Jenerali Moses Ali, Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uganda, ameanza rasmi kampeni zake za kugombea tena kiti cha ubunge cha East Moyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2026.
Akiwa na umri wa miaka 86, Jenerali Moses Ali amesifiwa na wananchi wa Uganda kwa mchango wake mkubwa katika utumishi wa umma pamoja na juhudi zake thabiti katika kupambana na rushwa.
Kampeni zake zimezinduliwa kwa nguvu, huku akisisitiza dhamira yake ya kuendeleza maendeleo katika eneo la East Moyo na kuchochea mageuzi ya kiutawala na kijamii.
Jenerali Moses Ali ni mmoja wa viongozi waandamizi nchini Uganda wenye historia ndefu ya kisiasa na kijeshi, na anatazamiwa kuwa mmoja wa wagombea wakuu katika kinyang’anyiro hicho. NB Umri is Just a Number 😃