Elections 2010 Jengo la Machinga ni hatari kwa binadamu: Wakaguzi

Elections 2010 Jengo la Machinga ni hatari kwa binadamu: Wakaguzi

Morani75

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2007
Posts
613
Reaction score
19
Wakuu, leo nimeisoma hii (a bit delayed though) kuhusu majengo yetu mapya ya wamachinga pale Karume... Kwa kweli ni masikitiko sana kwa ripoti hii walioyotoa kuhusu majengo husika.
Maswali yangu ni:
1. Nani alipitisha michoro, designs etc?? Hawakuona makosa then??
2. Majengo yameanza kujengwa sasa yanakaribia kwisha ndipo wataalamu eti wanasema hayapo kwenye viwango vya kukidhi matumizi ya bionadamu. Sasa tuweke ng'ombe au kuku humo ndani?? Walikuwa wapi hawa so-called wataalamu??
3. Zamani kuklikuwa na wakaguzi wa majengo, barabara na miradi yote ya ujenzi kutoka manispaa na idara nyingine husika. Wanakagua mabango etc, kisha wanaruhusiwa kupitia michoro etc, je hawa walikuwa wapi??
4. Mhandisi aliyefanya design ya majengo haya, alipewa vigezo gani katika kufanya kazi yake?

The list goes on and on!!
Kweli tumeingiliwa Tanzania.... Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!

Wakaguzi watahadharisha Jengo la Machinga ni hatari kwa binadamu

Na Mkinga Mkinga

JENGO jipya kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama machinga, linaloendelea kujengwa jijini Dar es salaam, si salama kwa binadamu kwa kuwa baadhi ya vipimo havikuzingatia matumizi ya jengo.

Hayo yamebainishwa jana na timu ya bodi ya wasanifu na wakadiriaji majengo iliyotembelea jengo hilo lililopo katika makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kulikaguzi jengo hilo linalotazama Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, msajili wa bodi hiyo, Abraham Marres alisema ngazi za kupandia kwenda juu za jengo hilo ni ndogo za kuwezesha watu wawili tu kupita kwa wakati mmoja hivyo kuwa hatari wakati kunapotokea matatizo yanayotaka watu wengi watoke kwa wakati mmoja.

Alisema hali hiyo ni tofauti na kimo cha maghorofa ya jengo hilo, ambalo lilitembelewa na Rais Jakaya Kikwete miezi michache iliyopita.

"Hapa hebu tuweke pembeni siasa, hizi ngazi ni nyembamba haziwezi kufikia upana wa zile za soko la Kariakoo ambalo limejengwa muda mrefu uliopita wakati mahitaji pamoja na idadi ya watu sio kama hii ya leo," alisema Marres.

Aliongeza kuwa, japokuwa hakuwa amepewa michoro ya jengo hilo ili kuweza kufanya ulinganifu kutokana na wahusika kutokuwepo kwenye eneo la ujenzi, bado uwazi kati ya paa na urefu wa mtu (headroom) katika kila ghorofa ni kidogo ukilinganisha na msongamano wa watu watakaoingia katika jengo hilo.

Ukaguzi wa jengo hilo umefanyika kutokana na bodi hiyo kuamua kupitia majengo makubwa yanayoyojengwa jijini Dar es Salaam ili kujionea kama sheria za ujenzi zinafuatwa na wataalamu wa fani hiyo.

Bodi hiyo jana ilifanya ukaguzi wa majengo mawili- Machinga Complex na jengo la ghorofa kwa ajili ya nyumba za polisi linalojengwa kando ya Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ukaguzi huo, mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk Ambwene Mwakyusa alisema imefikia wakati kwa wajenzi wote kutumia wataalam wa majengo ili kuondokana na adha ya kuanguka mara kwa mara kwa majengo hapa nchini ili kurejesha heshma ya taaluma hiyo ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi (Architect and Quantity surveyor).

Aliongeza kuwa kama taratibu hizo zitakuwa zinafuatwa basi itakuwa rahisi kuwawajibisha wabunifu majengo ambao katika taratibu za majenzi wao ndio huwa wanatakiwa kuwa wasimamizi wakuu wa ujenzi unaokuwa unaendelea.

"Katika shughuli hizi za ujenzi, anayetakiwa kuwa msimamizi mkuu wa majengo katika ujenzi wowote ule ni mbunifu majengo, pia wataalam wengine watakuwepo wakipeana maelekezo lakini chochote kikitokea katika eneo la ujenzi anayewajibishwa ni mbunifu," alisema Dk. Mwakyusa.

