Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Ili sarafu ya nchi iwe na thamani ni lazima iwe na mukabala wake katika dhahabu. Najua hii ni sera ya zamani ya uchumi, lakini tangu matatizo ya fedha ya dunia kulipuka, wengi wanaona turudie kwenye 'dhamana' hii ya dhahabu.
Nimesoma kuwa Misri ina akiba ya tani 76 za dhahabu ambazo zinaisadia sarafu yake hivi sasa isiporomoke thamani, ingawaje nchi hiyo inakabiliwa na matatizo makubwa ya kisiasa.
Tanzania ni nchi inayotoa dhahabu kwa wingi. Nadhani ni ya tatu au ya nne barani Afrika kwa utoaji wa dhahabu. Swali ni hili: Jee tuna akiba yeyote ya dhahabu?
Nani anayejua kiasi cha akiba ya Tanzania ya dhahabu, wana JF?