Jenga tabia ya kutambua mchango na juhudi za unaowaongoza au kuwasimamia

Jenga tabia ya kutambua mchango na juhudi za unaowaongoza au kuwasimamia

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
KIpindi fulani niliwahi kufanya kazi na wahindi ikiwa ndio ajira yangu ya mwanzo kabisa baada ya kumaliza kidato cha sita,nikiwa nasubiri matokeo nikapata hiyo kazi katika kampuni ya ujezi

Hawa jamaa kwa kawaida huwa hawana kawaida ya kukupongeza hata ufanye kazi vizur kiasi gani,wao ni lawama tu lakini wana tabia ya kuwaeleza watu wa pembeni kuwa fulani ni mchapa kazi mzuri sana,hata kwangu ilitokea hivyo

Kwao wao wanadhani lile jambo zuri ila kiukweli ni jambo baya sana linashusha sana morali ya kazi,na hata unaweza kuichukia kazi yenyewe,kwasababu utajitoa kwa moyo wote lkn machoni kwao watalaumu tu

Hakuna kitu kizuri kama kutambua mchango wa wafanyakazi wako,ukatambua juhudi zao hakika hii huwapa hamasa ya kujituma zaidi na kufurahia kazi yao,nawapongeza sana viongozi wa mabank hapa nchini,ni mara nyingi sana utakuta pale bank kuna tuzo ya mfanyakazi bora wa wiki au mwezi.

Kile kitendo tu cha kutambuliwa mchango wako ni motivation tosha kwa mfanyakazi azidi kupambana,na hata staff wengine wanapata hamasa ya kupambana zaidi ili mchango wao upate kutambuliwa

Katika mpira tunaona kuna mchezaji bora wa mechi husika au mchezaji mwenye nidhamu na mambo kama hayo,ni jambo zuri sana kwakweli,viongozi makini wanalitambua hili.

Na wewe mama ebu jifunze kutambua mchango wa dada wa kazi au kaka wa kazi,hujui ni kiasi gani watajisikia vizuri sana na hata mapenzi yataongezeka kwako na kwa watoto wako,mwambie dada wa kazi "tangu uwe nasi hapa tunakula kwa wakati,usafi umeimarika na hata watoto naona wanafuraha kwakuwa unawajali sana" hii kauli inaweza kuwa ni nyepesi lakini deep down ina uzito wa tani moja katika moyo wa mtu

Tujenge tabia ya kutambua michango,jitihada na kujitolea kwa watu wengine ili kuwapa moyo na kuzalisha hamasa kubwa mioyoni mwao,wakati mwengine watu hawahitaji fedha tu,bali wanahitaji hitaji la kutambuliwa mchango wao katika jamii husika

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom