Jengo la PSPF mita 134 ndo Refu Tanzania, Wenzetu wanajenga Jengo lenye Urefu wa Mita 1,700 huko Tokyo

Hakika baada ya mapinduzi ya fedha yao nilifikiri japan atatambua kuwa kumzidi uchina tena ni jambo lisilowezekana kutokana na ukubwa wa uchina
 
Wakijenga kuna occupants wa kurudisha mtaji na hatimaye faida?
Fikiri kabla ya kuandika
 
Tanzania wapangaji wa magorofani wachache sana.
Lile la mawasiliano tupu.
Yale ya Moroco sijui wataanza kupangisha lini maana toka 2016 huko yapo tu na yamekamilika.
Kuna chuo kilipanga KKKT Kinondoni toka kilivyohama hapajapangishwa tena.
 
Hii Japan si ndo juzi tu kumetokea tetemeko kwenye mji wa Kumamoto na kuua watu?! Anyways Tanzania magorofa marefu ya nini wakati nje kidogo tu ya miji mikubwa kuna mapori kibao. Kibongo bongo maeneo yaliyokaliwa na watu ni madogo kuliko yaliyo wazi. Kingine majanga ya moto, nyumba tu za chini kukitokea majanga ya moto hua tunashindwa kuzima, leo hii mtu anaongelea jengo la mita 1700, Mzee si itakua unajenga tu makaburi ya kuzikia watu na mali zao?!
 
Hapo tu Victoria maghorofa kibao yapo empty,,, mengine wamejaribu kupangisha watu waishi wananchi hawa afford gharama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…