Great Thinkers,
Naomba tulitazame suala hili kwa umakini.
Jumamosi iliyopita, Mbunge Zitto Kabwe alitoa taarifa kwamba amepata taarifa juu ya kuwepo operesheni maalum ya kutaka kumnyamazisha(kumuua). Taarifa kamili ipo kwenye uzi huu >
Zitto: Kuna operation maalum ya kunimaliza (kuniua) - JamiiForums
Sasa, ndani ya masaa 48 tangu Zitto avujishe mpango huo, ikaja taarifa mpya kutoka kwa Spika.
Spika Ndugai amtaka Prof. Assad(CAG) kufika mbele ya kamati ya maadili vinginevyo atapelekwa kwa pingu - JamiiForums
Inadaiwa kuwa lengo la Spika Ndugai ni kujaribu kumnyamazisha CAG (SAI) asiendelee kuzungumzia madudu ya Serikali/Bunge. Hii kwangu haiwezi kuwa coincidence.
Kwa msingi wa taarifa ya Zitto, ambayo alieleza kuwa kuna operesheni maalum ya kummaliza SAI (kirefu chake ni Supreme Audit Institution) ambaye kiongozi wake ni Prof. Assad;
Naomba kuhoji kuhoji maswali 3 yafuatayo;
1. Je, Zitto alijihami akidhani mlengwa ni yeye badala ya CAG?
2. Je, Zitto anashiriki kwenye mipango hii kwa kuhamisha magoli makusudi?
3. Kwanini Zitto ajinasibishe na SAI?
Kwa kuwa tunaye humu jamvini, Itapendeza zaidi kama
Zitto mwenyewe atakuja kufafanua hili. Otherwise, karibuni nyote kwa mawazo yakinifu.