Lazima tukumbuke haki huambatana na wajibu.
Kaka kwa umri wako kukumbatia theory za kuhalalisha ugandamizaji kam huu unatutisha sana endapo utapewa uheshimiwa wenye makali ya dola
Jaribio lolote la kulazimisha wanachama wachague kati ya mtuhuru,Zitto au slaa ni fikra muhali za kihuni ambazo zinaweza kukijeruhi chama.
Unataka kusema kuwa wanaCHADEMA hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao?
CHADEMA ina wafuasi wengi lakini ni wachache waliojitokeza mbele katika siasa za moja kwa moja.Hivyo CHADEMA inahitaji majabali haya machache kuendelea kuwemo katika safu moja ili kukiandaa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu.Tayari kulikuwa na wazo la kutumia "utatu mtakatifu" yaani Mtuhuru,Slaa na Zitto katika kuipasua na kiitesa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwakani na hatiame kukiandaa vyema chama na mwaka wa mavuno mwaka 2015.
Kaka hata mimi naomba utokee muujiza hili lifanikiwe. Lakini swali kwa unavyomjua MTUHURU wako unadhani anaaminika hata kumpendekeza Zitto kuwa Katibu wake? Na kama kulikuwa na mpango huo iweje Slaa aache kuchukua fomu za kugombe umakamo?
Zitto alikuwa ana wajibu wa kutafakari namna ambavyo "haki" yake ya kugombea ingesababisha mnyukano ambao ungeibua athari za muda mrefu kwa chama na wagombea. Hatuwezi kuhujumu demokrasia ndogo kwenda kuathiri demokrasia Pana.Hatuwezi kutetea udhofishaji wa CHADEMA Kwa kiisngizio cha demokrasia na kwa wakati huo tukiua demokrasia pana yani ushindani wa CCM na CHADEMA.
Kwa hiyo kwako wewe unaona ni sawa kabisa kuacha CHADEMA iliyojaa wasiokuwa tayari kupractice demokrasi kuwaongoza watanzania kufanikisha demokrasia pana. Unataka kusema wale mafisadi wa kenya walivyowalaghai wakenya na dudu lao waliloliita NARC na kuja na madudu kama ANGLO LEASING Scandals ndio mfano wa kuigwa kwa watanzania?
Kugombea kwa Zitto kungefaidisha zaidi CCM zaidi ambavyo ingefaidisha CHADEMA. Kama CCM wangeombwa ushauri basi wangesisitiza Mtuhuru na Zitto washindane. Hivyo uamuzi wa awali wa Zitto kugombea ulikuwa tayari una manufaa kwa wapinzani wa CHADEMA Hususani CCM.
Kama sio kujua kuwa mmoja wao angekosa ustaarabu wa kutumia siasa safi kufanya kampeni zake, uoga wa kutowashindanisha unatokea wapi. Yaani mnataka kusema yale mawazo ya wahafidhina wa CCM kuwa kumshindanisha JK na mtu mwengine kutavunja chama yana maniki. Ilikuwaje mkaanza kuwabeza wale kina mama na wazee wa watu walipoandamana kuwatisha wanaCCM wengine wenye nia ya kushindana na JK 2010? Au kwa sababu huyu ni mswahili Jakaya ni sawa lakini sio "mstaarabu" FREEMAN AIKAELI?
Inalekea kulikuwa na makundi ya muda mrefu ambayo Zitto anayafahamu kwa mujibu wa maandiko yake hapa, na pengine ndio msukumo wake kugombea. Kama ndivyo,Zitto amepwaya kiungozi kwa kuamua kugombea kwa msukumo wa kukuza na kumaliza kundi jingine.Umbea, majungu na husda haviwezi kamwe kufaulu kama kichocheo cha kuwa mwenyekiti wa chama kitaifa.
Makundi hayakuanza na Zitto ila yameanza na utamaduni wa kufukuzafukuza kila anayetofautiana na maslahi ya wachache yanayopewa jina la maslahi ya chama. Na usimsingizie Zitto kuwa aligombea kukuza ama kumaliza kundi jingine. Kama kitu alichokuwa anasisitiza kuwa kinatia umuhimu wa yeye kugombea ni kusamehe wale wote walionewa kwa kufukuzwa ama kusimamishwa uanachama mara baada ya kuonyesha tofauti zao na mwenyekiti wao. Na hili amelisema hata alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari. Sasa hii ya kumaliza kundi jingine yametka wapi. Usitie shaka Zitto hana roho ya korosho na wala utamaduni wa kuweka vinyongo na pia best wako Mnyika kamwe hawezi kugeuka adui wa Zitto kwani wametoka mbali. Kidudu mtu ambaye anapaswa kunyamzishwa ni mwengine ambaye sidhani kama ana umuhimu sana kwako.
