Jedwali la kodi za PAYE 2022 si la kitaalam

Hapa sasa ndio unazidi kunichanganya.
Magufuli mwaka jana alipunguza kodi 2% Ila hela iliongezeka karibia elfu 41.
Mwigulu kapunguza kodi 1% unasema itaongezeka 2500 ?
Unaona ni sawa ?
Kumbukumbu zangu zinaonnyesha kuwa punguzo la asilimia 2 lilfanyika July 2016, yaani kutoka 11% na kuwa 9% . Ukifuatilia mishahara ya june 2016 na July 2016 utagundua tofauti ya kodi ni kama shs 1500 hivi.
Mwaka jana kilichobadilishwa ni kima cha juu cha kutokatwa kodi kutoka 170,000 hadi 270,000 na wala si asilimia (zilibaki palepale) Mabadiliko hayo yalibadilisha tax brackets zote,zilikuwa:
170,000 - 360,000 kodi 9%
360,000 - 540,000 kodi 20%
540,000 - 720,000 kodi 25%
zaidi ya720,000 kodi 30%
Mabadiliko yakawa:
270,000 - 520,000 kodi 9%
520,000 - 760,000 kodi 20%
760,000 - 1,000,000 kodi 25%
zaidi ya 1,000,000 kodi 30%
Nadhani nimerahisisha mno maelezo ili wengi tuweze kuelewana (sikutaka kutumia lugha ya kile kinachozidi nk)
 
Sahihi kabisa kamanda
 
Hapa sasa ndio unazidi kunichanganya.
Magufuli mwaka jana alipunguza kodi 2% Ila hela iliongezeka karibia elfu 41.
Mwigulu kapunguza kodi 1% unasema itaongezeka 2500 ?
Unaona ni sawa ?
Ongezeko ktk mshahara ni sh 2,500 tu, hii ni kwa sababu wamepunguza %tu, magufuli alipunguza kiwango percentage na kima cha chini cha mshahara kinachotakiwa kukatwa kodi ndio sababu iliongezeka 51,000
 
[emoji24][emoji24][emoji24]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ongezeko ktk mshahara ni sh 2,500 tu, hii ni kwa sababu wamepunguza %tu, magufuli alipunguza kiwango percentage na kima cha chini cha mshahara kinachotakiwa kukatwa kodi ndio sababu iliongezeka 51,000
2500 kwa mtu wa laki 9. Je kwa laki 3 itakuwaje?
 
Hivi gratuity inakatwa kodi mwaka huu wa bajeti?
 
Kamakabuzi , hili hapa liko sawa mkuu?
 
Punguzo la kodi la 1% lililotangazwa na Rais ndio tumepigwa mwingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…