MPIRA WA TANZANIA UMEJAA WATU WAJINGA - JEMEDARI
Hivi yupo mtu anafikiri kwamba Mangungu akiondoka ndio timu itacheza vizuri?. Sifikiri hivyo, ni kauli aliyoanza nayo mchambuzi na mdau wa soka nchini Jemedari Said akiongea na waandishi wa habari Novemba 09, 2023 akitoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kwenye klabu ya Simba na kusisitiza kuwa, haya yote yanayotokea wameyataka wenyewe mashabiki wao na wao kama wadau walishaonya dhidi ya haya yanayotokea.
Jemedari ameendelea kwa kusema kuwa, wao kama wadau walishaonya lakini wanachama na mashabiki wa Simba SC walitoa majibu ambayo ameyaita ni mepesi kwamba wana furaha na kwenye timu kinachotafutwa ni furaha.
"Kwa bahati mbaya mpira wa nchi hii una watu wengi wajinga, wakati Simba wanabadilisha katiba na watu walikuwa wanawaambia kuwa mnafanya makosa, majibu yao yalikuwa mepesi tu kwamba sisi tuna furaha na kwenye mpira sisi tunataka furaha, mwacheni Dewji afanye chochote anachokitaka" alisema Jemedari
Jemedari ameongeza kuwa, inapotokea Simba ikifanya vizuri inakuwa ni ya Dewji na upande wake lakini ikifanya vibaya ni Mangungu ya Mangungu na wanachama jambo ambalo analiita ni wanachama kutumika kwa kujua au kutokujua
"Timu ikifanya vizuri ni ya Dewji na upande wake lakini ikifanya vibaya ni Mangungu na wanachama, ni aidha wanachama wanatumika na hawajui wanatumika huku wanajua" alisisitiza Jemedari na kuongeza
"Alivyomaliza Dewji katika nafasi ya mwenyekiti wa Bodi akamuachia Try again hivyo basi Try again kama ni tatizo basi tatizo kubwa ni Mohamed Dewji kwa maana yeye ndio amemweka"
Jemedari amemkingia kifua mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu kwamba yeye asilaumiwe kwa kuwa hana nguvu kikatiba na sio yeye amependa kuwa hivyo ni bali wanachama na mashabiki ndio wameamua awe hivyo.
View attachment 2810768