Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Whaat? hivi mwizi ukiiba ukijulikana ukirudisha ulichoiba ndio basi hamna hata kesi ni msamaha tuu? Hivi seria ya wahujumu uchumi inasema je? na kuhusu wizi sheria nayo inasema je?
Katika Taifa hili la Wadanganyika sidhani kama kutakuja tokea jipya labda karne ya 25. Nimetazama matokeo mengi ya uchaguzi mdogo tena yote yakiwa katika scandal kubwa kubwa (Mfano ile ya Buzwagi na hii ya BoT) lakini ndio kwanza CCM wamejizolea kura..Na sababu kubwa ni kwamba CCM wanafahamu kumwongoza kipofu kwa fimbo yake sio maneno, ishara,darasa ama maelekezo ambayo hutumiwa na vyama vya Upinzani. Wadanganyika sii wajinga nadhani wengi wetu vipofu wa akili (haioni mbali zaidi ya marefu ya mkono).
Kifupi, Ukitaka kupata mafanikio TZ basi usije akifikiria nje ya mfumo mpya wa Chumuka Chako Mapema laa sivyo basi upo karne moja nyuma ama enzi za Ujamaa. Naanza kuamini kuwa ukipewa madaraka, mshiko, panga nchini Tanzania basi ni Ujuha kama hutaitumia nafasi hiyo kujitajirisha.
Potelea mbali maslahi ya Taifa, hayo yatajengwa na kizazi kijacho mwaka 2500. Inauma sana lakini ndio reality!
Thaksin Shinawatra, the deposed former Thai Prime Minister, was greeted with a hero's welcome in the capital Bangkok yesterday as he returned home to face corruption allegations. ... ... ... ...
... ... After arriving, he was immediately taken to Bangkok Criminal court to answer a charge of abuse of power.
Ukiona Jeetu Patel karudi wakati Ballali kajificha basi ujue mazingaombwe yamepamba moto... hafungwi mtu wala nini badala yake ndio kwanza tutaanza kuwapigia makofi na kuwasifu, ama kweli as our very own Nyani Ngabu would say "waafrika ndivyo tulivyo"!
![]()
![]()
K akimpongeza mai waifu wake Mama Slama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kuchangia shilingi milioni moja katika mfuko wa elimu wa wilaya ya Bagamoyo wakati wa harambee iliyofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni.Katika Harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni tisa zilichangwa.Katikati ni Mwenyekiti wa harambee hiyo Bwana Jeetu Patel.
Click link uone Picha
Source: http://bp1.blogger.com/_HO8ijU76ZcQ/R8l_RQ556PI/AAAAAAAAOL0/ybfiryCHkYs/s1600-h/DSC00509.jpg(Picha na Caption)
Wabillah Tawfiq
huyo katikati siye jitu tapeli,ni muhindi mwingine tu.
Hivi jamani BALALI kafia wapi????? kwani kwenye news simsikii tena. Lakini naona BALALI kwa kuwa anajua mengi kuhusu ufisadi wa CCM anaweza kuambiwa akeep low profile wakati mambo yakipoa.
mmoja wa watu wanaotajwa kuhusika na wizi wa fedha za EPA Bw. Jeetu Patel imethibitika yuko Dar ambapo anasubiri kibano cha mahojiano siku chache zijazo. Haijajulikana ni ushawishi gani umetumika lakini vyanzo vya kuaminika vinaonesha kuwa kinachosemwa kurudishwa fedha za "EPA" ni mojawapo ya dili ambazo Jeetu kapewa ili asipambane na kibano kikubwa zaidi.
Mpango ulipangwa ni kuhakikisha baada ya kurudishwa fedha nyingi za EPA basi watakapotajwa hadharani, kutakuwa na sympathy kwa wahusika na logic itakuwa "waliohusika wameonesha uzalendo wao, na walitambua makosa na kwa vile wamerejesha kiasi kikubwa basi tunaamini kuwa hawatarudia tena". Makofi yatapigwa mwenye kusifiwa atasifiwa na shujaa atajulikana.
ebwana tutapataje picha ya Jeetu Patel?
Nanusa harufu ya kitu kama hicho!!! by the way, mtoto wako akikosea kosa kubwa kawaida haumuadhibu... nature ya binadamu...
Mfano mtoto wako amevunja glass... utampatia kibano cha hali ya juu... je akichoma nyumba ... no way... hakuna kibano chochote!!! Hili la Jeetu Patel linaelekea huko...