Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

 
Pole sana Zitto, lakini hizo ndio siasa kuna ups and downs. ndio kukomaa kwenyewe huko
 
1) I concur with M/falsafa1

2) kama ni family business sasa wale wanaosema ni chama cha wachaga, na huyu mamani mcgaga?

3) blaa blaaa blaaaa!! nyiiingi? wenyewe wanafanya wanajiandaa na mkutano wao wanavyojua wao.
kuku akinya fresh ila bata-ataambiwa kaharisha
 

Hiyo paragraph inabidi isomwe mara mbilimbili na Mh Zitto.........

Good point Mkuu Eric Ongara......unanikumbusha mbaali kwenye ule mjadala wa Majimbo..........
 

ni vema sana kusimamia hoja badala ya kutegemea "mtu"........hivyo basi tuwe huru kusoma hoja na tuzichambue kama kawaida yetu JF......au vipi Mkuu
 
ni vema sana kusimamia hoja badala ya kutegemea "mtu"........hivyo basi tuwe huru kusoma hoja na tuzichambue kama kawaida yetu JF......au vipi Mkuu

Umesahau jina la huyo bwana alokuwa akitumia kule bcstimes? heheheheheee.....ukilikumbuka wala hutashangaa tena...

Kwa kifupi mimi nadhana Zitto ni unstable and erratic politician. Hafai kabisa kushika nyadhifa za juu za serikali ya taifa! Ubunge ndio uwe kikomo chake.
 
Mkuu lakini twende mbele tukitazama nyuma.
.
Unajua naposoma maneno ya mzee Mtei, kisha nifikirie anayezungumzwa ni mtani wa jadi Ngabu ndio Zitto!.... Loooh ingekuwa kasheshe.. mzee wa watu pengine angekuwa amelazwa Hospital Pressure imepanda!.. hapo hapo sina hakika kutokana na reaction yako itakuwa ndio sababu ya kukuhukumu wewe uwezo wako ktk kuongoza...

Hata mimi kuna wakati hujiuliza kama ningeweza kuvumilia matusi ya Mzee Mtei na huyo Kibanda!
 
kavimba sana kichwa nae,tulimuona wa maana naona taratibu kesha boa watu sasa.........utajuuta kuingia siasa.
 

Kumbe mkuu ukitulia una pointi!!!!!
Hapa umeongea vizuri sana, tofauti na mabandiko yako mengine. I wish watu wangekuwa wanakaa chini na kuja na hoja kama hii hapa. U can post ten times kumbe ni posti yako moja au mbili ndo iko constructive.
Kwa namna hii JF ni jamvi kweli kweli, lakini sio kwa kushambulia watu wa kabila au dini fulani....
Hongera kwa hii posti...
 
Last edited:

Kuna mifano mingi sana ya watu waliokuja na kuvunja PRINCIPAL zilizokuwepo. Hawa walipelekea nchi kufanikia au kuangamia. Mtu kama Hitler amesaidia sna German kuwa sehemu ilipo. Leo wanalaani kuwa hata wao waliteseka, yes. Ila hawa akina BMW, VW, makampuni ya madawa nk walifaidika sana wakati wa Hitler na hilo technologia limewapa uwezo mkubwa sana wa kufika hapo walipo.

Ndiyo maana ninaipenda sana advertising SLOGAN ya Apple Comp. Inc ya miaka ya 90 isemayo "THINK DIFFERENT."
Tunahitaji mtu ambaye ataanza kuwabadili Watanzania mawazo ya kizamani yaliyopitwa na wakati. Ndiyo maana huwa nalaani Mrema kukosa Urais. Huyu bwana Tanzania ya leo kwa vyovyote vile ingelikuwa imebadilika na mentality za watu zingelikuwa tofauti. Tanzania ni kama Congo vile. Tumeridhika na kila kitu. Sasa mabadiliko yatoke wapi?
 

NN umenikumbusha kitu muhimu sana hapo.
 
Kwa kifupi mimi nadhana Zitto ni unstable and erratic politician. Hafai kabisa kushika nyadhifa za juu za serikali ya taifa! Ubunge ndio uwe kikomo chake.

Napenda kutofautiana na wewe mkuu....

Kusema ukweli nimemsoma Eric, Omar, NN, Ogah, Waberoya etc. vizuri sana. Hapa mtakubaliana na kutofautiana, ila ni vizuri watu wakajaribu kumtazama huyu Zitto kwa uzito unaotakiwa.

Kwa kilichojiri hapa majuzi naona Zitto kakosea sana. Ila kukosea huku ni kutokana na hulka yake ya kufanya mambo...KUJARIBU. Sio mtu wa kukaa nyuma na kuangalia watu wakifanya kwa sababu zozote zile ambazo unaweza kuzifikiria, mfano kuahirisha, uoga wa KUKOSEA, au ngoja tuone watakavyokosea etc etc. Pia naona experience kidogo kaikosa. Lakini bado yuko step ya mbele sana zaidi ya wengi wanaoongea kumponda hapa na kwingine kote.

