Jenerali on monday: Rasimu ya katiba

UFUNUO WA TANZANIA

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
471
Reaction score
166
Mkinga anachambua rasimu. Rasimu hii inalenga kuvunja muungano. Imechukua mambo kwenye katiba ya Zanzinzibar na kuyahamishia kwenye katiba ya muungano. Mchambuzi anaunga mkono uchambuzi wa Prof Shivji kwamba katiba hii imejikita kwenye Compromise ambayo ni Tu-agree to Dis-agree. Rasimu ya katiba imelenga sana mambo ambayo Zanzibar walikuwa wanayahitaji na pia yale ambayo katiba yao imeyaeleza. Vyeti vinauzwa na Rita kama Njugu. Serikali imejikita kuajiri polisi ambao ni zaidi ya 50,000 wakati uhamiaji ni 2400 tu. Maswala mengi ambayo yalipaswa kuwa ya muungano wameyapeleka kuwa ya serikali washirika. Rushwa imekithiri na ufisadi uongozi unaweza kununuliwa kwa uongozi wa ngazi yoyote. Kwa wasomi waliopo ni makini lakini kazi wanayoifanya si ya kiwango cha usomi wao. Hii inatokana na mvutano mkali uliopo ndani ya TUme. Hitimisho: Kweli kwa rasimu hii ya katiba tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kama kweli sisi WaTZ tuna dhamira ya kuendelea kuwa na Muungano. Lakini Kupanga ni kuchagua. Hata bila muungano kila nchi yaani Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwepo. Ila Zanzibar wajihadhari kwa kuwa Wapemba na Waunguja wanaweza kujitenga tena. Kwa rasimu tuliyonayo sasa Muungano unaenda kuvunjika . Uharaka haraka wa kupata katiba unatuponza. Ilipasa kwanza iitishwe kura ya maoni kama tunahitaji muungano au la na kama ndio uwe wa seriklai ngapi kabla ya kuanza kuandaa rasimu ya katiba. Mwisho
 
jamaa anaongea kwa jaziba nimeshindwa kumuelewa nimeamia eatv.niangalie miziki.
 
mkinga ni ccm ila amesema swala la katiba haikuwa ajenda ya ccm bali ya chadema
 
Katika nchi ambayo usalama wa Taifa umebaki kulinda CHADEMA walishinde uchaguzi....ndiyo maana vyeti vya kuzaliwa vinanunuliwa kama njugu...MKINGA analeta raha jamani....Angalieni channel 10
 
Mkinga anaujasiri wa kuzungumza mambo ambayo wengi hatuwezi kufanya hvyo.
kwa mtizamo wangu,leo Mkinga anazungumza kwa jazba,halafu anazungumza mambo mengi sana badala ya kujikita kwenye hoja moja.
Ndio maana hata Jenerali kamwambia awe logical na si kuzungumza kwa hisia.
 
Kuna kipindi channel ten: jenerali on monday; huyu jamaa (mgeni) anaongea kwa jazba sana sometimes anaenda nje ya topic( wanadiscus rasimu ya katiba) anamwaga mambo mbali2 hadharani! Yangu macho unaweza na wewe kuchek...
 
mkinga ana simu nne zikipigwa zote kwa onetime anapokeaje?
 

Nadhan ni jazba inatokana na uozo wa mamlaka kuto wajibika. Tanzania yangu inaangamia
 
Mwacheni atoke povu,zanzibr itang'oka kwenye makucha ya mkoloni mweusi akipenda asipende.
 
muungano uvunjike tu akina amijei watulipe umeme wetu
 
Kuna kipindi channel ten: jenerali on monday; huyu jamaa (mgeni) anaongea kwa jazba sana sometimes anaenda nje ya topic( wanadiscus rasimu ya katiba) anamwaga mambo mbali2 hadharani! Yangu macho unaweza na wewe kuchek...

Ooooh!jazba kwani ulitaka awe anackekacheka?jambo kubwa kama hilo lazima atokwe povu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…