Aidha msajili Marres alisema kuwa majengo yote si nyumba, ila nyumba ni majengo akimaanisha kuna taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kutofautisha kati ya mambo hayo mawili, hali ambayo husababisha wajenzi wengi kufanya vitu kiholela.

Msajili huyo alishauri majengo yote makubwa yatolewe kwa zabuni akisema kwa kufanya hivyo itawafanya wazabuni kuwa na ushindani na hivyo kuwezesha kupatikana kwa mtu ambaye ni bora zaidi, kuliko kutumia mkandarasi wa kujuana.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tatizo la majengo kuanguka kutokana na kutofuatwa kwa taratibu za ujenzi, ikiwa ni pamoja na jengo la Kisutu, pamoja na hoteli ya Chang'ombe Village.

Mwananchi, 04/11/2008
 
Baada ya ukaguzi wangesema hatua gani zichukuliwe
 
jamani tuna matatizo gani? yaani mpaka raisi anakwenda kukagua jengo halikidhi viwangoooo...huu ni usaniii mbaya kwani hapa tunacheza na maisha ya watu kwa kuendekeza siasa za kujipendekeza kwa wateule. nilimsikia meya siku raisi katembelea akimsifia mheshimiwa ulitushauri na sasa tumetekeleza.. jamani hawa viongozi wasiojali jamii na wanaotumia upeo mdogo wa jamii kubwa wanayoiongoza HAWATUFAIIIII. Meya wa jiji kama dar hana vision na sio mtu wa vitendo kimaendeleo bali sifa tuuu kwa wateuleeee....TUREKEBISHE MFUMO HUU WA KUWAPATA VIONGOZI WETU TUKIANZA NA MAMEYA WA MAJIJI.. WACHAGULIWE NA WANANCHI SIO UTARATIBU WA SASA....

Sasa na hiyo bodi mapendekezo yake nani wa kuyafanyia kazi?? hawana meno kuzuia kuendelea kwa ujenzi ili kuokoa maisha ya watu pindi litakapoanza kutumika????
 
Mkuu Morani naomba nitoe moaoni tofauti kidogo.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kulikaguzi jengo hilo linalotazama Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, msajili wa bodi hiyo, Abraham Marres alisema ngazi za kupandia kwenda juu za jengo hilo ni ndogo za kuwezesha watu wawili tu kupita kwa wakati mmoja hivyo kuwa hatari wakati kunapotokea matatizo yanayotaka watu wengi watoke kwa wakati mmoja.
.........
Aliongeza kuwa, japokuwa hakuwa amepewa michoro ya jengo hilo ili kuweza kufanya ulinganifu kutokana na wahusika kutokuwepo kwenye eneo la ujenzi, bado uwazi kati ya paa na urefu wa mtu (headroom) katika kila ghorofa ni kidogo ukilinganisha na msongamano wa watu watakaoingia katika jengo hilo.
Walienda kukagua kienyeji? Walipaswa wafanye mawasiliano (ikiwa ni pamoja na kuomba/kupitia michoro) ndipo wakakague...hawa ni wataalam na sio wanasiasa.

“Katika shughuli hizi za ujenzi, anayetakiwa kuwa msimamizi mkuu wa majengo katika ujenzi wowote ule ni mbunifu majengo, pia wataalam wengine watakuwepo wakipeana maelekezo lakini chochote kikitokea katika eneo la ujenzi anayewajibishwa ni mbunifu,” alisema Dk. Mwakyusa.
Kuanguka kwa majengo (kwa mtizamo wangu) kunahusiana na uhandisi zaidi kuliko ubunifu. Pia msimamizi mkuu wa ujenzi si lazima awe mbunifu majengo, ila yeyote mwenye taaluma ya 'construction management', lakini lazima awepo mbunifu kama sehemu ya timu. Nadhani ni kosa mbunifu kuwa kiongozi wa timu anayeichezea (au ni falsafa ya kocha mchezaji?). Ni vema msimamizi mkuu wa ujenzi wa jengo akawa tofauti na wasimamizi wengine.

Baada ya udhaifu huu kufanyike nini? Majengo haya yabolewe?
 
Hili jengo lilikuwa bomu toka lilipobuniwa! Leo ndio hao wakuu wanatambua hilo? Umesikia wapi jengo la biashara la machinga la ghorofa? Wametupa hela zao kama walivyofanya kwenye masoko ya kisasa huko Kijitonyama na kwengineko. Mara kumi wange-pedestrianise mitaa kadhaa na kuruhusu wamachinga wafanye biashara zao humo.

Kwenye hili, tumeliwa! Tena sana.
 
