Jela miaka 30 kwa kumbaka shangazi yake

Jela miaka 30 kwa kumbaka shangazi yake

Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu Reiga Innocent (21), mchimbaji wa madini na mkazi wa Iwindi, Mamlaka ya Mji Mbalizi , kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka shangazi yake mwenye umri wa miaka 63.

Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba 13, 2026 na Hakimu wa mahakama hiyo, Tedy Mrimba, baada ya mahakama kuridhika kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 29, mwaka huu.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio, mshtakiwa alifika nyumbani kwa mhanga majira ya jioni na kumkuta akiwa peke yake, kabla ya kumshika kwa nguvu na kumbaka.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Imelda Luko, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo, kwa lengo la kukomesha vitendo vya ukatili wa kingono.

Chanzo : Nipashe

Nchi ya kianithi sana hii ...vitendo vikubwa vya kihalifu watu awafungwi vifungo vikubwa ila mahakama zinahukumu vifungo vikubwa kwa mambo ya UCHI ....Uwezi kuwa na mfumo wa kipumbavu na kianithi namna hii kisha nchi ikawa sana ..kosa lolote linalousu mambo ya uchi ilitakiwa kifungo kikubwa kabisa ni miaka 2 hadi 4 tu labda ilo kosa liwe na makando kando mfano brutal rape nk
 
Zipo kesi za kwenda jela mwanaume, sio masuala ya utelezi na wanawake mkuu.
Kabisa bwashee, nikiwa moro kuna muha mmoja alitaka kuning'oa meno kisa anadai nilim,,,mb,,,,a demu wake , dah yani ni ushamba wa hali ya juu kupanic mambo madogo wakati maisha bado yanahitaji energy na akili kuvuka.

Kujifunza namna ya kujikontrol ni muhimu sna asee majuto ni mjukuu
 
Jamaa atatoka akiwa na miaka 51

Unatoka jela ukiwa huna nyumba, watoto, ajira wala biashara ya kumpa kipato

Kuna wakati mwingine, vyema kuongozwa na kichwa cha juu badala ya hivi vichwa vyetu vya Chini

Angeweza kwenda pale Mafiati, kwa shilingi 5,000 angepunguza uzito

Ama vipi sabuni ya 500 tu angepunguza uzito 🙌

Anyways, majuto mjukuu
 
Kwa mishepu iliyopo mbeya huwez kuwa mzima wa akili ukamtaman shanganz yako mzee ivyo ,ameshindwa hata kwenda mafyati pale akaokota mtumwa mmoja ,na chochote kimkute jela pia💯
Hio akili watu wengine hua hawana wanajifanya Mungu Mungu sijui Mungu kufanya nini mwisho anajinyonga mwisho anabaka kwanini usiende kununua malaya wamejaa kibao pale Mbeya Pazuri hadi Mafiati ukapoa zako maisha mengine yakaendelea kwani lazima mpaka ubake kibibi cha miaka 63?
 
Ukiyatafakari maisha,utagundua hapa Duniani kila kitu ni fake,ni binadamu waneamua kuvihalalisha baadhi ya vitu fake,na hivyo ndivyo vinavyotesa binadamu wengi.

Ukiwa unaangalia namna watu Wanavyomiliki biashara kubwa na miradi mikubwa unaweza kuta unapata kisukari.

Ukisema uangalie mahusiano ya watu Kwa nje unaona majamaa yanamiliki wanawake wazuri Kwa Sura na bright kichwani,na wanaonekana wakipendana huku wewe mahusiano na NDOA yako vikipumulia mipira.

So maana yangu ni nini,

Kila unachoona Bora Kwa wenzio,huo ubora unawapa wewe,na unawapandisha kulingana na Aina ya maisha yako unayoishi.

Niliwahi kwenda Kwa Jamaa mmoja ni mtu wa Shinyanga huko ila anaishi mkoa mmoja kusini mwa Tanzania,jamaa kiumri nimemzidi kama miaka minne hivi ,ila jamaa anamiliki Mali za kufa mtu,Kwanza ana watoto 22,ana wake watano wanaoishi sehemu moja,ana mashine za umwagiliaji kwenye shughuli zake za kilimo,ana mashine za usagaji na ukoboaji wa nafaka ikiwa huduma hiyo anatoa kijiji kizima na vijiji Jirani.

Ana Toyota Hilux tatu kwaajili ya mizunguko ya shambani kwake. Ana combine mbili kwaajili ya kuvunia mpunga,ana trekta ambazo sikujua idadi yake pamoja na powertillers.

Ana Fuso mbili kwaajili ya kusafirishia mazao yake mpunga na ufuta kwenda kwenye godown la kijiji chini ya chama cha ushirika wa wakulima.

Ana godown lake mwenyewe ambalo siyo fuso zinapark nje zipakie mizigo Bali zinaingia ndani.

Hapo nyumbani kwake kuna watu wasiopungua Hamsini kila siku wapo vibarua wa kulima,kupanda kupalilia,wapo wanaochunga mifugo n'gombe, mbuzi,kondoo na punda.

Yaani vyakula vinapikwa kila muda kama vile kuna send-off au sherehe fulani kumbe ni maisha ya watu ya kila siku.

Huyu mtu anazungumzia Milioni mianane kama anazungumzia elfu nane.

Mimi nilijifanya chizi wa bia ,kumbe jamaa ana mafriji hapo hapo nyumbani na zikiisha ana pikipiki matairi matatu anaenda kwenye godown la beer analeta zake pombe na life linaendelea,
Niliinjoi mtu kaishia darasa la Saba lakini anatembelea gari ambayo Mimi sina.

Lakini yote hayo nilijua ni ubatili tu,maisha yanapita ukiwaza sana unaweza kufanya vitu kwasababu ya ujinga.

Kubaka wazee au watoto ni mashariti ya kishirikina kwasababu ya kutafuta maisha mazuri.

Ndugu zangu maisha mazuri yapo tu

Stay safe
Enjoy life.
 
Kwanini afungwe? Wakati nature ndio inataka hivyo? Kwahiyo mahakama ziko against na nature??
 
Back
Top Bottom