Jenerali Ulimwengu, amekosoa vikali mfumo wa kisiasa nchini na namna nchi ilivyoingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kufuata ushauri wa kina uliotolewa na Tume ya Jaji Nyalali mwaka 1992.
Akizungumza leo Septemba 7, 2026, katika mkutano uliowakutanisha wadau kujadili hali ya kisiasa nchini ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Jenerali Ulimwengu ameeleza kuwa maoni na mapendekezo mengi ya msingi ya Tume ya Nyalali yalikataliwa na badala yake kimbilio likawa ni kukumbatia jina la vyama vingi pekee.
Jenerali Ulimwengu amebainisha kuwa mfumo wa sasa umekosa misingi muhimu ya demokrasia kama vile fursa ya wagombea binafsi kuwania nafasi za uongozi kuanzia udiwani, ubunge hadi urais, hali inayobana uhuru wa wananchi kujieleza na kushiriki siasa nje ya mfumo wa vyama. Ameongeza kuwa hatua ya kuwataka raia wanaohoji mfumo huo kuunda vyama vyao binafsi ni sehemu ya mtazamo usio sahihi wa kujiona kuwa Watanzania ni wa kipekee tofauti na mataifa mengine.
Amesisitiza viongozi kuacha dhana ya kujiona wa kipekee (exceptionalism) na badala yake wakubali kuwa nchi inaongozwa na sheria za kiasili zinazotawala binadamu wote, na kwamba Taifa linapaswa kujitathmini kwa uwazi na kujenga mifumo inayojali uhuru wa kweli wa wananchi badala ya kujifariji na mifumo inayolinda wachache.