Jenerali Mirisho Sarakikya: Niliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi nikiwa na umri wa miaka 30

Jenerali Mirisho Sarakikya: Niliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi nikiwa na umri wa miaka 30

Siyo Sarakikya. Ni Sayole aliyekuwa mkuu wa chuo Monduli Tanzania Military Academy.


Kuna uzi ulitupiwa hapa JamiiForums kuhusu aliyepata kuwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli (TMA), na baadaye kuwa chief of Staff TPDF / JWTZ Lt. Gen Gideon Sayore na Jakaya Kikwete :

 
MAFANIKIO TPDF SHEREHE ZA MIAKA 60 YA UHURU


Major General Shabani B. Mani mkuu wa kamandi ya jeshi la anga anasimulia muendelezo wa TPDF / JWTZ kuzidi kujipanga kisasa tangu Tanzania ilipopata uhuru.
Source : Ulinzi Channel
 
Ila kama unafahamika na wakubwa hukosi kitengo kizuri....

..zamani kila graduate wa udsm alikuwa anapata kazi serikalini au ktk mashirika ya umma.

..kulikuwa hakuna haja ya kujuana na mkubwa yeyote, wahitimu watarajiwa walikuwa wanajaza fomu kueleza wanataka kufanya kazi wapi na wanapangiwa kulingana na walichochagua.

..wakati mwingine serikali ilikuwa inapeleka wanafunzi nje ya nchi kusoma ili watakaporudi waajiriwe ktk taasisi fulani.

..kwa mfano, kabla kiwanda cha karatasi Mufindi hakijaanza kazi, serikali ilipeleka wanafunzi India, kusomea taaluma mbalimbali zilizokuwa zinahitajika kiwandani.
 
Zamani wasomi walikuwa wachache sana au vijana waliaminika?

Mfano Mwl Nyerere alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika akiwa 'under 40'.....tena aliongoza harakati za Uhuru akiwa kwenye early 30's tu.

Mstaafu Sarakikya alikuwa mkuu wa majeshi akiwa na miaka 30 tu.

Mstaafu Dr Salim Ahmed Salim alikuwa balozi wa Tz huko Misri akiwa kwenye early 20's.

Vijana wa zamani walikuwa na kipi tofauti na sisi mpaka kupata madaraka makubwa wakiwa na umri mdogo?....sisi wa Leo tunakwama wapi? ....
Huo umri kwa miaka ya Sasa Ni special kwa ajili ya kula tunda kimasihara.
 
HUU uzee ni tabu, kumbukumbu zangu zinanisuta kuwa aliyeshitakiwa na Jakaya ni Sayore( aliyekuwa mkuu wa chuo cha kijeshi cha Monduli) na "SI" sarakikya. Sarakikya hajawahi kuwa boss wa Jakaya. iLA inaonesha mpeleka mashitaka alikuwa na lake jambo
Pamoja na kusahihisha, pia umechapia huo ndiyo mwisho wa uanajeshi waJakaya. KLama ipo hiyo barua inawezekana, lakini Kikwete aliendelea kuwa jeshini na kupanda hadi cheo kuwa kanali. Sijui kama unajuwa Kikwete alikuwa usalama wa taifa miaka yote mpaka alipokuwa raisi, ila yeye hakukaa au kuifanyia hiyo kazi katika ofisi na majengo ya usalama wa taifa. Siku zote kazi zake zilizokuwa zinajulikana ni za kiraia kumbe hizo zilikuwa geresha tu.
 
07 January 2022

Mkuu wa Majeshi wa Kwanza JENERALI SARAKIKYA, Asimulia Alivyoshiriki Kuliunda Jeshi



Katika interview hii maalum mhitimu wa chuo tajwa kabisa cha kijeshi duniani cha Sandhurst huko Uingereza, Jenerali mstaafu Mirisho Sam Hagai Sarakikya anaelezea alivyojiunga jeshi mwaka 1959 ambapo aliwakuta David Musuguri na Mwita Waitara wakiwa na vyeo vya juu vya nyota ya kitambaa siyo ya chuma mabegani ....pia undani wa maasi ya mwaka 1964 na utumishi wake jeshi hadi anastaafu jeshi mwaka 2002.

Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya kwa mstuko mkuu akiwa afisa kijana umri miaka 30 tu mwaka 1964 aliteuliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Mkuu wa Majeshi.

Hii ni kufuatia maasi ya jeshi la KRA mwaka 1964 na serikali kuamua kuwatimua waasi wote kutoka jeshini kutokana na kukosa uzalendo, hivyo kuanza upya kuunda jeshi litakalokuwa na uzalendo kwa Taifa.

Hivyo akapandishwa cheo kuwa Brigedia kwa wakati huo Brig. Mirisho Sam Hagai Sarakakya kwa kuwaongoza maafisa wenzake na kwa bahati nzuri hakukuwa na afisa yoyote aliyeshiriki katika maasi hayo yaliyokuja kuzimwa na Jeshi la Uingereza lililoombwa kuzima maasi ya askari ... walishughulika kuunda upya jeshi lililo na mtizamo wa kulitumikia Taifa na wananchi hivyo kuwa JWTZ .

Hivyo chini ya uongozi wake Jenerali Sarakikya walipewa jukumu la kupatikana Jeshi la nchi kavu infantry, jeshi la majini navy, jeshi la anga, na kufuatiwa na kuanzisha pia shule za wapiganaji shule za maofisa, staff college, vyuo vya maofisa.

Jenerali Sam Hagai Sarakikya sasa ni mstaafu kwa miaka inayozidi 10 anajisikia fahari kuazimishwa kwa miaka 60 ya uhuru pia kuundwa upya jeshi la kizalendo hadi kuwa la kisasa na operesheni mbalimbali JWTZ ilizoshiriki Seychelles, Comoros, Mozambique, South Sudan, DR Congo n.k
Source : Ulinzi Channel


Habari za ziada :

TPDF / JWTZ December 2021



Video courtesy of Wasafi Media


Kamandi ya Jeshi la anga la Tanzania


Video courtesy of the Boss tv

Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania NAVY


Rear Admiral Michael Mumanga mkuu wa kamandi ya jeshi la wanamaji - Navy
Video courtesy of Ulinzi Channel
Gen. Mwita Waitara hakuwahi kuwa Mkubwa kwa cheo kwa Gen. Sarakikya, nadhani umechanganya majina.
 
Gen. Mwita Waitara hakuwahi kuwa Mkubwa kwa cheo kwa Gen. Sarakikya, nadhani umechanganya majina.

..Mirisho Sarakikya aliondoka jeshini mwaka 1974 akiwa Meja Jenerali [ 2 star general ]

..alibaki na rank hiyo mpaka pale Rais Mkapa alipompandisha kuwa Jenerali [ 4 star general ].

..sasa kati ya 1974 mpaka Sarakikya anapandishwa ngazi, Twalipo, Musuguri, Kiaro, walitangulia kuwa Majenerali [ 4 star ].

..Kwa hiyo mchangiaji akisema Twalipo, Musuguri, au Kiaro, walikuja kuwa mabosi kwa Mirisho Sarakikya hawatakuwa wamekosea.
 
Zamani wasomi walikuwa wachache sana au vijana waliaminika?

Mfano Mwl Nyerere alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika akiwa 'under 40'.....tena aliongoza harakati za Uhuru akiwa kwenye early 30's tu.

Mstaafu Sarakikya alikuwa mkuu wa majeshi akiwa na miaka 30 tu.

Mstaafu Dr Salim Ahmed Salim alikuwa balozi wa Tz huko Misri akiwa kwenye early 20's.

Vijana wa zamani walikuwa na kipi tofauti na sisi mpaka kupata madaraka makubwa wakiwa na umri mdogo?....sisi wa Leo tunakwama wapi? ....
Hakuna facebook, instagram, tiktok na picha za ngono. Zamani ukiwa na kiu ya kusoma unakuwa msomi kweli. Sasa hivi distractions nyingi, ukitoka nje tu unakutana na wadada wamevaa nusu uchi
 
Back
Top Bottom