07 January 2022
Mkuu wa Majeshi wa Kwanza JENERALI SARAKIKYA, Asimulia Alivyoshiriki Kuliunda Jeshi
Katika interview hii maalum mhitimu wa chuo tajwa kabisa cha kijeshi duniani cha Sandhurst huko Uingereza, Jenerali mstaafu Mirisho Sam Hagai Sarakikya anaelezea alivyojiunga jeshi mwaka 1959 ambapo aliwakuta David Musuguri na Mwita Waitara wakiwa na vyeo vya juu vya nyota ya kitambaa siyo ya chuma mabegani ....pia undani wa maasi ya mwaka 1964 na utumishi wake jeshi hadi anastaafu jeshi mwaka 2002.
Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya kwa mstuko mkuu akiwa afisa kijana umri miaka 30 tu mwaka 1964 aliteuliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Mkuu wa Majeshi.
Hii ni kufuatia maasi ya jeshi la KRA mwaka 1964 na serikali kuamua kuwatimua waasi wote kutoka jeshini kutokana na kukosa uzalendo, hivyo kuanza upya kuunda jeshi litakalokuwa na uzalendo kwa Taifa.
Hivyo akapandishwa cheo kuwa Brigedia kwa wakati huo Brig. Mirisho Sam Hagai Sarakakya kwa kuwaongoza maafisa wenzake na kwa bahati nzuri hakukuwa na afisa yoyote aliyeshiriki katika maasi hayo yaliyokuja kuzimwa na Jeshi la Uingereza lililoombwa kuzima maasi ya askari ... walishughulika kuunda upya jeshi lililo na mtizamo wa kulitumikia Taifa na wananchi hivyo kuwa JWTZ .
Hivyo chini ya uongozi wake Jenerali Sarakikya walipewa jukumu la kupatikana Jeshi la nchi kavu infantry, jeshi la majini navy, jeshi la anga, na kufuatiwa na kuanzisha pia shule za wapiganaji shule za maofisa, staff college, vyuo vya maofisa.
Jenerali Sam Hagai Sarakikya sasa ni mstaafu kwa miaka inayozidi 10 anajisikia fahari kuazimishwa kwa miaka 60 ya uhuru pia kuundwa upya jeshi la kizalendo hadi kuwa la kisasa na operesheni mbalimbali JWTZ ilizoshiriki Seychelles, Comoros, Mozambique, South Sudan, DR Congo n.k
Source : Ulinzi Channel
Habari za ziada :
TPDF / JWTZ December 2021
Video courtesy of Wasafi Media
Kamandi ya Jeshi la anga la Tanzania
Video courtesy of the Boss tv
Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania NAVY
Rear Admiral Michael Mumanga mkuu wa kamandi ya jeshi la wanamaji - Navy
Video courtesy of Ulinzi Channel