Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Mkuu MamaNa , Binafsi nimefuatilia sana thread hii na familia yangu ilifuatilia kwa umakini kipindi kile;Nakupongeza sana kwa kushare na jamii mambo muhimu, hili ni jambo ambalo taifa letu limekuwa likikosa. Ila kuna jambo moja kuu lilikosekana --Je unaweza kutupa overview ya benefits and challenges ulizopitia (si unajua all roses have thorns) ; Ili mtu ajiandae , tafadhali share nasi ulivoanza--uliwekeza kiasi gani, ukakwama wapi, na wapi ulibreak through nk (just briefly) maana bado tuko gizani

Binafsi sijawahi kupata ugumu wowote katika kurun Mradi huu kwakuwa nina uzoefu wa kutosha sana katika kilimo hiki. Nimesoma kwa muda mrefu sana na kuanza kujaribu taratibu nje huku nikiwa nafanya research ya magonjwa, mazingira na dharura zote za ukulima. Kisha nikaanza kwa kufata muongozo bila kukosea masharti au kupuuzia ushauri na kanuni. Sidhani kama kuna ugumu wowote katika hili swala kwani Nimeamua kwa moyo mmoja kulifanya.
Halichukui Muda sana, japo linahitaji umakini wa hali ya juu. hivyo basi Kazi zote kwenye Greenhouse nazifanya mwenyewe na zinanichukua Saa moja tu kila siku asubuhi. Mengine yote ni automatic.
Nimeshabreak through siku nyingi sana na sasa mradi unajiendesha wenyewe. Kuna baadhi ya mambo nadhani ukipiga simu ntakuwa katika nafasi nzuri zaidi kukuelezea. bado sijawa comfortable kuzungumzia finances kwa kina huku nikijitolea mfano mimi mwenyewe kwa sababu za kiusalama zaidi.
 
Kazi yako ni nzuri,japo uliniambia ume update video ya ile program ya TBC uliyohojiwa, ipo post no ipi tafadhali
 
Kazi yako ni nzuri,japo uliniambia ume update video ya ile program ya TBC uliyohojiwa, ipo post no ipi tafadhali
Angalia page no 14, Post No 279 kwenye uzi huu.
 
Najenga demo site sasa hv hapadar, ikikamilika ntaupdate uzi huu.
Ntafatilia kuhusu oxfam pia, asante kwa taarifa. Tanzania imeoza sasa hv, ni muhimu sana kuwa makini na kuchagua repolutable people to work with...mbegu feki, mbolea feki na madawa feki yamejaa sana nchini hapa, imekuwa ni vilio na.mayowe ya kila siku kwa wakulima.
nASHUKURU KWA USHAURI MKUU,KAMA IYO SITE IKIWA TAYARI USISITE KUTUJULISHA WADAU ILA NITAKUPIGIA ,KUNA MAMBO YA ARDHI NAYAWEKA SAWA.UNACHOSEMA NI CHA KWELI WATANZANIA LONGOLONGO SANAAAA.
 
Mamana Naomba kujua hapa Dar naweza lima strawberry ?mbegu mnazo? Na nikitaka matikiti maji na carrots?
 
Mamana Naomba kujua hapa Dar naweza lima strawberry ?mbegu mnazo? Na nikitaka matikiti maji na carrots?
Strawberry hailimwi kwa kupanda mbegu bali inapandwa Splits (nadhani kwa kiswahili itakuwa vikonyo), Ukitaka seedlings za strawberry tutakupatia tu. Carrots na Matikiti yes unaweza kulima lakini hutokuwa umetumia vema space yako kwani hazirefuki futi 12.
 
nASHUKURU KWA USHAURI MKUU,KAMA IYO SITE IKIWA TAYARI USISITE KUTUJULISHA WADAU ILA NITAKUPIGIA ,KUNA MAMBO YA ARDHI NAYAWEKA SAWA.UNACHOSEMA NI CHA KWELI WATANZANIA LONGOLONGO SANAAAA.
Site ilishakamilika zamani sana, na wiki Tatu zijazo Mungu akipenda Naanza kuvuna kutoka hapo.
Karibu sana.
 
Maelezo zaidi na mawasiliano tafadhali, napatikana kwa dwapps@yahoo.com

Maelezo yote yapo hapa hapa, ukisoma uzi mzima utayapata bila shaka, Nachelea kurudia yale yale nikawapoteza wale ambao wamekuwa wakifuatilia uzi huu kwa muda mrefu. Mawasiliano pia nimeainisha hapo juu. Namba ya simu ni 0714881500 na Tunapopatikana pia nimeshataja.
Naomba uchukue muda wako wenye thamani kusoma uzi mzima tafadhali.
 
Huu ukulima wa kutumia green houses nimeona kipindi cha AMKA NA BADILIKA kinachoendeshwa na Bw. Sanctus Mutsimbe TBC1, nikajua kuwa kumbe kuwa billionea kwa kutumia kilimo ni kama swala la masaa tu! Ahsante sana kwa taarifa.
 
Strawberry hailimwi kwa kupanda mbegu bali inapandwa Splits (nadhani kwa kiswahili itakuwa vikonyo), Ukitaka seedlings za strawberry tutakupatia tu. Carrots na Matikiti yes unaweza kulima lakini hutokuwa umetumia vema space yako kwani hazirefuki futi 12.

Nahisi kuna kipengele kwenye swali lake hujakijibu mkuu unaweza lima strawberry Dar?
 
Huu ukulima wa kutumia green houses nimeona kipindi cha AMKA NA BADILIKA kinachoendeshwa na Bw. Sanctus Mutsimbe TBC1, nikajua kuwa kumbe kuwa billionea kwa kutumia kilimo ni kama swala la masaa tu! Ahsante sana kwa taarifa.

Kabisa mkuu, na Mimi ndiye niliyekuwa nahojiwa naye.

Karibu sana.
 
Kabisa mkuu, na Mimi ndiye niliyekuwa nahojiwa naye.

Karibu sana.

Hivi hili suala lenu hasa kupima udongo na maji ni wakweli maana sisi watanzania kuingizana mjini wala sio kazi kubwa. Unaweza kulipa hela yako ya kupima udongo na maji ukaja ukakuta ofisi imefungwa. Nasema hivyo kwani nina uzoefu wa watu kutapeliwa sijui wanatafutia kazi nchi za nje lakini watoe hela kwanza kwa ajili sijui ya usaili na porojo kibao. Matokeo yake watu walishaka vichwa.
 
Mkuu uliahidi utaweka hewani website yenye dondoo kadha wa kadha na Je una detailed manuals za baadhi ya mazao - tunaweza kuchangia mkuu kama zipo tuelekeze
 
Back
Top Bottom