Jenga gorofa moja kwa gharama nafuu

ha ha ha kila kitu kina umuhimu wake mkuu, ulimwengu wa sasa unataka ujenge kwenda 'vertical' na si 'horizontal'
 
Mbwembwe zote za umaarufu jf unaishi kwenye rava fooo endelea kudanga ufikie tulipo
Rava foo wapi niringe??? Naishi kwenye kiota....nawe ulidanga ndio ukafika huko? Basi nami ntafika ngoja nikomae kudanga
 
Rava foo wapi niringe??? Naishi kwenye kiota....nawe ulidanga ndio ukafika huko? Basi nami ntafika ngoja nikomae kudanga
Rava Foo ni nyumba za maskini Kama wewe umaarufu jf kumbe mshamba tuuu
 
Aisee,swali rahisi tu mkuu.Mpk Hilo ghorofa la Bei rahisi kukamilika litakua limetumia sh. Ngapi(just rough estimates).
Ukipiga mahesabu ya hivyo hutojenga mkuu; ni sawa na kujiuliza tangu uzaliwe mpaka hapo ulipofikia umetumia fedha kiasi gani?

Kawaida kwenye ujenzi hasa kwa sisi masikini, tunaanza na tulichonacho, mwisho wa siku matokeo unayaona. Cha muhimu sana, unatakiwa uwe na kiwanja, hiyo ndio 'Principle' au pakuanzia.
 
Kuna jamaa mmoja anaendelea na ujenzi wa ghorofa 3(la kibiashara) majuzi nimeona anashusha mifuko ya cement tani 40,nondo zinashushwa Kama vile anafungua kiwanda nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Kuna jamaa mmoja anaendelea na ujenzi wa ghorofa 3(la kibiashara) majuzi nimeona anashusha mifuko ya cement tani 40,nondo zinashushwa Kama vile anafungua kiwanda nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Ujenzi wa kuanzia ghorofa 2 nakuendelea inabidi ujipange sana; ndio maana watu wengi huishia ghorofa moja.
 
Teh teh nimeshindwa kujenga Hilo ghorofa kwa Sasa hivi,lkn hizi za kajamba Nani hunikosi.

Teh teh hakuna principal ya Mishahara wa laki 5 itakayojenga ghorofa,Maisha yako yote sahau hio mzee.

Kuna jamaa humu JF Ni daktari,alileta plani yake ya kujenga kagorofa ka kiaina tu,tena kwa kujibanana na kusimamia kweli kweli mpk hesabu zake za mwisho alikua ametumia karibu mil 60 na ujenzi ulikua unaendelea yaani bado kwa Sana tu,sasa Hawa watumishi wa chini mil 60 tu yenyewe kuifikisha sijui itakua Ni baada ya miaka mingapi .😁😁😁
 
🀣🀣🀣 nimecheka sana mkuu
 
Kuna mzee mmoja miaka hiihii alinunua jengo pale Morocco Road na kisha akaivunja.

Baadae baada ya ukimya nikaona ghorofa ile yabomolewa yote hadi chini, kisha ikaanza kujengwa ghorofa ingine matata sana.

Baada ya miezi kadhaa ghorofa ikasimama na ikakamilika na sasa amepangisha NGOs moja hivi.

Yule mzee yupo zake huko Madale ametulia anavuta tu mpunga waingia kwa akaunti.

Nikawa nimejifunza kitu kikubwa sana.

Je, amechukua mkopo benki?

Je, alidunduliza?

Au alifanya namna fulani hivi?
 
Kuna mzee mmoja miaka hiihii alinunua jengo pale Morocco Road na kisha akaivunja.

Baadae baada ya ukimya nikaona ghorofa ile yabomolewa yote hadi chini, kisha ikaanza kujengwa ghorofa ingine matata sana...
Inawezekana mafao,mikopo bank, na vyanzo vingine alivyonavyo; ila wengi huwa ni mikopo bank, kwa mfano wenye viwanda hukopa hata zaidi ya bilioni 3; na kiwanda kinatumika kama dhamana + vyanzo vingine
 
Yule mzee yupo zake huko Madale ametulia anavuta tu mpunga waingia kwa akaunti.
hela zinaingia ?
anaweza kufa hajarudisha gharama za kujenga

na bado kuna:
property taxes
business taxes
maintenance costs juu yake
real estate market volatility

renti za $10,000 za JK zilishuka mpaka $3,000 kwa JPM, sijui kama zime rebound
 
hela zinaingia ?
anaweza kufa hajarudisha gharama za kujenga

na bado kuna:
property taxes..
Kwa kuwa Morocco Road ni Prime Area inawezekana kupata zaidi ya hizo $3000.

Ni kweli wakati wa JPM biashara zilivurugika lakini kwa sasa zaonekana zarudia pre 2015.

Ila kwenye maitenance costs mara nyingi owner anashare na mpangaji ila kama ni mimi ntaongeza kwenye full rent.

Hiyo property tax au business tax itategemea na jengo kama ni la kibiashara au nyumba ya kawaida ya kupanga.
 
Inawezekana mafao,mikopo bank, na vyanzo vingine alivyonavyo; ila wengi huwa ni mikopo bank, kwa mfano wenye viwanda hukopa hata zaidi ya bilioni 3; na kiwanda kinatumika kama dhamana + vyanzo vingine
Inaonekana ametumia mafao na akaongeza na mkopo wa benki.

Yaani mafao kanunua jengo na kiwanja kisha akapmba mkopo ajenge.

Benki pia huweza kukupatia au recommending a good contractor akujengee jengo la maana.
 
ha ha ha kila kitu kina umuhimu wake mkuu, ulimwengu wa sasa unataka ujenge kwenda 'vertical' na si 'horizontal'
Mkuu kwa nchi zetu hizi bado tuna mapori mengi sana hatujafikia kuanza kuwa na umuhimu wa kwenda vertically hasa kwenye nyumba za kuishi. Hata nchi zilizoendelea wanaenda vertically mijini tu, ukiingia interior huko watu wanaishi nyumba za chini kawaida.

Ushauri wangu:

Kama una chini ya Tsh 100m isiyo na mawazo, usije hata ukawaza kujenga ghorofa! Kwa chini ya pesa hiyo, hicho utakachojenga kitakua sio ghorofa! Gharama utakazotumia kujenga hicho "kituko" unaweza kujenga nyumba kali sana ya chini ukafunga AC, solar heaters, pavings nje nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…