Jeff Lea punguza Uinglishi tafadhari

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Kwa kweli mie nakereka mno kumsikia huyu jamaa kwenye vipindi vya michezo radio E FM ya Dar.

Huyu ndo anajifanya mchambuzi wa michezo hasa soka hapa nchini lakini hata neno jepesi tu la Kiswahili yeye atalitamka Kiinglishi. Anajimwambafai kutaka tumuone kazowea Uinglishi sana au vipi sijui, watangazaji wengi wanaifahamu lugha hiyo lakini nadra mno kumsikia akijikokotoa kutafuta neno la Kiinglishi na hata baadhi ya wachambuzi wenzake.

Nausihi uongozi wa hiyo radio kumshauri apunguze kujimwambafai kwa lugha ya wenzetu kwani maneno ya Kiswahili yapo mengi tu kwenye soka.

Aksanteni.
 
1. Kiingereza ni lugha yetu pia, so si ajabu kuongea kiingereza, ingekuwa anaongea kireno hapo ungekuwa na point kwa sababu hiyo si lugha yetu. Unaona hata mimi nimechanganya kiingereza ili tuelewane?

2. Kuna mazingira ukiongea kiswahili unajitesa mwenyewe. Kwa mfano mkiwa na wapasua mbao hata ambao hawakugusa darasa moja, vipimo vinavyotumika ni english tupu.

Kwenye mpira huwezi kukwepa english, mfano; penalt, winger, ball possession, foul, midfielder na mengine mengi.
 
Shida kaajiriwa kwa connection na siku hizi wanadanganyana eti "kipaji"

elimu imewekwa kando,sifa ya kuajiriwa saivi imegeuka eti "kipaji" kisha

elimu ndio ifate,muulize uandishi habari alisomea wapi na mwaka gani?

na alianza fanya kazi media gani kabla ya kuwa pale alipo,majibu atakayo

kupa ndio utajua siku hizi wenye elimu za fani husika wameachwa nyuma

wanaajiriwa watu kutokana na muonekano wao,ushawishi wao,nk,tusubiri 2040 tuone tutakua wapi.
 
Tatizo kasoma Kenya na SA
 
Ni utoto tu akikua ataacha.
 
alianza kazi tbc
 
huyu jamaa ana elements za u slay queen, ata kule tweeter utadhan hajawah kuishi bongo na lugha mama inamsumbua, sijui baadhi ya wabongo tunakwama wapi!
 
Bila kuongea lugha ya malkia atajuaje Kama mnajua Kama amesoma M.Tc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…