Nachotamani kukiona kikitokea mbeleni ni kwa Zitto na wenzake huko CHADEMA kukaa chini na kujiangalia wapi tumekosea. We always learn from mistakes. Kilichotokea kisiwarudishe nyuma na kusambaratika. Wanatakiwa waonyeshe ukomavu kwa kutoka katika hii crisis kifua mbele, kuwashangaza wale wote waliokuwa wakiwaombea mabaya.

Kingine kitazamwe kwa nini hii ishu ya CHADEMA imekuwa kubwa namna hii?? Naweza kusema ni kutokana na nguvu yao ambayo walishajikusanyia. So huu ni wakati wa watu kumeza pride zao, kushuka chini, kukiweka chama mbele, kujisafisha na kikubwa kujifunza kutokana na kilichotokea kisitokee tena....
 

Zitto moyo na mapenzi yake kwa sasa yako CCM na kwa Kikwete:

1. Kamati ya madini
2. Dowans
3. Bajeti iliyopita ya serikali

and on and on
 

Mkuu Techmaro,

Chukua 5 kabisa. Kuna watu kibao tuna tabia hata kusema asante tunasubiri kwanza kuangalia nani kaweka asante ili kuficha msimamo wetu. Tukishaona fulani na fulani wako wapi (kama Mbunge wetu wa Sikonge - Nkumba) basi ndiyo na sisi tunaibuka kusema.

Ndiyo sababu pekee inawafanya wengine wampende Lowassa kwani na yeye huwa hasubiri. Ila Lowassa ana ujinga mmoja. Yeye atafanya jambo lolote limwijialo kichwani hata kama watamwambia kuwa hapa hapafai kwa hilo. Alilia Richmonduli na pamoja vitu kibao kukosekana, alipindisha kila mstari hadi ikapatikana. Watu kama hawa ni HATARI sana. Hawaambiliki wala hawashauriki.
Zitto na yeye pia ana PUPA. Hakai kusubiri wengine wanasemaje. Anaruka na kufanya lile ambalo yeye anaona linafaa. Ila pamoja na hayo, anaonekana ni mtu anayeweza kupokea USHAURI mara akionyeshwa kuwa hili dogo umechemka. Wengine wanamlaani kwa hilo. Anyway, kila mtu na mawazo yake. Ila ukweli lazima usemwe kuwa "ZITTO ANAFIKIRI TOFAUTI. Yes, Apple computer wanasema "THINK DIFFERENT".
 
Sijui ni lini tutaanza kuwashangilia mashujaa badala ya kuwanyamazisha na kuwakebei.

Mrema alipoyamwaga mapungufu ya CCM miaka ya 90 alitolewa mbio na kunyimwa mkate hadi sasa kakonda kiasi kwamba mafundi cherahani wameacha kuendelea kupunguza size ya kofia yake.

Leo hii Zitto anapoyamwaga matatizo ya Chadema (rushwa, ukabila na udini) wengi tunaona katenda dhambi! Ati tunataka akaongelee chumbani kwa Chadema, kana kwamba Taifa ni Chadema.

Huu ni upumbavu husiopimika; nchi inaliwa, ukabila na udini unaenea ndani ni nje ya Chadema, kadhalika democracy inanyanyaswa ndani na nje ya Chadema. Wachache wanaojitoa mhanga kukemea mambo haya hadharani tunawafanya wawe apologetic, kwa visingizio vya "kukeuka maadili" au kutunza "heshima ya chama". Huu ni upumbavu kwa herufi kubwa.

Chama kinatunza maadili gani kama wanachama wake niwapika majungu, wala rushwa, wakabila, wadini, na wazee wake hawatoi baraka zao kwa mwanachama anayetumia haki yake ya kimsingi ya kugombea uenyekiti?

Halafu hii kitu nayo inanisumbua: Hivi wazee wa Chadema ni akina nani na wana mamlaka gani ndani ya katiba ya Chadema? Mkutano wa wazee hawa huitishwa na nani? Mbowe? Slaa? Na ili niwe "mzee" wa Chadema natakiwa niwe wa namna gani? Wazee hawa ushauriwa na nani?
 
Leo hii Zitto anapoyamwaga matatizo ya Chadema (rushwa, ukabila na udini) wengi tunaona katenda dhambi! Ati tunataka akaongelee chumbani kwa Chadema, kana kwamba Taifa ni Chadema.

Unataka kubadili historia au wewe ndiye unataka Zitto akaongelee chumbani kwa Chadema? Zitto kaflip flop, kajichanganya, karopoka na zaidi ya yote, kaonyesha mapenzi yake yako mbali na chama chake.

Akikosolewa hapa ni makosa? Zitto si MUNGU kwamba hakosei na JF haina mtu ambaye haguswi. Zitto kachemka na anapata vidonge vyake kama wengine woooote.
 

Hivi kukemea kwake dhidi ya maovu ya Chadema ndio kigezo cha kumshutumu kwamba hana mapenzi na Chadema? Kumbe ukiwa kiongozi wa Chadema kamwe hutakiwi kukemea maovu ya Chadema hadharani hata kama maovu hayo ni pingamizi la juhudi za kumletea maendeleo Mtanzania!!

Nisingependa nishawishike kwamba ni Kweli chadema ina wenyewe...na nisingependa nishindwe kukubali kwamba "na wenyewe ni wachaga".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…