Jenerali Muhoozi aponda Ujerumani kumtuma balozi mfupi Uganda, atuhumu kuunga mkono Upinzani

Jenerali Muhoozi aponda Ujerumani kumtuma balozi mfupi Uganda, atuhumu kuunga mkono Upinzani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Jeshi la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameeleza kutoridhishwa kwake na namna Ujerumani ambayo inajulikana kuwa na watu warefu na kutuma Balozi mfupi nchini Uganda.

1748325178889.png
Balozi wa Ujerumani nchini Uganda, Mathias Schauer, amekuwa akitofautiana na mamlaka ya nchi hiyo kwa muda sasa kwa sababu anatuhumiwa kuunga mkono makundi ya upinzani dhidi ya utawala wa Rais Yoweri Museveni.

Msemaji wa Jeshi la Uganda, Kanali Chris Magezi, tarehe 23 Mei 2025 alifichua kwamba wakati Uganda inajiandaa kwa uchaguzi wa Rais wa 2026, kutakuwa na kuibuka kwa makundi yenye silaha yenye lengo la kuvuruga usalama wa viwanja vya umma na kutatiza shughuli.

Kanali Magezi alieleza kuwa baadhi ya waliokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na wanachama wa chama cha NUP kinachoongozwa na mwanasiasa Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine.

Askari huyo alieleza kuwa alipokuwa akiwafuatilia wafadhili wa vikundi hivyo vinavyopinga NRM, ilibainika kuwa kuna baadhi ya balozi za nchi za Umoja wa Ulaya (EU) mjini Kampala.
 
Back
Top Bottom