Jenerali Ulimwengu adai wamiliki wa vituo vya mafuta wanahujumu miradi matumizi ya gesi kwenye magari

Jenerali Ulimwengu adai wamiliki wa vituo vya mafuta wanahujumu miradi matumizi ya gesi kwenye magari

Jenerali Ulimwengu amefanya tafakuri kuhusu nishati ya mafuta na gesi katika kufanikisha usafiri nchini. Kwa tathmini yake amebaini wamiliki wa vituo vya mafuta wapo mstari wa mbele kukwamisha matumizi ya gesi nchni.

Gesi ni rahisi sana lakini pamoja na urahisi wa bei idadi ya vituo vya mafuta vinavyojengwa ni vingi jambo linaloashiria kwamba miamba imeshika soko na mifumo ya maamuzi ya nchi.

Hoja ya Jenerali inaungwa mkono na ya Mbunge wa Geita maarufu kama Msukuma. Alidai bungeni siku chache zilizopita kwamba issue ya gesi imekamatwa na serikali na hawataki kutoka vibali kwa sekta binafsi.

Wakati haya yanasema msimamizi wa sekta hii Mhe. Biteko bado akajitokeza adharani kutoa maoni ya serikali ikiwa ni pamoja na kuzipinga au kuziunga mkono tuhuma hizi.

Kwanini serikali isisitishe kwa muda ujenzi wa vituo vipya vya mafuta na kuwaelekeza wawekezaji wawekeze kwenye vituo vya gesi?
Kwani ntu akitaka kujenga kituo cha gesi mwenye kituo cha mafuta anamzuiaje? Kibali kinatolewa na serikali iweje walaumiwe wengine? Watanganyika wanapenda kulia lia huku hawachukui hatua stahiki.

Suala la biashara linategemea nguvu ya soko ( demand & supply) na sera za kodi nk.

Kwanza baadhi yetu hatuna mpango wa kugeuza magari yetu yawe ya gesi yaani mtu anunue benz halafu atafute nishati ya bei rahisi. Kama sina hela ya mafuta napaki gari kwani lazima niendeshe? Halafu hiyo gesi ni kampeni tu lakini factors nyingine nyingi zikitiliwa maanani mtu anaweza kuanua asibadilishe gari lake liwe la gesi.

SI busara kufuata vitu kwa upepo inatakiwa mtu afanye analysis vizuri kabla ya kuamua jambo.
 
Ni kweli kama ulivyoshauri na magari yakuagiza yawevyale yanayotukia Gas has ya serikali na mashirika ya umma
Vituo vya gesi wapi Nchi Nzima Hadi utake serikali iagize Magari yanayotumia gesi tu? Kazi ya kufungua vituo vya gesi ni kazi ya sekta binafsi havipo .Sasa havipo mikoani hayo Magari ya gesi yakiletwa yatajaza wapi? Huko mikoani?
 
Kwani ntu akitaka kujenga kituo cha gesi mwenye kituo cha mafuta anamzuiaje? Kibali kinatolewa na serikali iweje walaumiwe wengine? Watanganyika wanapenda kulia lia huku hawachukui hatua stahiki.

Suala la biashara linategemea nguvu ya soko ( demand & supply) na sera za kodi nk.

Kwanza baadhi yetu hatuna mpango wa kugeuza magari yetu yawe ya gesi yaani mtu anunue benz halafu atafute nishati ya bei rahisi. Kama sina hela ya mafuta napaki gari kwani lazima niendeshe? Halafu hiyo gesi ni kampeni tu lakini factors nyingine nyingi zikitiliwa maanani mtu anaweza kuanua asibadilishe gari lake liwe la gesi.

SI busara kufuata vitu kwa upepo inatakiwa mtu afanye analysis vizuri kabla ya kuamua jambo.
Uko sahihi watu wengine wanachangia kijinga kama vile serikali inazuia watu binafsi kufungua vituo vya gesi za Magari. Dar vipo lakini waliochangamka kufunga ni taxi za Uber tu watu binafsi wamegoma kufunga na Elimu wanayo kuwa gesi Rahisi .Hawataki kufunga pamoja na uwepo wa vituo vya kuwaza hata Generali ulimwengu mwenyewe akitaka hata kesho apeleke gari yake watamungia mfumo wa gesi na hata akitaka kufungua kituo Cha gesi ya Mafuta leseni ndani ya Siku saba atapata kama eneo lake lilishakuwa cleared na NEMC kuwa hakuna athari za mazingira
 
Vituo vya gesi wapi Nchi Nzima Hadi utake serikali iagize Magari yanayotumia gesi tu? Kazi ya kufungua vituo vya gesi ni kazi ya sekta binafsi havipo .Sasa havipo mikoani hayo Magari ya gesi yakiletwa yatajaza wapi? Huko mikoani?
Kwani sasa hivi hapa Dar wanajazia wapi??
 
