Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Mkuu kuna watu ni km nguruwe ndo hilo jamaa kisa lina kaa kwa shemeji yake linaona ni sawa tu watu wasipewe stahiki za.
 
JWTZ hawana sera ya kuwalinda watu ambao wanakuwa trained kwa kiwango cha Ukomandoo, hawa jamaa walitelekezwa na wamepitia wakati mgumu mno.
Kwa hiyo wanajilinda wenyewe?
 
Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa kama haina "database" ya watumishi wake wa vyombo vya usalama basi ianze sasa mara moja bila kujali watumishi hao wametoka kwenye vyombo hivyo kwa sababu gani kama kustaafu, kufukuzwa, utoro, kuacha wenyewe, ulevi, kuugua, n.k.. Kukiwepo na "databse" (siku hizi teknolojia imerahisisha kila kitu) itakuwa rahisi sana kwa serikali kujua nani yupo wapi anafanya nini na ni namna gani wanaweza kuwasaidia wakiwa nje ya majeshi yetu inapotokea kuna fursa au kama kuna mtumishi kapata tatizo. Lakini kitendo cha kuwaacha tu mtaani watu waliopata mafunzo ya hali ya juu ya kupambana na maadui ni hatari sana kwa raia wa kawaida. Hao watu wana familia zinazowategemea sasa je wakikosa njia halali za kulisha familia akitokea mtu muovu akawaunganisha pamoja kwa mfano makomandoo 10 tu hivi si hata polisi wanaweza kukimbia vituo vyao polisi?

Na watu wengi wamelalamika hapa kuwa ndugu zao waliokuwa jeshini kuwa walifukuzwa bila kupewa chochote sasa sijui lina ukweli kiasi gani. Kwa mtizamo wangu naona serikali inapaswa ilifuatilie hili jambo kwa haraka sana ili kupata ukweli wake. Na ikiwezekana iundwe tume huru nje ya jeshi ambayo hao watumshi watapeleka malalamiko yao kwani watu wamesema hapa kuwa walishapeleka malalamiko yao jeshi na hayakufanyiwa kazi. Lengo hapa liwe kujua kweli kuna malalamiko kweli au hakuna. Na iwapo kutakuwa na ukweli ndani yake basi hao watu wapewe stahili zao haraka sana kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Lakini vile kuwepo na utaratibu ambao kila mtumishi wa vyombo vya usalama anapoacha au kufukuzwa walau apewe "a certain minimum amount" akanze maisha mapya ya kiraia bila kujali kastaafu, kafukuzwa, kaacha mwenyewe, n.k. kutokana na unyeti wa kazi hizi za vyombo vya usalama.

Kila siku viongozi wanapopiga kelele uzalendo basi wajue kuna gharama za kuwafanya watu wawe wazalendo. Raia akikosa uzalendo ni tatizo lakini hao watumishi wa vyombo vya usalama wakikosa uzalendo Inawapasa viongozi wetu wajue kuwa ni tatizo kubwa sana na ni bomu litakalokuja kulipuka baadae. Kwa hiyo ni vyema basi serikali ijatahidi sana kutatua changamoto zao kwa wakati.

Ni mtizamo tu.
 
Ww Hamnazo Mkuu hatuna CDF anayeitwa Mabeho Nchi hii
 
Achana na MATAGA hayo mkuu hayana uwezo wa kufikiri wala utu, yanajiona malaika siku zote
 
Kwamba ukiwa komandoo uachwe ufanye utakacho?
 
Unless Kuna mission wanacheza, but if it were me, ningewakung'uta mingumi na mitama watesi wangu then nafia in Action!
 
Inasikitisha
 
Hii kesi inalipa aibu kubwa sana Taifa letu!
Inawaumbua wakubwa mno mno na taasisi zake!
Raisi angewatafuta na kuwachukulia hatua kali waliomlisha matango pori kuhusu kesi hii nae akaidanganya dunia!
Wote walishinikiza kuipeleka hii kesi mahakamani wachukuliwe hatua na fedha za walipakodi zirudi kwa kukatwa au kutaifishwa kwa mali zao.
 
Mkuu!Ina maana makomandoo ni kama laana kwa taifa?Hawapendwi,hawathaminiwi ?au wanaonekanaje kwani???AU UKOMANDO HAUNA MAANA TENA HAPA NCHINI!!!
 
JWTZ hawana sera ya kuwalinda watu ambao wanakuwa trained kwa kiwango cha Ukomandoo, hawa jamaa walitelekezwa na wamepitia wakati mgumu mno.
Nchini zingine huwatumia kwa kazi maalum pindi wakiwa wamestaafu mfano china America Uk German France kenya Uganda huwatumia kwenda kufundisha nchi zingine kisha Serikali kuingiza Pato na wengine husalia kuwa washauri wa kijeshi hupewa vitengo maalum, lakini kwa Tanzania ni ajabu wanastaafu wanabakia kuhangaika mitaani na wakipata ajila binafsi DC Sabaya kwa kutaka kumfurahisha magufuli anawabambikia kesi ambayo imelichafua kulitia aibu jeshi la Polisiccm.
 
Mkuu!Ina maana makomandoo ni kama laana kwa taifa?Hawapendwi,hawathaminiwi ?au wanaonekanaje kwani???AU UKOMANDO HAUNA MAANA TENA HAPA NCHINI!!!
Dc Sabaya alitaka sifa kwa kuwabambikia kesi ya ugaidi kumbe hakujua ataidhalilisha Taaluma ya ukomandoo
 
JWTZ ni lazima waje na kauli, hili hatuwezi kunyamaza kabisa - kesi ya Mh. Mbowe imefurumua mengi...

Na naomba mawakili wajipange kuwafungulia mashitaka hawa jamaa Jummanne, Mahita, Goodluck, Azizi, na baba yao Kingai... hawa watano wametumia madaraka yao vibaya, ushahidi tunao umeshiba.

WASHITAKIWE MARA MOJA.
 
Pengine mungu ana makusudi yake, mungu kafungua mabaya yaliyokuwa yamejificha kwenye utawala wa magufuli na hii itakuwa fundisho kwa utawala huu na Tawala zijazo
 
Mahita na kingai yafaa kufikishwa The Hague kabsa kwa unyama waliotenda kuwapiga kuwatesa watu waseme Ugaidi hewa, kulazimisha mtu akubali ugaidi ambao haukuwepo ni kitendo kibaya sana, mahita na kingai waseme walipo Urio na mwenzake ambaye inasemekana alikufa kwa Mateso yao ya kumfurahisha DC Sabaya.
 
Mahakama ya kimataifa vyama tasisi za haki za binadamu wawamulike Mahita na kingai na pia wasomewe Albadiri kila kona Duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…