Je, zuio la mikutano ya upinzani kwa miaka 5 ni faida au hasara kwa waliotoa wazo hilo?

jo mose

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2020
Posts
3,476
Reaction score
4,074
Bashiru na polepole hawana tena uwezo wa kuiokoa ccm isife.

Chama kimegawanyika vipande vipande kwa sababu ya watu hawa wawili. Hawakuwahi kuwa wana CCM kabisa, wamekuja wameleta aidia za kizamani kabisa wakidhani Watanzania wako stone age. Hawa wapo chamani kwa maslahi yao tu ya kupata pesa, wala si kufanya chama kisonge mbele hata kidogo.

Wale CCM asili Waliokipigania chama hawataki kabisa kuwasikia hawa watu, wamekuja kuvamia chama, na kujiona wao ni bora sana kuliko waliowakuta.

Hawa ndio walikuja na wazo la kununua wapinzani. Unanunuaje mtu mmoja, wakati alipigiwa kura na maelelfu, yaani unachukua mayai, unaacha kuku, kuku ataendelea kutaga, halafu unashangilia umemkomoa kuku.

Hawa ndio walimdanganya raisi awekeze mamiradi ya fedha nyingi kuwa ndiyo yatakayompigia kura, leo hatuuziki kabisa kwa wananchi, unamwambia mtu tumejenga fly over wakati yeye anakunywa tope.

Hawa ndiyo walimsapoti raisi wetu, azibe mdomo vyombo vya habari visitangaze habari za upinzani, iwe ni CCM tu, leo sisi tunatafuta raia waje kwenye mikutano tena kwa gharama kubwa, wakati wapinzani wetu, raia wanamtafuta kwa gaharama zao mgombea wao kujua hata yuko wapi.

Ndio waliomdanganya ya kwamba upinzani umekufa, wamekaa kinafiki kabisa, leo kwa ground tunapata shida mnoo mpaka lazima tuwalazimisha watumishi woote wa serikali na wanafunzi kuja kuongeza vichwa kwenye mikutano yetu.

Walimdanganya sana mkuu kwamba anakubalika na asijali sana kelele za watu, ona mpaka leo tunafikia hatua ya kupiga magoti kwa raia tuliowaambia watalimia meno.

Yako mengi sana ndugu zangu, lakini kwa kweli tuna hali ngumu, kama chama tukubali tumekosea na hawa watu wawili wamesababisha magawanyiko mkubwa sana chamani. Sasa hivi tupo CCM asili na CCM Mpya, hii CCM Mpya ni kikundi kidogo sana cha Bashiru, Polepole na wahamiaji toka upinzani, ambao hawajawahi kuwa wana CCM, na wamekuja kuchukua nafasi za CCM asili waliokipigania chama.

Hawa watu wawili wamesababisha mpaka sasa tume ya uchaguzi na polisi wanaanza kutumika vibaya ili kuokoa jahazi, wakati chama kilipaswa kiwe na nafasi nzuri sana ya kushinda mwaka huu.
 
Dalili ya chama mfu ni kubebwa na dola badala ya hoja
 
Hakuna faida yoyote.Tatizo kubwa ni unafiki.naamini kuna watu wakubwa serikalini na ndani ya Chama ambao waliona hatari iliyokuwepo lakini kwa unafiki wakakaa kimya.Kama hukubaliani na mkubwa "UNAJIUZULU" nothing more nothing less!

Sasa leo anaachiwa JPM pekee yake. Natamani Tundu Lissu akamjibu Ndugai Kongwa, bunge limekuwa sehemu ya serikali
 
Muwe mmepata hasara au faida, ila sisi wananchi tumpata faida ya kutosikia makerere yenu muda wote wa miaka mitano
 
Umeandika ukweli mtupu. Ila mataga watapinga. Kupiga marufuku wapinzani kufanya siasa, kununua madiwani na wabunge, kujenga mamiradi makubwa ili tu kupata ujiko wa kisiasa, nk. vyote hivi vimeshindwa kabisa ni kumsaidia mgombea wa chama kongwe!

Ngoja avune alichopanda. Na Lissu anaendelea tu kuwanyoisha. Hakuna namna.
 
Bashiru na polepole hawana tena uwezo wa kuiokoa ccm isife.

Chama kimegawanyika vipande vipande kwa sababu ya watu hawa wawili. Hawakuwahi kuwa wana CCM kabisa, wamekuja wameleta aidia za kizamani kabisa wakidhani Watanzania wako stone age. Hawa wapo chamani kwa maslahi yao tu ya kupata pesa, wala si kufanya chama kisonge mbele hata kidogo.

Wale CCM asili Waliokipigania chama hawataki kabisa kuwasikia hawa watu, wamekuja kuvamia chama, na kujiona wao ni bora sana kuliko waliowakuta.

Hawa ndio walikuja na wazo la kununua wapinzani. Unanunuaje mtu mmoja, wakati alipigiwa kura na maelelfu, yaani unachukua mayai, unaacha kuku, kuku ataendelea kutaga, halafu unashangilia umemkomoa kuku.

Hawa ndio walimdanganya raisi awekeze mamiradi ya fedha nyingi kuwa ndiyo yatakayompigia kura, leo hatuuziki kabisa kwa wananchi, unamwambia mtu tumejenga fly over wakati yeye anakunywa tope.

Hawa ndiyo walimsapoti raisi wetu, azibe mdomo vyombo vya habari visitangaze habari za upinzani, iwe ni CCM tu, leo sisi tunatafuta raia waje kwenye mikutano tena kwa gharama kubwa, wakati wapinzani wetu, raia wanamtafuta kwa gaharama zao mgombea wao kujua hata yuko wapi.

Ndio waliomdanganya ya kwamba upinzani umekufa, wamekaa kinafiki kabisa, leo kwa ground tunapata shida mnoo mpaka lazima tuwalazimisha watumishi woote wa serikali na wanafunzi kuja kuongeza vichwa kwenye mikutano yetu.

Walimdanganya sana mkuu kwamba anakubalika na asijali sana kelele za watu, ona mpaka leo tunafikia hatua ya kupiga magoti kwa raia tuliowaambia watalimia meno.

Yako mengi sana ndugu zangu, lakini kwa kweli tuna hali ngumu, kama chama tukubali tumekosea na hawa watu wawili wamesababisha magawanyiko mkubwa sana chamani. Sasa hivi tupo CCM asili na CCM Mpya, hii CCM Mpya ni kikundi kidogo sana cha Bashiru, Polepole na wahamiaji toka upinzani, ambao hawajawahi kuwa wana CCM, na wamekuja kuchukua nafasi za CCM asili waliokipigania chama.

Hawa watu wawili wamesababisha mpaka sasa tume ya uchaguzi na polisi wanaanza kutumika vibaya ili kuokoa jahazi, wakati chama kilipaswa kiwe na nafasi nzuri sana ya kushinda mwaka huu.
Ni fundisho kubwa sana kwamba huwezi kuuwa vyama vya upinzani, tena ccm na m/kiti wake wamejiweka mahali pabaya kabisa.
 
Ni rahisi kufanya ngono kuliko kuuwa upinzani kwa kusomesha watu namba hizi itikadi zilifaa miaka ya 70
 
Back
Top Bottom