Jenerali Ulimwengu: Kuna utamaduni kitu kikishatokea hutakiwi kuuliza maswali kimetokeaje au tunafanyeje

Jenerali Ulimwengu: Kuna utamaduni kitu kikishatokea hutakiwi kuuliza maswali kimetokeaje au tunafanyeje

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jenerali Ulimwengu, amekosoa utamaduni unaoendelea nchini wa kukwepa kuhoji au kutowajibika pindi matatizo yanapojitokeza katika michakato ya uchaguzi na mfumo wa kidemokrasia.

Akizungumza leo Septemba 15, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jenerali Ulimwengu amebainisha kuwa tabia hiyo imekuwa kama utamaduni wa "kufunika kombe" na kuendelea na mambo kama vile hakuna kilichotokea.

Amerejea jinsi alivyowahi kumuuliza aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hayati Jaji Damian Lubuva, kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 lakini hakupata majibu ya kueleweka.

Amelinganisha hali hiyo na nchi jirani ya Malawi, ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2014 alioshiriki kama mwangalizi, matokeo ya kila jimbo na mgombea wa kila chama yalichapishwa kikamilifu kwenye magazeti ndani ya siku tatu tu baada ya uchaguzi kuitishwa.

 
Back
Top Bottom