Kwa tajiri kwenda Kwenye ufalme wa mbinguni ni heri ya ngamia atapita katika tundu la sindano !!
 
Nilivyoangalia CLIP YA DR. SHUKURU KAWAMBWA akipambana na UHARIBIFU WA MAZINGIRA KULE BAGAMOYO mpaka akadhalilishwa GHAFLA kichwani likaja jina la JENELALI ULIMWENGU na MACHIMBO YAKE YA MCHANGA YANAVYOHARIBU MIUNDOMBINU.........

NEMC
WNAMAZINGIRA
WIZARA YA MADINI
MMETEMBELEA MACHIMBO YA MCHANGA YA ULIMWENGU?????????
Yapo wapi tutume vijana kwa wazee
 

VITUO 9 VYA KUJAZA GESI ASILIA KWENYE MAGARI KUJENGWA​

Mkurugenzi wa Biashara ya Mafuta na Gesi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. Wellington Hudson amesema jumla ya vituo tisa (9) vya kujaza gesi asilia kwenye magari vinatarajia kujegwa na kukamilika katika kipindi cha miezi 24.
Dkt. Hudson ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akifanya mkutano na Waandishi wa Habari kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya foleni iliyopo kwa sasa katika kituo cha kujaza gesi asilia kwenye magari cha Ubungo kutokana na hitilafu iliyotokea katika gari la kubeba gesi (CNG tanker) kupeleka kituo cha Anric TAZARA.
Dkt. Hudson amesema kuwa pamoja na kuharibika kwa lori hilo, foleni iliyopo katika kituo cha Ubungo kinadhihirisha mwitikio mkubwa wa wananchi wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari.
Wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuweka mifumo ya gesi asilia kwenye magari kiasi kwamba vituo vilivyopo vinaonekana kuzidiwa na ili kutatua changamoto hii zipo jitihada mbalimbali ambazo TPDC inaendelea kuzifanyia kazi ambapo hadi sasa kampuni zipatazo 20 zimepewa leseni ya kujenga vituo vipya katika maeneo mbalimbali alieleza Dkt. Hudson.
Aidha katika adhma hiyo ya kuongeza vituo nchini, TPDC itajenga Kituo Kikuu (Mother station) katika maeneo ya Mlimani City chenye uwezo wa kuhudumia magari sita kwa wakati mmoja pamoja na malori sita ya kubeba CNG kwaajili ya kupeleka katika vituo vidogovidogo.‘’Nipende kuwahakikishia kwamba, uwepo wa kituo hiki kikubwa utasaidia kuongeza kasi ya uwepo wa vituo vingi vidogovidogo vya kujaza gesi asilia kwenye magari.‘’
Akiendelea kutoa ufafanuzi Dkt. Hudson amesema kabla ya mwisho wa mwaka huu vituo viwili vya kujaza gesi vinatarajiwa kujengwa na kampuni ya TAQA DALBIT katika maeneo ya Uwanja wa Ndege na eneo la Sinza mkabala na Barabara ya Sam Nujoma ambapo vituo hivyo vitakuwa na karakana ya kuweka mfumo wa CNG.
Aidha, Dkt. Hudson amesema Kampuni ya TURKY Petroleum itajenga kituo eneo la Bagamoyo, Kampuni ya Anric itajenga eneo la Mkuranga, Kampuni ya BQ itajenga kituo eneo la Goba pia Kampuni ya DANGOTE itajenga eneo la Mkuranga. Uwepo wa Vituo hivi vyote vitasaidia kutatua changamoto za ujazaji wa gesi asilia kwenye magari.
 
Baadhi ya watanzania Kuna shida Kuna siku Hata yakikosekana maandazi mtaani watasingizia serikali

Vitu vya CNG ni fursa kubwa Kwa sekta binafsi ajabu hiyo fursa Kwa leseni zilizotolewa zimetolewa Kwa wafanyabiashara wa wenye asili ya kutoka Asia wachina,waarabu, Wahindi na mmoja Toka nje mnigeria Dangote

Waswahili Tena matajiri akina Msukuma wanalaumu serikali bungeni badala ya kuchukua hiyo fursa Msukuma ana mabasi zaidi ya mia moja si angefungua kituo Cha CNG kihudumie Hata mabasi yake

Dangote mnigeria ana malori mamia kaamua ajenge kituo Cha gesi .Sababu Kwa Sasa anajaza kituo Cha gesi Cha wachina

Mtaji mkubwa kuanzisha hivyo vituo ni kuanzia minimum bilioni moja na laki Tano Kwa kituo kidogo kisichohudumia magari mengi Kwa Wakati moja yaani kile chenye pump ya kujazia moja Sio nyingi kama vituo vya mafuta na gharama yaweza zidi hapo sababu ya gharama Mfano ya kununua eneo utakapoweka kituo.na ununuzi wa magari au kukodi ya kubeba CNG kuifikisha kituoni kwako
 
Back
Top Bottom