukuza fikra huru za kuwasilisha sera za chama kwa wananchi. Ni kutokana na chaguzi hizi huwafanmya viongozi wetu wawe active, waweze kuonyesha uwezo wao wa kuongoza kwa sababu bila hivyo watapoteza kura na imani ya wananchi.

Kuzuia Demokrasia na uwakilishi wa mawazo ambayo hujenga sera na utekelezaji wake ni sawa na Taifa linalokuwa chini ya Udikteta. Kiongozi anakuwa hana sababu ya kufanya kazi kwa bidii kwani hana mpinzani. Kila anachofikiria yeye ndio kitakuwa, na kwa bahati mbaya ndivyo tawala za Kiafrika zinavyojiendesha..
Natofauti kati ya nchi moja hadi nyingine ktk maendeleo yake ni pale kuna Demokrasia ya kweli yaani kuna ushindani wa shina ktk chama kupropagate sera na Utekelezaji wake kichama na kwa mapana yake mrengo na sera Kitaifa.

Binafsi nilitegemea Zitto na Dr. Slaa kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chadema lakini kama uloandika ndivyo Ilivyo (yaani mwenyekiti ndiye mgombea kiti cha Urais) basi chama Chadema wamecheza mbovu na rafu..isipokuwa kosa la Zitto linakuja tu ktk kuandika vitu ambavyo yeye mwenyewe aliafiki mwanzoni wakati wazee hao wa chama hawana UWEZO kulingana na katiba kumwengua.

Kukubali kwake ushauri wa wazee hao wa chama kisha akaja wageuka na kusema walimlazimisha hali akijua fika kwamba Kikatiba hawana uhuru huo ni kuonyesha uvivu mwingine wa kifikiri. Zitto alitakliwa kuendelea kipigana kama mama Clinton alipoambiwa ajitoe akazua hoja ya kwamba anashutumiwa kwa sababu yeye ni mwanamke!... Froim that day alipindua upepo wa kura..Kwa mamillioni wanawake walimuunga mkono na kumpa kila nguvu kuendelea hadi siku alokuja shindwa..

Wakuu zangu tusidanganyane hata kidogo.. Siasa ni mchezo mchafu, yaliyomkuta Zitto ni mambo ya kawaida kabisa ndani ya chama. hata huko Marekani ndani ya Demokratic wana tofauti zao na wana makundi ya kuunga mkono/kupinga sera na utekelezaji wake ikiwa wanaona hautakuwa na manufaa kwa wananchi wake. Obama leo hii anakabiriwa na Upinzani mkubwa toka ndani ya chama chake. na wapo viongozi wa chama chake wanampiga madongo ktk TV kila siku kuhusiana na mpango wake wa Afya kwa wote..Ni jukujmu la Obama kuwa convince wabunge wake kwamba mpango wake utakuwa na mafanikio ya kudumu na hautaiweka nchi ktk madeni na matatizo zaidi. Hii ndio Demokrasia ya kweli nasii kugombea vichwa vya watu kutokana na majina yao.

Ushabiki wote ulokuwepo hapa JF ni ushabiki wa vichwa vya watu..Tuanshindwa kuelewa kwamba ushindi wowote ule hutokana na team work. Tunacholalamika ni kuwekwa bench kwa Zitto na Mbowe kuchukua nafasi ya Goalkeeper wakati sisi sote sii makocha wa team Chadema. Hao wazee tunaowalaumu wana akili, hekima na busara kuona nje ya sanduku la ushabiki na kama wao ni washabiki basi tutawahukumu pindi Ushindi utakapo kosekana kwani hata Mkapa na JK walipogombea Urais wapo wana CCM wengi walipinga nyendo zilizotumika. yet CCM wameendelea kushinda na ndio Ilani kubwa ya chama.. To win by all means necessary!
Mkielewa undani wa maneno haya, kazi za wazee ktk chama mtaweza kuelewa kwamba Demokrasia pia nimfumo unaofuata mahesabu na sayansi kama majaribio yoyote yale ktk maabara..Mkikosea hesabu Demokrasia inaweza kuwa mbegu ya magugu na mtavuna magugu.

Kifupi tuachane na habari za Zitto na viongozi wa Chadema.. tuwe na subira tupate kujua kinachoajiri hivi sasa. Sote tulivutiwa na kugombea kwa Zitto na sote tulihudhunishwa na kujitoa kwake lakini hatuwezi kutunga visingizio ikiwa mchezaji wetu mwenyewe kavua njumu na kuondoka iwe kwa hasira au kutofahamu athari za maamuzi kama hayo...Alotuangusha sote ni Zitto, period!

Yaliyopita sii ndwele tugange yajayo... wazee walichemsha na mkuu wetu Zitto pia ka smell..hivyo mashambulizi yote yanazunguka pande mbili na hakuna mwenye nafuu kati yao. Kukikomboa chama ni kuachana na yote haya na tusubiri maamuzi ya wahusika na jinsi chama kitakavyo fikia maamuzi yake kwa manufaa ya chama na wananchi wote.
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…