Kuanguka kwa majengo (kwa mtizamo wangu) kunahusiana na uhandisi zaidi kuliko ubunifu. Pia msimamizi mkuu wa ujenzi si lazima awe mbunifu majengo, ila yeyote mwenye taaluma ya 'construction management', lakini lazima awepo mbunifu kama sehemu ya timu. Nadhani ni kosa mbunifu kuwa kiongozi wa timu anayeichezea (au ni falsafa ya kocha mchezaji?). Ni vema msimamizi mkuu wa ujenzi wa jengo akawa tofauti na wasimamizi wengine.

Baada ya udhaifu huu kufanyike nini? Majengo haya yabolewe?

Mkuu, failure ya jengo si kuanguka tu. Yale yaliyotokea tabora hivi karibuni ni failure. Yale yanayoendelea kutokea shimoni kariakoo ni failure! Mtu anayewajibika katika failure zote hizi ni mbunifu maana ndiye anayeamua upana wa milango na ngazi, sehemu ya madirisha, idadi ya watu watakaoweza kutumia na kuhakikisha kuwa matakwa ya mshitiri yanazingatiwa bila ku-affect usalama wa watumiaji. Wahandisi wote wanamsaidia mbunifu katika kutimiza haya malengo. Kwa vile yeye ndiye aliyelibuni jengo basi common sense inasema kuwa itakuwa vyema kama akisimamia ili ahakikishe kuwa aliyokusudia yanatimizwa. matatizo yakitokea baadae ni yeye atakayewajibika. Hii ni common sense lakini ukweli ni kuwa kutokana na kuwepo na aina nyingi ya mikataba si kila wakati huyu mbunifu anakuwa msimamizi. Hii inatokana wakati mwingine na complexity ya majengo yanayojengwa siku hizi na vile vile washitiri kutaka kuhakikisha kuwa wanapata value for their money. Si kosa kwa mbunifu kusimamia alichojenga lakini si lazima iwe hivyo. Mshitiri ndie muamuzi wa mwisho na inabidi apime pros and cons. Siku hizi washitiri wengine wamekuwa na mtindo wa kuajiri mtaalamu mwingine baki atakayewasimamia wote ( Client representative). Huyu ni kuhakikisha kuwa mbunifu, wahandisi na makandarasi wa stay focused na ku-deliver walichoahidi. Katika mfumo huu, mbunifu anabaki kuwa msimamizi bali Client Representative anaweza kumchongea kwa mshitiri. Mfumo huu unamfanya mbunifu kuwa makini zaidi.
 
Yaleyale niliandika jana. Siasa na field ya UJENZI wanapendana kama chanda na pete. Watu wanazidi kukusanya pesa za uchaguzi. Wameyajenga bomu kwa bei ya ovyo na mwisho yabomolewe au wayabadili na hii itakuwa kwa pesa kubwa sana.
Au ni ile ajali ya huku kwetu Tabora ndiyo imewaamsha? Naona zamani walikuwa wanasema ahh hivyo hivyo. Ila sasa wameona watu wanakufa wanaanza kuamka. Hawa wote inabidi kubadili inchi na unaanzia kuwachapa risasi wahusika waliokula 10%.
 
tatizo la wasomi wa tanzania ni kuendeshwa na watu wasio na taaluma husika ktk utendaji, wahandisi wanapokea maagizo ya wanasiasa na kuyatekeleza bila kujali madhara yake.

1,kwa ufinyu wa mawazo yangu jengo linapojengwa linatakiwa kukaguliwa hatua kwa hatua na wakaguzi wa ndani na nje ili kujiridhisha na ujenzi.
-Je kwa bongo hili ilipo kweli au anaogopwa makamba.
2,kujiita msomi au mwanataaluma ukiwa tanzania ni aibu,tena sana ukilinganisha na mambo yanavyokwenda, ndivyo sivyo.
 
We unadhani lini rais au waziri wa wizara gani sijui inayohusika na mradi huo ataunda tume kama hawakujenga kitu kibovu cha angalau kuu watu kidogo au wengi?
Watu wanafukuzia posho za tume ya kuchunguza wewe unalalamika mkuu?
 
