Jenister Mhagama, Simbachawene, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao na PSSSF

Jenister Mhagama, Simbachawene, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao na PSSSF

Mhe Jenister Mhagama, Mhe Simba Chawene Waziri wa mambo ya ndani, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao yetu na PSSSF, Tumestaafu Mwaka jana mwezi wa 12 Hadi sasa Hatuja pata mafao yetu wala Pesheni hatulipwi. Jana tarehe 1/11/2021 saa 1 usiku tumeenda kukagua akaunti zetu ATM tukiwa wastaafu 4 hamna kitu.

Msemaji wa Serikali anacho kizungumzia kuhusu malipo yetu si kweli, Mara aseme tumekosea taarifa tunahitaji kurekebisha, mara anasema huenda tumetapeliwa sasa tunashindwa kuzieleza familia zetu ukweli. Hii haiwezi kuwa kauli za Msemaji wa Serikali kwa niaba ya Serikali vema akafuta kauli kama hizi, hata tukitapeliwa yeye Msemaji inamhusu nini. Kama Serikali ikiwa haijapata pesa za kutulipa Wastaafu aseme tu ukweli.

Tumeenda mara kadhaa ofisi za Mkoa za PSSSF hawana majibu, wanasema tu zilipokelewa mwezi wa 1 ziko mikononi mwao pale makao Makuu ya PSSSF basi hakuna jibu lingine.

Mhe Jenister Mhagama, Mhe Simba Chawene, IGP Simon Sirro tusaidieni tulipwe mafao yetu PSSSF tusaidieni, mpo ofisini maisha yenu ni mazuri, Nauli zetu pia ambazo zipo kisheria toka tumejaza miezi 2 kabla ya kustaafu hatuja lipwa na madeni mengine ya kwenda wkenye vyeo kama nauli hazijalipwa.

Ombi hili liwafikie popote mlipo au anayesoma awafikishie.
Mimi natamani mfe kabla hamjapata
 
Mkuu kwani wewe ulikuwa unafuatilia makato yako yalikuwa yanapelekwa kwenye mfuko?
Hata wapelekewe makato, kutoa hawataki kufuata utaratibu
Au wanataka mpaka watu waandamane na mabango.
Labda mkurugenzi na mhasibu hawataki kufanya kazi bila bughudha
 
Ndio uchumi wa Kati unaokuwa kwa 7%.
Naona mwezi huu hawalipwi kabisa sababu hata sisi ambao tumestaafu na kustaafu kwenyewe tumestaafu ( just waiting to kick the damn bucket and exit) hatujalipwa hela ya hazina. Pole sana.
Au hawana hela
 
Watu na bahati zao. Enzi zile za mjomba hapo PSSSF kingeumana
 
Sasa huyo Mhagama anatoa wapi hiyo sauti ya mamlaka?
Anaposimamia huyo lazima pawe donda ndugu
 
Back
Top Bottom