muhomakilo jr
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 15,301
- 13,858
Mdosi manji kazingua,sasa mzee Akilimali alipe deni alambe ujiko..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usiweke team zisizo husika ,we sema yanga.Haya matimu yetu yasiyo na mipango ya kujiendesha kisasa acha tu lipigwe mnada!
Labda ukiondoa Azam Fc tuUsiweke team zisizo husika ,we sema yanga.
Wakiambiwa club zijiendeshe zenyewe wao hawataki wanataka kumtegemea mtu sasa mzee akilimali alipe hilo deni
Acha uongo wew.Jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambazo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.![]()
Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa kampuni ya udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.
Akizungumza na gazeti hili jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwepo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.
Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la Makao Makuu haujafanyika.
"Ni kweli kesi iko katika mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi", alisema kwa kifupi Mkwasa, Kocha na Mchezaji wa zamani wa timu hiyo.
Chanzo: Nipashe
Tatizo linakuja kwamba wanachama wengi ni hewa hata ukifuatilia kadi za uwanachana hawan.Yanga ina mashabiki zaidi ya milioni kumi nchi nzima, wanafika hata milioni ishirini.
Viongozi wakiweka utaratibu mzuri mashabiki wana moyo sana na team yao,ukipata mashabiki milioni moja tu kila mmoja akachanga shilingi mia tano tu tayari una shilingi milioni mia tano, deni linalipwa na chenji ya soda ya wachezaji inarudi.
Sidhani kama mashabiki wenye uchungu na team yao watakuwa tayari kusimama pembeni kuangalia club inakwenda shimoni wakati wanaweza kufanya jambo,kinachokosekana hapa ni ubunifu,na muhimu zaidi washabiki wahakikishiwe uaminifu mipangilio mizuri, nina hakika wataonesha ushirikiano- jambo hili ni kubwa lakini ni dogo sana wanayanga wakiwa na umoja kwani UMOJA NI NGUVU.
Kama halikupaswa kuwepo basi ilikuwa haina umuhim wa wakandalasi kabla gorofa halija jengwa lazima lipimwe kwamba linafaa au halifai.Lipigwe mnada tu! Na atakayelinunua atakuwa fala kwa sababu hilo eneo lote la bonde ni condemned! Ni ubutu tu wa serikari zetu kutekeleza maamuzi, vinginevyo hilo jengo kwanza halikupashwa kuwepo.
HumjuiMzee Akilimali ni Nyani..?