Jela Kifungo cha Maisha kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka 9

Jela Kifungo cha Maisha kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka 9

Joined
May 24, 2017
Posts
11
Reaction score
14
Mahakama ya Wilaya ya Temeke imemuhukumu Mkazi wa Chamanzi, Said Wanie (35) kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Pia mahakama hiyo imemuagiza mshtakiwa huyo kumlipa mtoto huyo fidia ya kiasi cha Sh500,000.

Kati ya Mei 3, 2020 maeneo ya Chamanzi Wilaya ya Temeke mshtakiwa huyo alimlawiti mtoto huyo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi, Anna Mpessa alisema mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyotolewa na daktari vikionyesha kuwa mtoto huyo amelawitiwa.


Chanzo: Mwananchi
 
Kunae mmoja mtaani kwetu kambaka mtoto wake wa Miaka 9 Ila saiv anadunda tu uraiani
 
Zamu yake, kwenda kupumuliwa na nyampara huko segerea
 
Back
Top Bottom