Watu wa kulaumiwa hapa ni ma'architecture' (samahani MKJJ, wahandisi nafasi yao ni ndogo sana katika hii ishu hususan tukiangalia majengo). Wao ndio wanaobuni na kudesign majengo na inawabidi wafikirie watumiaji wote ( walemavu wa miguu, vipofu, viziwi, mama waja wazito, watu wa makamu, watoto wadogo n.k.) Hili mara nyingi hawafanyi. Pamoja na hao ni manispaa na vyombo vya serikali vinavyotoa vibali vya ujenzi. Hawa wanapaswa kushinikiza hadi regulations zinazotumika zibadilishwe na kuingiza kipengele cha accessibility kwa jamii nzima kwenye public buildings ( si ya serikali peke yake)
I stand to be corrected, lakini ninavyofahamu mimi building regulations tunazozitumia ni zile tulizorithi kutoka kwa waingereza na kuzitia vilaka. Sidhani kama moja ya kilaka kinahusu accessibility kwa watu wote! Ramp kama zinawekwa ni kama mawazo ya baadae lakini ni mara chache sana kupewa uzito tokeahatua za mwanzo. Ni majengo mangapi ya public ( ya serikali, bar, hoteli, kumbi za mikutano, vituo vya reli, vituo vya mabasi, airport, makanisa, misikiti n.k) vyenye vyoo kwa ajili ya walemavu? Ukweli ni kwamba hatuwajali na tunawaona ni kero.
Huyo muungwana aliyesimama kushoto unaweza kukuta ni wakili wa huyo mlemavu na anaona anamchelewesha!
Tuna safari ndefu lakini......Amandla.................!