Imebidi niliseme hili maana sioni watu wakilisema sana....

ujenzi wa majengo yanayoitwa machinga complex kwa maoni yangu

ulikuwa ni mpango wa kipuuzi sana........na hakuna faida yeyote itakayokuja
kutokana na hilo.........na..ni matumizi mabovu ya pesa....

kwanza gharama iliyotumika ya bilioni kumi.....ukitazama
bilioni kumi ingeweza kutumika kwenye mambo mengi ya maana

mfano mradi wa mabasi yaendayo kasi,ambao nao gharama zake
zilitajwa ni bilioni kumi za msaada....

tungeweka mabasi hayo yaendayo kasi kwenye njia kuu

nne za jiji basi msongamano na foleni zingepungua sana....

kingine ni ukosefu wa masoko makubwa pembezoni
mwa jiji ambayo yangesaidia kupunguza msongano wa wanaokwenda na kutoka kariakoo..

tatu ni bora tujiulize,hivi hao wamachinga hizo bidhaa

wanazitoa wapi????????
nani anaeagiza kutoka nje?????
kwa nini yeye anaeagiza asiuze mwenyewe ili kupunguza gharama
za middleman????????

kwa nini tu invest kwa wamachinga wakati sio wao wanaotengeneza wala
kuagiza bidhaa hizo??????

halafu hayo majengo ya machinga complex sana sana yataongeza
foleni na msongamano jijini......
 
Kwani ni pesa hizo tu za ujenzi wa machinga complex ndio tumezipoteza? we do it everyday, even worse we will keep on doing that.
 
kwani ni pesa hizo tu za ujenzi wa machinga complex ndio tumezipoteza? We do it everyday, even worse we will keep on doing that.

kilichinifanya niandike ni pale
nilipomuona adam kimbisa akijisifia kuwa
machinga complex ni ubunifu wake.....kama vile ni jambo la maana...
Wakati mimi naona ni ujinga mtupu..........
 
kilichinifanya niandike ni pale
nilipomuona adam kimbisa akijisifia kuwa
machinga complex ni ubunifu wake.....kama vile ni jambo la maana...
Wakati mimi naona ni ujinga mtupu..........
Boss naomba nitofautiane na wewe kuhusiana na Machinga complex.

Mfumo wa biashara huwa una chain ndefu saaana kutokea kwa manufacturer mpaka kwa mteja mwenyewe. Na chain hiyo mara nyingi hutegema aina bidhaa.

Pia kumbuka Machinga Complex imekuja kwa lengo la kurasimisha mfumo wa biashara za mitumbo na wakati huohuo kuhakikisha mpangilio wa jiji unakuwa sasa. Kwahiyo nadhani tuipime machinga kwa malengo haya, je yanafikiwa au yatafikiwa?

Ila kwa ujumla si potevu wa fedha tena kama zimetumika ipasavya.
 
Mafisadi wameshafanya vitu vyao tena! Mungu inusuru Tanzania yetu.
 
Wanaongeza foleni tu....na msongamano...
Na bandari ya nchi kavu (kwa ajili ya makontena toka bandarini) iliyojengwa maeneo ya Kamata (karibu na darajani tokea mataa ya Chang'ombe)?

Sijui nani huwa anatoa plans hizi... Barabara ya Mwenge - Ubungo (Sam Nujoma Rd) tayari ishaanza kuharibika vibaya, sasa hii ya kuweka eneo la kutunza makontena hata kabla ya kuandaa barabara ni mawazo ya binadamu mwenye kufikiria mbali kweli?

Sometimes akili za watawala wetu zinachanganya mno! Hii inahitaji washauri kujua kuwa ni makosa makubwa yanafanyika?
 
Mkuu invisible.....
Viongozi wetu hawana imagination
from the end kuja kwenye mwanzo...
Wao kila kitu ni kutatua tatizo linapojitokeza....

Wanasema zaidi ya watanzania milioni moja na nusu
wana matatizo ya afya ya akili.....
I keep asking myself,ni viongozi wangapi hawapo kwenye kundi hilo?????????
 
mkwere mwezenu anajua atapata kura za machinga hapo.
lakini kama wajumbe wliotakulia jamaa ameboronga
 
kilichinifanya niandike ni pale
nilipomuona adam kimbisa akijisifia kuwa
machinga complex ni ubunifu wake.....kama vile ni jambo la maana...
Wakati mimi naona ni ujinga mtupu..........

Mkuu lile ni jambo la kijinga kabisa. Ningekuwa JK kama kulikuwa na ulazima wa kutumia pesa hizo kwa ujenzi wa nyumba, basi ningetumia pesa hizo kujenga flats 4 za kisasa na kuzifanya makazi ya expatriates watakaokuja kufanya kazi hapa bongo. Mpaka sasa hatuna facility ya namna hiyo amabye ingeweza kuwa na manufaa ya muda mrefu. For sure ni ujinga mtupu it wastage of money.
 
Leteni zile picha kwanza ya machinga complex,niliona picha yale banda utasema ya wanyama na ni madogo mno na pia nafasi ya kupita kwenda kwenye mabanda ni madogo sana.nina wasi wasi na afya za watanzania kwenye lile jengo na wizi pia.
 
Back
Top Bottom