Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Naanzisha maudhui haya kwa minajili ya kuwafungua macho watu wengi ambao hawajapata nafasi ya kutembea, na ambao siku zote wanalishwa propaganda za watawala. Kwamba nchi ina amani, mshikamano bla bla bla.
Zamani walikuwa wanatoa mifano ya South Afrika, Angola, Namibia n.k. jinsi mtu mweusi anavokandamizwa huko na kuwa Watanzania wako huru na inapasa kujivunia nchi yao.
Ila mapambano yalipogeuka kuwa ya uchumi wakawa hoja hizo hawanazo. Sasa nadhani hoja moja tu wanayo, nayo ni ile ya amani. Hii pia inatafunwa siku hadi siku kutokana na kupungua mno kwa migogoro Afrika.
Katika matembezi yangu, na kusema kweli nimetembelea nchi ambazo zilikuwa katika vita tangu 70 au 80s, kama Chad,Sudan hata Somalia. Ila kitu kimoja ambacho Tanzania ni tofauti kabisa, ni jinsi maisha ya raia wengi yalivyo duni na mabaya. Kwa hili, hata Somalia ina afadhali. Bila shaka, ni uongozi mbaya, tangu uhuru, ndio ilioifanya Tanzania kufikia hapa, ingawaje ina utajiri mkubwa.
Kama mtu ana jina la nchi yeyote duniani ambayo raia wake wengi wanaishi maisha duni, ya kudhalilishwa na watawala, kuliko Tanzania....aitaje.