Hii mada nillikuwa sijaisoma lakini imekuwa kibwagizo kikubwa leo baada ya kumsikiliza Jenerali kwenye marudio ya Kongamano la Katiba. Vimeoana sana, haswa pale anavyoelezea jinsi alivyoshiriki kumsaidia Mkapa kupambana na Mrema wakati huo. Ikabidi mambo yapindishwe pindiswe kwa sababu ya Mrema asiweze kupumua.
Nimempenda kwa sababu moja tu, kuwa ni kati ya watu wachache sana waliowahi kufanya kazi na viongozi wa juu wa CCM walio na ujasiri wa kutoka hadharani na kuelezea mapungufu ya hiki chama kilicholewa madaraka. Tunaomba wajitokeze kwa wingi zaidi kwani hizi ndiyo dalili nzuri za kuzaliwa upya kwa Taifa letu.