Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Nafikiri tungejikita zaidi kwenye kutendewa haki na vyombo vyetu.

Hao makomandoo kuteswa ni jambo moja. Lakini mbaya zaidi ni kuteswa na chombo tunachokiamini na kupewa dhamana ya usalama wa raia.

Ikiwa wanautendea hivi mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu?

Hapa tungeweka pembeni tofauti zetu zote na kupiga kelele kuangaziwa kwa namna hiki chombo kinavyotekeleza majukumu yake, leo kwa makomandoo, nani anajua kesho watamwangukia nani? Anaweza kuwa ndugu yako au wewe mwenyewe.
Kitendo cha kwenda kumpiga kumtesa mtu wakati ukijua kuwa hana kosa siyo gaidi ndicho kimelitia Doa jeshi la Polisiccm
 
Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa kama haina "database" ya watumishi wake wa vyombo vya usalama basi ianze sasa mara moja bila kujali watumishi hao wametoka kwenye vyombo hivyo kwa sababu gani kama kustaafu, kufukuzwa, utoro, kuacha wenyewe, ulevi, kuugua, n.k.. Kukiwepo na "databse" (siku hizi teknolojia imerahisisha kila kitu) itakuwa rahisi sana kwa serikali kujua nani yupo wapi anafanya nini na ni namna gani
Jeshini yapo matatizo mengi, Sheria za jwtz ni zilezile za mkononi hazijafanyiwa marekebisho, hakuna vifungu vya kuwabana wakuu wa kijeshi kuwafukuza Asikari kiholela pasipo kuwapa nafasi ya kutosha kujitetea, wapo wanasheria wa jwtz lakini ni wachache sana ni nadra kuwatetea Asikari masikini ambao hawana ndugu mkubwa au network jeshini,

Asikari wengi hufukuzwa jeshini kiholela pasipo kujali gharama zilizotumika kumfundisha kumpa ujuzi wa kijeshi, tena wengine hufukuzwa hata kwa wivu wa Mapenzi kisa pengine kuna mwanamke yupo na boss lakini anampenda Asikari wa chini ndipo boss hutengeneza mitego na mazingira ya kumfuza kazi ama kumhamishia vikosi vya mbali zaidi na wengi ndipo huacha wenyewe kwa Hofu, jwtz yafaa itengeneze Sheria mpya nzuri iwashirikishe Asikari wote wapate kutoa maoni kwa uwazi mkubwa.
 
Acha ufala kwani yeye hana damu kwani yeye siyo binadamu kupigwa kwa uonevu kusingiziwa uongo ulitaka anyamaze? Si uliona yule mwenzao alivumila maumivu akaishia kufariki kwa mateso, kulazimisha mtu akubali ugaidi hewa ndicho kilimliza zaidi.
Bongo ina makomando mdebwedo.
 
Sasa kama jeshi linaitisha press kulalamikia matapeli unategemea nini? Kwa sasa jeshi linawajibika kwa ccm zaidi kuliko nchi. Kunafanyika chaguzi za aibu ndani ya nchi, jeshi liko kimya na kuona sawa ili mradi ccm wanatangazwa washindi. Ukakamavu wa jeshi unaonekana zaidi wanapotishia raia wasio na silaha wala mafunzo ya kikakamavu. Tuombe tu vita isitokee maana itakuwa aibu. Nilijiuliza Kagame alijiamini nini kumtishia JK wakati ule, kumbe anajua siri ya urembo. Isije ikawa udhaifu uliopo kwenye taasisi nyingine za umma, upo na jeshini pia.
Aiseeee !!
 
Ukomandoo, kumbe ni jambo la hovyo såna, unateseka kujifunza kufanya mission ngumu halafu unakuja kutupwa kama takataka
 
So sad aisee, yaani kama waliyosema ni kweli basi kuna shida somewhere kwenye mifumo yetu au sheria zetu.

Testimony ya criminal defendant kwenye kesi yake mwenyewe sio ya kulalia mlango wazi. Vinginevyo, hakuna criminal defendant anayeweza kupatikana na hatia!
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)

Don’t take anything at face value. These are criminal defendants. Testimonies za criminal defendants kwenye kesi zao wenyewe katu sio za kulalia mlango wazi. Vinginevyo, hakuna criminal defendant anayeweza kupatikana na hatia!
 
Mahita na kingai yafaa kufikishwa The Hague kabsa kwa unyama waliotenda kuwapiga kuwatesa watu waseme Ugaidi hewa, kulazimisha mtu akubali ugaidi ambao haukuwepo ni kitendo kibaya sana, mahita na kingai waseme walipo Urio na mwenzake ambaye inasemekana alikufa kwa Mateso yao ya kumfurahisha DC Sabaya.

Hivi mbona CDO Lt urio hakutokea kutoa ushahidi ?
 
Niliwaahi andika humu, ila shida ni kutafutana.


Mimi Kaka yangu ( mtoto wa mama mkubwa)

Wakiwa pale kambi ya ukomandoo Morogoro...

Posho zao wakawa hawapewi, wakaamua kuja Dar makao makuu JWTZ kulalamikia.


maajabu, wakapewa Kesi za Uhaini, uhujum, uasi, uporaji wa Mali za Raia.


Walikua vijana 60 wa Mafunzo ya ukomando

30 wakasamehewa ...30 Wakafungwa jela mwaka 2015 akiwemo Kaka yangu huyo.


Waziri Mkuu anajua, Mwinyi anajua, Mwanasheria Mkuu wa wakat huo anajua,Mkuu wa Majeshi alopita anajua ..maana suala lao lilijitokeza 2013 .


WAKAFUKUZWA KAZI BILA KUPEWA BARUA YA KUACHISHWA KAZI, BILA KUPEWA MAFAO YAO, IKUMBUKE TOKA HUO MWAKA 2013 MPAKA 2015 ,MISHAHARA YAO ILISIMAMISHWA.


Walikua kuachiwa mwaka 2017 kwa msamaha

mpaka naongea hii Leo, Hawa vijana wamejitahidi kutafuta haki zao sanaaa ,wametumia wanasheria wapiiii..suala lao linaminywa chini chini.






KWA sasa wamebaki vijana 29. ..baada ya mmoja maisha kumchanganya, akaungana kwenye ujambazi,... Alipigwa risasi.
Hii nchi inanuka dhuluma na laana za watu.
Kamwe haitaendelea. Nchi za wetu hawa huthaminiwa na kulindwa vema.
 
Inaelekea JWTZ inathamini wanajeshi wakiwa na afya njema lakini pindi wakiumia au kupata maradhi wakiwa kazini inawatelekeza!

Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuangalia upya jambo hili kwani halina afya kwa ustawi wa jeshi letu.
Jeshi letu la ovyo hasa kwa askari wasio na vyeo. Ni takataka
 
Back
Top Bottom