Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Ni aibu kubwa mazingira ya jengo hili kuwa machafu ili hali liko katikati ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Uchafu huo unaharibu taswira ya mji na kuufanya kuonekana mchafu na kuibua maswali mengi kwamba inamaana watu wenye mamlaka hawaoni uchafu huo?
Natoa wito kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kuhakikisha ukarabati na usafi ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu, kama hivi karibuni Katibu Tawala Mkoa wa Katavi alivyoripoti kipindupindu.
Nashauri kwa kuwa jengo hilo liko Manispaa ya Mpanda ni vema sasa Wilaya ya Tanganyika ikalimilikisha jengo hilo kwa Manispaa hiyo kwani itakuwa rahisi kwa jengo hilo kukarabatiwa na mazingira yake kufanywa kuwa safi.
Kwa sasa jengo hilo linatumika hususani wakati wa mitihani ya Wanafunzi, ndio huwaga tunaona wanakwenda hapo na limefanywa kuwa kama bohari ya kutunzia mitihani.