UFUNUO WA TANZANIA
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 471
- 166
Mkinga anachambua rasimu. Rasimu hii inalenga kuvunja muungano. Imechukua mambo kwenye katiba ya Zanzinzibar na kuyahamishia kwenye katiba ya muungano. Mchambuzi anaunga mkono uchambuzi wa Prof Shivji kwamba katiba hii imejikita kwenye Compromise ambayo ni Tu-agree to Dis-agree. Rasimu ya katiba imelenga sana mambo ambayo Zanzibar walikuwa wanayahitaji na pia yale ambayo katiba yao imeyaeleza. Vyeti vinauzwa na Rita kama Njugu. Serikali imejikita kuajiri polisi ambao ni zaidi ya 50,000 wakati uhamiaji ni 2400 tu. Maswala mengi ambayo yalipaswa kuwa ya muungano wameyapeleka kuwa ya serikali washirika. Rushwa imekithiri na ufisadi uongozi unaweza kununuliwa kwa uongozi wa ngazi yoyote. Kwa wasomi waliopo ni makini lakini kazi wanayoifanya si ya kiwango cha usomi wao. Hii inatokana na mvutano mkali uliopo ndani ya TUme. Hitimisho: Kweli kwa rasimu hii ya katiba tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kama kweli sisi WaTZ tuna dhamira ya kuendelea kuwa na Muungano. Lakini Kupanga ni kuchagua. Hata bila muungano kila nchi yaani Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwepo. Ila Zanzibar wajihadhari kwa kuwa Wapemba na Waunguja wanaweza kujitenga tena. Kwa rasimu tuliyonayo sasa Muungano unaenda kuvunjika . Uharaka haraka wa kupata katiba unatuponza. Ilipasa kwanza iitishwe kura ya maoni kama tunahitaji muungano au la na kama ndio uwe wa seriklai ngapi kabla ya kuanza kuandaa rasimu ya katiba. Mwisho