Jela kwa kukataa chanjo

KJ07

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2021
Posts
2,370
Reaction score
5,381
Watu saba wote Wakazi wa Kijiji cha Kalambo Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela kila mmoja na Mahakama ya mwanzo Wilaya ya Kalambo baada ya kugoma Watoto wao wenye umri kati ya miezi 9 hadi 59 wasipewe chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubela wakidai chanjo sio maagizo ya Mungu.

Hukumu hiyo imetolewa February 26,2024 na Mahakimu wa Mahakama hiyo Elis Mkama na Suzy Mkinga kwa Washtakiwa hao ambao ni Abiniel Isaya (27), Misheck Simon (28), Isack Simon (26), Yona Simon (30), Efeso Peter (28), Job Simon (36) na Joshua Meshack (40)

Akitoa taarifa kuhusu hukumu hiyo leo February 27, 2024, RPC wa Rukwa, Shadrack Masija amesema chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa na Wizara ya afya katika Kijiji hicho February 18, 2024, ambapo sababu ya kugomea ni imani ya dini yao ya Kanisa la Watchtower kwamba chanjo sio maagizo ya Mungu.

RPC Masija mesema “Kugomea chanjo inayoelekezwa na Serikali ni kufifisha juhudi za Serikali za kupambana na maradhi hivyo amewahimiza Wananchi wazingatie maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Serikali na wazitii Mamlaka za Serikali kwani zimewekwa na Mungu ambaye ndiye wote tunamwabudu”

CREDIT: MILLARD AYO

 
Dhehebu ni 'watchtower' au Mashahidi wa Jehova, ambao wanachapisha vipeperushi vyenye jina watchtower?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Katika huduma za kitabibu, kuna Uhuru wa kukataa matibabu, ila unakiri kimaandishi kukataa hiyo huduma. Wangehukumiwa pale ambapo, kuna madhara kwa wale waliokosa huduma kutokana na maamuzi yao.
Katiba mpya inahitajika katika kila nyanja kwa kweli!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Nataka kifungu cha Sheria kinachompa hakimu ruhusa ya kumfunga mtu anayegomea chanjo.
Hao walikuwa wanawavizia kitambo, chanjo ilikuwa chambo tu
Kesi ya Mauaji ya watoto wadogo
Watoto hawajagoma bali wao watu wazima wanazuia haki ya mtoto kuishi kwa kuchanjwa kuzuia asipate maradhi ya kumuua ndio wanashinikiza watoto wasichanjwe ili wafe
Huyo hakimu kawapa adhabu ndogo sana Serikali ikate rufaa wapewe hukumu kubwa zaidi
 
Kifungu gani cha sheria wamehukumiwa nacho?

Chanjo ni muhimu
Matumizi ya akili kwenye sheria yanaashiria mafanikio ya chanjo alizopata mtoa hukumu
 
Nakubaliana nawe, ni njia ya kutisha watu wasiwe na uhuru wa Imani zao kama ilivyoainishwa na katiba.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Serikali zote zinawaogopa watu wanaomwabudu Mungu kwa u serious bila kujali dini yao.
Mtu yeyote aliye serious na Imani yake anaweza kuikosoa serikali muda wowote akaharibu hali ya hewa.
Serikali inapenda wachungaji wazinzi, masheikh ubwabwa na mapadre wazinzi ambao kazi yao kubwa ni kuipongeza serikali
 
Huu ndio ukweli
 
Nakubaliana nawe, ni njia ya kutisha watu wasiwe na uhuru wa Imani zao kama ilivyoainishwa na katiba.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Sio kweli

Ni kosa kisheria kuzuia mtu mwingine asipate tiba ni sawa. Na kuzuia askari asifanye kazi yake

Hao walikuwa wanazuia watu wengine yaani watoto wasipate tiba na kuzuia madaktari kufanya kazi yao
 
ulishawahi sikia kesi ya hospitali ya bichi pale mbezi.....?

ukielewa nia basi hata wanao utadhibiti nini cha kuwaingia mwilini mwao.
 
Soma Public Health act ya Tanzania
 
Mashahidi wa Jehova hata ukipata ajali huruhusiwi kuongezewa damu ya mtu mwingine ni marufuku kwa imani yao
 
Kila mtu abaki na maamuzi yake ,kosa ni kuhamasisha ila kama hawajafanya hivyo, basi ni uonevu.
Kuna maamuzi binafsi lakini ogopa kufanya maamuzi juu ya mtu mwingine mfano kuzuia mtoto asipate chanjo kitu ambacho ni hatari kwa Maisha yake mtoto ni kuyaweka Maisha ya mtoto hatarini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…