Jengo la PSPF mita 134 ndo Refu Tanzania, Wenzetu wanajenga Jengo lenye Urefu wa Mita 1,700 huko Tokyo

Jengo la PSPF mita 134 ndo Refu Tanzania, Wenzetu wanajenga Jengo lenye Urefu wa Mita 1,700 huko Tokyo

Acha Japan ajitutumue alafu China aje afanye kufuru ya kujenga jengo ambalo mtu atakuwa anachukua wiki nzima kufika juu.
Tatizo kibongobongo, wengi tunadhani jengo kuwa na gharofa nyingi ni maendeleo na ujuaji. China, Japan etc wao population yao ni kubwa na maeneo ya kuishi ni yamepungua ndiyo maana wanafanya hivyo. Sisi kwa ujinga wetu tunaiga. Hilo wanalosema linajengwa Zanzibar nalo ni ulimbukeni kwa kiarabu tu. Zenji wameiga kwa waarabu ambao hupenda kufanya vitu kwa sifa na ufahari kwa sababu tu wana fedha.
 
Kwa japan ni hatari sana kufanya ujenzi wa aina hiyo... ni kisiwa cha baharini ambacho hukumbwa na madhira kama tetemeko.. unaweza ukabisha ila hata ujenzi wa titanic ulikatizwa na mambo yasitozuilika na mwanadamu...
Ushauri wangu wawe na kiasi
Unahisi wao hawajui hiki ulichoandika?
 
Hapo tu Victoria maghorofa kibao yapo empty,,, mengine wamejaribu kupangisha watu waishi wananchi hawa afford gharama
Tunataka kuigaiga tu.

Miaka ya mwanzo ya tisini nilikuwa na rafiki yangu mmoja Mjapani. Siku moja tumekaa hapo Bamaga Bagamoyo Road.

Sasa, nikamuona yule Mjapani anapaangalia sana pale, lile eneo la kuelekea Mwenge. Nikamuuliza mbona unapaangalia hivyo?

Akasema hii nchi mna bahati sana bado hamjajua tu, hii sehemu natamani ningekuwa na uwezo wa kupata sehemu iko wazi kama hivi Tokyo.

Yani alishangaa sana kuona eneo kubwa kama lile liko wazi tu, mjini Dar.

Wenzetu wanajenga maghorofa marefu kwa sababu hawana nafasi. Manhattan wamejenga mpaka wakakiongeza kisiwa ili kuongeza ardhi.

Sisi tunataka kujenga kwa mapambo!
 
figganigga umepuyanga. Lile mawasiliano tower limewashinda kulijaza bado mnataka majengo marefu ya nini?

Wajapan sio wenzako, wao hawakuoni wewe kama mwenzao hata kwa bahati mbaya. Hizi shobo za kuita watu "wenzenu" muache.
 
China tuu yenyewe Shanghai tower imepangishwa nusu tuu kwingine wamekosa wapangaji ndio iwe bongo
 
Tatizo kibongobongo, wengi tunadhani jengo kuwa na gharofa nyingi ni maendeleo na ujuaji. China, Japan etc wao population yao ni kubwa na maeneo ya kuishi ni yamepungua ndiyo maana wanafanya hivyo. Sisi kwa ujinga wetu tunaiga. Hilo wanalosema linajengwa Zanzibar nalo ni ulimbukeni kwa kiarabu tu. Zenji wameiga kwa waarabu ambao hupenda kufanya vitu kwa sifa na ufahari kwa sababu tu wana fedha.
Wabongo tunaiga kila kitu hata vile ambavyo vinaweza kuwa na madhara kwetu sisi tunaiga tu.
 
Back
Top Bottom