Jenerali Ulimwengu: UDSM imekuwa "Extended High School"

Jenerali Ulimwengu: UDSM imekuwa "Extended High School"

Udsm ikiwa kama secondary school, hizo vyuo vya kata kina udom na wenzake vitakuwa nini. Bado udsm ni Baba na mama wa vyuo vyote hapa nchini.
 
Professor Anangisye!
Alikuwepo eti prof. Bunsen Burner(sic) kila siku domo dhidi ya Chadema likafumbwa kwa kupewa uteuzi, na yule Mkumbo njaa kali naye Chadema, Chadema akapewa uteuzi, kimya.
Wakati wa Saba Saba nilitembelea banda la maonesho la UDSM halikuwa tofauti na la wanafunzi wa sekondari, hawakujipanga wala kujiandaa zaidi ya kuonesha vigari viwili vya kuungaunga vinatumia umeme, kwa wale wapenzi wa DIY (electronics) wanajua ni nini.
 
Kiufupi anasema UDSM ni kama Sekondari ya Kata, hakina hadhi ya Chuo Kikuu tena maana kimehama kutoka kwenye tafiti na mijadala na kuwa extended school 😂😂

Naunga mkono hoja ya ulimwengu.

haisaidii. vijana someni kwa bidii sana na msonge mbele. wakati wa akina generali umepita na kama kuna jambo walisahau kulifanya ndio wana kumbuka sasa, basi wajue tu mambo yanabadilika, waew waungwana tu. Haiwezekani kufanana na wao
 
Huyu Mzee ukisoma title ya habari zake unaweza kusema ni mwehu. Ila ukimsikiliza kwa makini utagundua ni namna gani yupo sahihi.

UDSM na baadhi ya vyuo vingine ila nakazia UDSM pale hamna kitu. Kwanza ogopa sana elimu inayotolewa kwa watu wengi kivile.. yaan lecturer anatoa madini mbele ya watu 300+ hapo hamna cha maana..

Ni kama shule za msingi darasa moja lina wanafunzi 100+ ukija ktk hizi Shule za mtaala wa Cambridge unakuta darasa moja wanafunzi 15 tu.. inamaana hata utilization ya resource ni nzuri na Mwalimu anaweza kufanya follow up kichwa kwa kichwa.. tofauti na hizi shule zenye kujaza majitu mengi darasani.
 
Karibia sehemu zote hata hizo Secondary and High Schools.

Mmesahau hata Jf ya sasa inasemwa iko unga sana tofauti na ya miaka ya 2012 kushuka nyuma ambapo Jf ilikuwa na mijada ya motomoto ,positive comments kwenye nyuzi nk.

Kadri muda unavyozidi kwenda kizazi kinabadilika..
 
Wanakuambia huko juu ni mserereko tu, degree unaipata unaiona ikija waziwazi labda uikatae mwenyewe. Huku chini ndio kuna elimu unaisotea kwa jitihada kubwa na unaweza usifike juu ukaishia chini pamoja na kusoma kwa bidii kubwa
 
palikuwa pamechangamka mijadala mbalimbali ya critical thinkers, Ila leo profesa Sheria anasema hajui Zanzibar ni nchi ama sio nchi Mambo yanaenda Kasi sana.

Ndio maana chinua Achebe kwenye moja vitabu vyake anasema Kuna usaliti mkubwa wa wasomi kwa watu wa kawaida waliwasomesha kwa Kodi zao baada ya kupata elimu wamewageuka na kulinda tabaka tawala na kandamizi.
 
Tunasubiri majibu kutoka UDSM
Anakuwaje sahihi kutaka ya kale yaote yalivyofanyika kale yafanyike hivyo leo. Angesema ya kale yafanyike si kwa style ya kale ila ya kisasa angalau angekaribu na sahihi. Leo kuna electronics, computer science including artificial intelligence(AI) kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo accounting, finance, economics etc...anataka hao watalaam wawe wanajaa nkrumah kila mara kuendesha mijadala ya kudai uhuru, haki za binadamu, kubishana kisiasa/kiuana harakati?. No hakuna wanafunzi wala wanataaluma wa aina hii leo. Mijadala inayoendeshwa sasa iko kiutalaam zaidi, economics wanamijadala yao, accounting, finance, electronics/IT na wanalika watalaam wa maeneo hayo nje ndani si kila mtu na sometimes inafnyika virtual. Mijadala general mpaka Uronu na Jenerali anaalikwa haina nafasi kubwa tena. Nyau mijadala inafanyika across disciplines kila mara na publications ni nyingi na bora zaidi leo kuliko zamani ambapo hata plagiarism test haikuwepo. Ukiona kitu kimetoka leo ni original siyo kumbakumba tena. Ktk hilo wneo hajielewi huyu mzee yeye na supporters wake. Yaani yuko sawa na mwanaume anayeclaim kuelewa mp zaidi ya mwanamke mwenyewe kisa tu ameoa au aliwahi kuoa😀😀
 
Back
Top Bottom