Jeneza la ajabu lililogunduliwa Alexandria, Misri lafunguliwa

Baba wa Mapaka

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
1,827
Reaction score
1,655
Wiki tatu zilizopita, wanaakiolojia nchini Misri waligundua jeneza kubwa lililoundwa kwa mawe magumu ya matale (granite) ya rangi nyeusi katika mji wa Alexandria.

Jeneza hilo lilikuwa limekaa kwa zaidi ya miaka 2,000 bila kufunguliwa.

Uvumi ulianza kueneza upesi, kwamba huenda jeneza hilo lilikuwa na mabaki ya kiongozi maarufu wa Wagiriki, Alexander the Great (Alexander Mkuu), au pengine kitu cha laana kubwa.

Kwa mujibu wa wataalamu walipolifungua, jeneza hilo halikuwa na hata kimoja kati ya vitu hivyo viwili.

Badala yake, waligundua mifupa ya watu watatu na maji machafu sana ya rangi ya hudhurungi ambayo yalitoa uvundo usioweza kuvumiliwa, mkali ajabu.

Waziri wa Vitu vya Kale wa Misri alikuwa ameteua kamati ya wanaakiolojia wa kufungua jeneza hilo ambalo liligunduliwa katika eneo kulikokuwa kunafanyika ujenzi.

Makaburi yaliyo na 'ujumbe kutoka kuzimu' MisriMji wa kale sana wagunduliwa MisriKemikali inayounda sehemu ya ndani ya dunia

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha El-Watan cha Misri, awali walijaribu kuinua kifuniko cha jeneza hilo hadi sentimeta tano hivi juu (inchi 2), lakini uvundo wa ajabu uliwazuia kuendelea na kulazimika kuondoka eneo hilo.

Baadaye walilifungua, wakiwa wamejiandaa kwa vifaaa, wakisaidiwa na wahandisi kutoka kwa jeshi la Misri.

"Tuliipata mifupa ya watu watatu, na inaonekana ni kama walikuwa wa familia moja... Kwa bahati mbaya, miili hiyo haikuhifadhiwa katika hali nzuri na ni mifupa pekee iliyosalia," amesema Mostafa Waziri, katibu mkuu wa Baraza Kuu la Vitu vya Kale Misri.

Jeneza hilo lilipatikana na mifupa ya watu watatu, wanaoaminika kuwa maafisa wa jeshi wa kale

Akizungumzia wasiwasi uliokuwa umeenea kwenye vyombo vya habari kwamba kufunguliwa kwa jeneza hilo pengine kungesababisha laana kutoka kwa Mafirauni, Bw Waziri alisema: "Tumelifungua na, namshukuru Mungu, kwamba hakujawa na giza duniani.

"Nilikuwa wa kwanza kutazama ndani ya jeneza hilo ... na niko hapa, nimesimama mbele yenu... na niko salama."

Licha ya hayo, eneo lilikopatikana jeneza hilo watu wamehamishwa huku kukiwa na wasiwasi kwamba linaweza kutoa hewa yenye sumu, gazeti la serikali ya Misri la Al-Ahram limeripoti

chanzo cha habari hii BBC swahili
Jeneza la ajabu lililogunduliwa Misri lafunguliwa

_102617235_tomb.jpg
 
Kweli Egypt ni source of all civilization.......kuna mengi huko ambayo hata hayajavumbuliwa
 
View attachment 814696
Hili ni Jukwaa la jokes mkuu
 
Back
Top Bottom