Jenista Mhagama: Taifa lina dawa za kujitosheleza za kufubaza virusi vya ugonjwa wa ukimwi

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema kuwa kutokana na madiliko ya kisera ya Nchi ya Marekani baada ya kuingia madarakaini Serikali mpya ya Rais Trump kuathiri Sekta ya Afya Serikali imefanya Tathimini ya kina ambapo wamepata majibu kuwa Taifa lina dawa za kujitosheleza za kufubaza virusi vya ugonjwa wa ukimwi

Mhagama ameyasema hayo Leo Aprili 25,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari

Mhagama amesema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kwani Serikali imeshafanya Tathimini ambapo sasa Kuna dawa hizo za ARV mpaka za mwezi Juni 2025

Mhagama amesema kuwa kutokana na Tathimini hiyo ya kina ya mahitaji ya Wizara ya Afya tayari wameshapata fedha Shilingi bilioni 93 kutoka Serikalini ambapo zimewezesha kuagiza dawa za magonjwa mengine ambayo fedha zake zilikuwa zikifadhiliwa na wafadhili

Aidha Mhagama amewataka wananchi kutulia kwani hakuna upungufu wa Dawa na hawatapata matatizo ya aina yoyote

Source: Wasafi Tv
 
Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema kuwa kutokana na madiliko ya kisera ya Nchi ya Marekani baada ya kuingia madarakaini Serikali mpya ya Rais Trump kuathiri Sekta ya Afya Serikali imefanya Tathimini ya kina ambapo wamepata majibu kuwa Taifa lina dawa za kujitosheleza za kufubaza virusi vya ugonjwa wa ukimwi

Mhagama ameyasema hayo Leo Aprili 25,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari

Mhagama amesema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kwani Serikali imeshafanya Tathimini ambapo sasa Kuna dawa hizo za ARV mpaka za mwezi Juni 2025

Mhagama amesema kuwa kutokana na Tathimini hiyo ya kina ya mahitaji ya Wizara ya Afya tayari wameshapata fedha Shilingi bilioni 93 kutoka Serikalini ambapo zimewezesha kuagiza dawa za magonjwa mengine ambayo fedha zake zilikuwa zikifadhiliwa na wafadhili

Aidha Mhagama amewataka

wananchi kutulia kwani hakuna upungufu wa Dawa na hawatapata matatizo ya aina yoyote

Source: Wasafi Tv
Time will tell!
 
Siku zote usiwaamini wana siasa wote ni waongowaongo tu kwa maslahi yao.
 
Vizuri mh Waziri ingawa mwezi juni siyo mbali.
Hata hivyo msisahau na chanjo za Kifaduro, Pepopunda na Surua kwa watoto wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom