Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Wapo watakaosema kuwa magereza hatari kwa vijana inaweza kuwa ni Komboinsin Juvenile Prison kutoka Burkina Faso, ama lile gereza la Gitarama ambalo kwa sasa linaitwa gereza la Muhanga kwa Kagame lililopo ndani ya taifa la Rwanda, ama gereza la Nsinda.
Lipo kundi la watu wengine watakuja mbele na kudai kuwa gereza la Chikurubi ndani ya nchi ya Zimbabwe ndio linashika nafasi ya kwanza. Ila hata ukisema gereza la Addis Ababa Remand Home ama, Magereza ya Watoto Nigeria (Alagbon, pamoja na Kano) bado kuna gereza moja lilikuwa ni moto wa kuotea mbali haswa kwa wafungwa ambao walikuwa ni vijana wadogo.
Ndani ya mji mdogo wa Marianna, uliopo ndani ya jimbo la Florida, Marekani, palikuwa na jengo la kutisha ambalo ndani yake lilificha mateso ya kutisha kwa zaidi ya karne moja.
Dozier School for Boys – awali gereza hili lilikuwa likifahamika shule kwa jina la Florida State Reform School – lilianzishwa mwaka 1900 kama taasisi ya marekebisho ya tabia na miendendo ya wavulana waliodaiwa na kukutwa na hatia za uhalifu, matumizi ya silaha haramu pamoja na mauaji.
Lakini nyuma ya pazia la nidhamu na maadili, kulikuwa na giza la mateso, ulawiti, mauaji, na vifo visivyoelezeka.
Katika kipindi cha zaidi ya miaka 111 ya uendeshaji wake hadi kufungwa mwaka 2011, zaidi ya watoto 120,000 walipitia gereza hili, huku wengi wao wakipitia shurba isiyo ya kawaida kabsa. Wengi waliingia ndani ya shule hiyo kutokana na makosa madogo kama wizi mitaani, kutoroka nyumbani, kushiriki kwenye vitendo vya uhalifu au hata kwa sababu tu ya kusingiziwa na watu.
Lakini walichokutana nacho humo kilizidi ubaya wa kosa lolote, kwani ilikuwa ni dunia nyingine tena yenye utofauti mkubwa sana. Kama nje mtoto alidhania kuwa kukutana na wauaji ni jambo la hatari basi ndani ya Dozier School for Boys ilikuwa ni mara tano yake, hii shule ilikuwa ni Devil’s Private Office ilikuwa ni hatari zaidi ya kukutana na John Dillinger, Charlie Wall, ama genge la uhalifu la The Ashley.
Wapo watu walipaita majina maarufu kuonesha kuwa haikuwa shule ya kawaida hata kidogo, wakazi wa 7th Avenue waliibatiza shule hii jina la Devil’s Little Paradise, kwamba ni paradiso ndogo ya mzee baba Shetani huku wale wanaoishi mitaa ya Franklin Street wakipabatiza jina White House, mahala ambapo palikuwa panaishi ndoto mbaya kwa wavulana waliokuwa wakikosea au kuadhibiwa bila sababu.
Humo ndani watoto waliofungwa, endapo ukifanya kosa basi walikuwa wakipitia mateso haswa kama watu wazma, wapo waliopigwa kwa mijeledi hadi kupoteza fahamu, wengine walifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia kwa kulawitiwa na wahudumu.
Mmoja wa manusura, Robert Straley, alisimulia kuwa aliteswa vibaya akiwa na miaka 13.,“Nilipewa kipigo kama vile jambazi sugu, sikuwa na usaidizi na nilisubiri kifo maana nilijua kuwa nitakufa kwa hakika. Kilio chetu kilikuwa ni kama sauti tamu za vifo,” alisema.
Wakurugenzi wakuu na waandamizi wa shule ya Dozier School for Boys walibadilishwa mara kadhaa, lakini baadhi yao waliandamwa na tuhuma nzito.
Mzee baba Arthur G. Dozier, ambaye shule hii iliitwa kwa heshima ya jina lake, aliongoza kwa miaka mingi huku ripoti za mateso zikiendelea chini ya uongozi wake. Wafanyakazi na wasimamizi wa shule hii walihusishwa na njama ya kuficha taarifa kuhusu vifo na kuzikwa maiti kwa usiri mkubwa sana, baadhi ya makaburi yenye maiti nyingi zilizozika pamoja yalikuja kugunduliwa miaka mingi baadaye.
Hata Mary Zahasky alipoingia kama superintendent mwanzoni mwa miaka ya 2000 alidumu kwa kipindi kifupi kwani 2009 alikubali kujiuzulu mara baada ya kuonekana kuwa hali ya usalama na afya ndani ya shule hii haukuwa mzuri, alivyotoka tu, James Godwin ambaye alikaa ofisini mpaka 2011 ambapo shule hii ilifungwa rasmi.
Mwaka 2012, timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha South Florida waliingia kazini huku timu hii ikiongozwa na Dr. Erin Kimmerle, walichimba na kugundua zaidi ya makaburi 100 – mengi yakiwa hayajulikani maiti ambao waliozikwa humo.
Serikali ya jimbo la Florida ilithibitisha kuwa watoto wengi walikufa kwa kupigwa, njaa, na uzembe wa huduma za afya. Taarifa ya watafiti hao walionesha wasiwasi kuwa wapo watoto ambao walipoteza maisha baada ya vipigo vizito haswa sehemu za kifua na kichwani.
Miongoni mwa waliowahi kufungwa hapo akiwa bado janjaro ni Roger Kiser, ambaye baadaye aliandika kitabu cha kumbukumbu zake: The White House Boys. Aliwasimulia marafiki zake waliopotea, waliouawa au waliotoweka ndani ya shule hiyo pasipo taarifa yoyote.
Mwandishi Colson Whitehead, kupitia riwaya yake The Nickel Boys (moja ya riwaya bora sana ambayo iliteka soko la vitabu duniani), alihifadhi kumbukumbu ya kisa hiki kwa njia ya fasihi, akifichua uovu na ubovu wa mfumo wa marekebisho haswa wa shule na magereza ya vijana.
Ndani ya The White House Boys kulikuwa na ubaguzi haswa kwani watoto wa kiume wenye asili ya ngozi nyeusi hawakupewa adhabu sawa na wale ambao ni wazungu, hata baadhi ya huduma za kijamii watoto wenye ngozi nyeusi walipitia changamoto za kiafya zaidi kuliko watoto wa kizungu, ingawa kwa wakati mwingi watoto wote waliona moto wa gesi ukiwanyoosha.
Gereza la Dozier haikuwa tu ni shule ya kurekebisha tabia za vijana bali ilikuwa ni mahala ambapo bila shaka shetani alikaa kwa utulivu akishuhudia namna vipenzi vya Mungu vinavyotiana mateso pasipo huruma yoyote. Humo ndani aliishi Shetani bila shaka.
MOJA YA KAULI MBAYA ILIYOTUMIKA NDANI YA DOZIER SCHOOL FOR BOYS ILIKUWA NI "JUTIA KOSA KABLA HUJAAMUA KUKOSEA KWA MAANA UKIKOSEA UTAJUTA KWANINI ULIKOSEA."