Jela maisha kwa kumnajisi mwanae

Jela maisha kwa kumnajisi mwanae

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MAHAKAMA ya Wilaya ya Temeke imemuhukumu kifungo cha maisha kijana wa miaka 26 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumnajisi mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitano.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Aziza Kalli wa mahakama hiyo, alisema kuwa baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, mtuhumiwa huyo, Halfan Abdallah, 26, ameonekana kuwa na hatia katika kosa hilo.

Akisoma maelezo ya awali, Kalli alisema kuwa mnamo Mei 15 mwaka jana, majira ya 11:00, maeneo Kibumo Kigamboni, mtuhumiwa alimlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtuhumiwa alijitetea akisema: "Mheshimiwa, naomba unipunguzie adhabu ya kifungo kwa kuwa hivi sasa nilipo, ninaumwa ugonjwa wa henia (busha)... hapa nilipo ninaumwa kweli, na tatizo linalonisumbua ni henia, kwa hiyo naomba unipunguzie adhabu ya kifungo.”

Hata hivyo, ombi hilo lilipingwa na Hakimu Kalli aliyeeleza kuwa sheria ipo wazi na inasema kuwa atakayefanya kitendo kama hicho kwa mtoto aliye na umri chini ya miaka kumi, anastahili kifungo cha maisha.

“Kitendo alichofanya mtuhumiwa kinastahili adhabu ya kifungo cha maisha,” alisema Hakimu Kalli.

Mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Isaya Mwanga aliieleza mahakama hiyo kuwa kitendo alichofanya mtuhumiwa ni kibaya ikizingatiwa kuwa ni mzazi wa mtoto huyo na kwa hiyo anastahili adhabu kali.

Hukumu hiyo ilitanguliwa na ushahidi kutoka kwa watu watatu, akiwemo mtoto aliyefanyiwa vitendo hivyo, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kibugumo na ofisa mtendaji wa Kata ya Kibugumo wilayani Temeke.

Akitoa ushahidi mtoto huyo aliieleza mahakama kuwa kijana huyo alikuwa akimfanyia mwanae vitendo hivyo wakati wa usiku na baada ya kupiga kelele ndipo majirani waliposikia na kwenda kumsaidia.

Alisema baada ya majirani kufika eneo la tukio na kujua kilichotokea walitoa taarifa kwa ofisa mtendaji huyo ambaye alimkamata mtuhumiwa na kufikisha kwenye mikono ya sheria.

Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kibugumo alisema baada ya kupokea taarifa hizo alifanya uchunguzi na kubaini ukweli wa taarifa hizo na ndipo alichukua mtoto huyo na kwenda hospitali ambako alipimwa na ukweli kubainika kuwa alikuwa akifanyiwa vitendo hivyo.

Jela maisha kwa kumnajisi mwanae
 
duh hiyo kiboko - tena ka kijana kake ka kiume miaka 9 - naungana na mdau kuwa ana mashetani ya ngono jamaa hakuwa mzima - mi nafikiri adhabu inamtosha kama ana jeuri akafanye ushenzi huo huko gerezani hatufai kwenye jamii kabisa.
 
Back
Top Bottom