Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kitaendelea kusimamia ubora wa elimu katika Jimbo la Peramiho na kuongeza miundombinu ya vyumba vya madarasa 255 ili kuwezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora zaidi
Hayo yamebainishwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Bi. Jenista Mhagama, akiwa katika Kijiji cha Lipokela, Kata ya Mbingamharule akinadi Sera za CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuomba ridhaa kwa wananchi kukipigia kura ya ndio chama hicho ili kiendelee kuwaletea maendeleo
Amesema kupitia ilani ya CCM, zaidi ya vyoo vya 150 vitajengwa katika shule zote za msingi katika Jimbo la Peramiho
Kuhusu elimu ya Sekondari, Bi. Mhagama amesema kuwa Serikali ya CCM inayomaliza muda wake imefanya kazi kubwa ya kuboresha ubora wa elimu na sasa ufaulu wa wanafunzi wa Sekondari umeongezeka kutoka asilimia 76 hadi 97 ndani ya kipindi cha miaka mitano
Bi. Mhagama amewaomba wananchi ifikapo Oktoba 29, 2025 kushiriki kwenye uchaguzi mkuu na kukipigia kura ya ndio CCM kupitia wagombea wake kuanzia Mgombea Urais Dkt Samia Suluhu Hassan, yeye mwenyewe anayegombea nafasi ya Ubunge pamoja na Madiwani wagombea kupitia CCM