Zitto anaelewa kanuni, mazoea na taratibu za uendeshaji wa chaguzi zake za ndani. Kama alikuwa na nia njema alipaswa kuwa ameepika michakato hii ili isije ikadhuru nia yake ya kugombea na pengine kuwa na athari hasi kwa taathira ya chama kwa ujumla wake. Uzembe wake katika kutathmini hili ni hujuma za wazi dhidi ya haki yake kama mgombea na ustawi wa chama kwa ujumla wake. Ushauri uliotolewa na kamati ya wazee wa chama ni jambo ambalo Zitto alipaswa kulingamua hata kabla.Pengine lengo lilikuwa kukivua nguoa chama au kuwashwa na msisimko wa ndani.
Dogo umefikia lini umri wa Wazee wa Chama unakuja na mawazo mgando kama haya. Yaani U-CCM umewaathiri namna hii. Kama ninyi mliokulia katika enzo za siasa za ushindani mnafikiria hivi iweje leo muwashangae MAGOGO yaliyofubaa ya CCM?
Ipo changamoto ya chama ya kuwa na utegemezi usio wa kwaida kwa mtuhuru, slaa na Zitto kutokana na mitaji yao mikubwa ya kisiasa. CHADEMA inao watu wengi wenye weledi wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika medani ya siasa, hivyo kunapaswa kuwa na mkakati kambambe wa kuzalisha na kutambulisha kwa umma wanasiasa wengi zaidi.Utatu mtakatifu uliapaswa kuwa nyenzo ya kutengeneza mabingwa wapya. Zitto kwa uzembe au kiburi aliamua kupuuza hali halisi ya chama na kuamua liwalo na liwe! Suluhisho lake la mvutano wa ndani lilikuwa ni kusambaratisha wapinzani wake wa ndani na pengine kukisambaratisha kabisa chama kwa ujumla wake.
Aliyechukua fomu na kujaza kuomba ridhaa ya wanachama wake kuwa kiongozi wao na waliotumia bisara zisizo na hakima kumshinikiza ajitoe kwa kuogopa athari za siasa chafu za KIJANA wao na baadae wafuasi wake kuendeleza kumwaga sumu dhidi ya mwenzao, ni yupi ambaye anataka kukisambaratisha CHAMA?
Maandiko ya Zitto kama majibu ya Tuhuma dhidi zake JF
kwanini hakuna msukumo wa mlevi mwanaume kulazimisha kulatiwa?
Ina maana huyajui haya kama yanatendeka?
Ikiwa wabaya wake ni John Mrema na John Mnyika, kwanini ameamua kugombana na chama kizima? Uchaguzi wake makini wa maeneo ya kugusa katika majibu yake ni kielelezo cha mpangalio uliojaa uovu, fikra duni na nia mbaya, mathalan maelezo yanayoibua hisia kama suala la marehemu wangwe ni kielelezo halisi kuwa Zitto ana nia mbaya na CHADEMA. Huwezi kujisaidia katika kisima ambacho unatumia kwa maji ya kunywa na kupikia kisa umekasirishwa na mwanakijiji mmoja.
Ni wapi Zittoa amesema hawa ni wabaya wake. Na kama wakati Zitto anakubali ushauri wa wazee wao wanaingia mitandaoni na kwa waandishi wa magazeti kuendeleza propaganda zao kama walizotumi kumfrustrate Kaborou na Chacha Wangwe ulitaka Zitto awanyamazie. Ili iweje? Watu wazoee uzandiki wao hadi waamini?
Ikiwa ni kweli Mrema na Mnyika wamemtuhumu Zitto ni kwa nini kama kama kiongozi ameshindwa kutumia miundo ya chama kutataua? Na mbona amekishambulia chama kwa ujumla wake? Amekihusisha chama na uchaga( ni sawa na kuthibitisha propaganda za CCM au kuunga Mkono msimamo,mkakati na mtazamo wa CCM dhidi ya CHADEMA), maauji na matumizi mabaya ya fedha. Hizi sio tuhuma za kwa watu binafsi! Inaelekea anaowalenga wana mapenzi makubwa kwa chama zaidi yake, hivyo kete yake yeye ni kwa kuumiza kile kinachopendwa na hao maadui zake wa kubuni.
Unataka kuniambia kuwa Zitto angeenda kukimbilia kwa hao wazee ambao nao wanakuja kudai kuwa Zitto ana tuhuma za kuhonga vijana kwa ushahidi wa sms na vijikaratasi? Sijui kuhusu mauaji lakini unataka kusema CHADEMA hakuna tuhuma za matumizi mabaya? Hayo ya uchaga ni nani kama sio wenyewe wanayoyatengenezea mazingira ya kuyahalalisha. Tatizo hizi natural born arrigances zinawafanya muwe reckless kiasi cha kufanya yaleyale ambayo maadui zenu wangependa muyafanye ili muwathibitishie mapungufu yanu.
Hivi iweje mtu anayetumia fedha za chama vibaya, akatumia ukabila katika kufanikisha malengo yake akawa na mapenzi na chama chake na yule ambaye anamwambia kuwa acha kutumia ukabila ndiye akawa hana mapenzi nacho. Kwani haya yameanza kusemwa lini? jee kuna suluhu iliyofanyika kichama? Na imekuwaje kuwa hata alliances za utetezi wa MBOWE na mashambulizi dhidi ya Zitto zikawa na picha ya udini? sitaki nije kwa undani wake hapa lakini kama unahitaji nishtue nitakushukie the whole chain...
Ni kama anatuambia yeye haipendi CHADEMA kihivyo! wakiendelea kumgusa ataua chama! Huu ni ubakaji wa chama na kuibua hofu za kibazazi. Ni kama anawaambia wanaCHADEMA wasimuuzi lasivyo atanyea kisima?! Hatuwezi kuendesha chama kwa hofu na kuwaza ni lini Zitto atakunya katika kisima. Kuna maswala mengi ya kuwaza katika mustakabali wa nchi zaidi ya kunya kwa Zitto.
Kwa makusudi Zitto ameamua kupotosha suala la BAVICHA. Ushindi wa kafulila anauzungumzia anaujaje?. Nilibahatika kushuhudia uchagauzi ule, matokeo hayakutangazwa kutokana na idadi za kura kuzidi idadi ya wapiga kura. Hali ilivyoanza kuwa tete Zitto alitoa kauli tata kuwa vijana leo watatupiana ngumi na kutokomea, yeye kama kiongozi wa kitaifa anaamua kukimbia hali ile ulikuwa ni udhaifu mwingine mkubwa wa kiungozi wa Zitto.
Ulitaka abaki ili mtimize mpango wenu wa kumchoma visu?
Msiamazi baada ya kutangaza hali halisi ya zoezi la kura, aliwaapa wajumbe nafasi ya kutoa maoni yao ambao wengi walimtuhumu moja kwa moja Zitto pasipo kutafuna maneno kuwa alishiriki kuhujumu uchaguzi ule.
Tangu lini kumpigia kampeni mtu kukageuka kuwa kuhujumu uchaguzi?
hatukumsikia hata wakala wa kafulila akilalamikia kudhulumiwa. Ni aibu kwa Zitto kufanya jitihada za kuhalalisha uhuni ule. Ikiwa alibainie jitihada za hujuma dhidi ya Kafulila ni kwanini hakuziwasilisha katika kikao cha jumapili cha kamati kuu?
Tangu lini aliyeshinda uchaguzi akalalamika kuwa kadhulumiwa? angewasilishaje taarifa wakati wenye chama wameshinikiza hata majibu yasitolewe.
Kuhoji kamati ya wazee chini ya Mtei kuendelea kusimamia uchaguzi zinaozendelea wakati tayari baraza la wazee limechagua viongozi wake ni kielelezo cha kukosa uwajibikaji wa pamoja.
Yaani sasa mnataka hata watu wasihoji makosa ya kikatiba? Kazi kwelikweli.
Baada ya kikao cha kamati kuu jumapili iliyopita umma ulielezwa kuwa tofauti kati ya Zitto na Mtuhuru zimefutwa. Sasa hapa Zitto anaposema siku wakipatana na Mtuhuru wapambe nuksi watakoma anataka kusema nini? Kwamba walituzuga? Walifanya unafiki?
Kama msingeendelea na propaganda zenu dhidi yake ni wazi mambo yangekuwa shwari sasa. Kosa ni lenu mliochukulia uamuzi wake wa kujitoa kama weakness na mkaendeleza mpango wenu wa kummaliza kisiasa...Na msipoangalia mtaadhirika maana FREEMAN na ZITTO walijuana siku nyingi na wamefanya mengi pamoja.....wakati ninyi mnaendela na ujinga wenu huku wenzenu wanaangalia jinsi gani ya kufanya kazi pamoja huko mbele kuendeleza libeneke (ofcourse kama mmoja wao hajaendeleza chuki zake)
Jitihada za Kuiua CHADEMA ni jambo lisilovumilika kwa hali yoyote ile.Ni ushenzi na laana iliyo kuu. Naami hili ni jaribio la mwisho la CHADEMA kudhihirisha ukomavu wake wa kisiasa na kuwarejeshea matumaini watanzania. Upuuzi na udhaifu wa Zitto unaweza kusahihishwa
Wenye jitihada ya kuiua CHADEMA ni wale walio tayari kufanya lolote ili mradi kulinda vyeo vyao na maslahi yao hadi kuwafanya wazee kutumia busara isiyo na hekima kumshawishi Zitto kujitoa......
omarilyas