The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
View: https://youtu.be/WhlUbdvI5CA?si=6EYlRBSl4ZN0QnT5
Akihojiwa na SAUT DIGITAL, Mwanasiasa na mwanachama mwaminifu wa CHADEMA, jirani yake Tundu Lissu huko wanakoishi kwa takribani miaka 21 Mzee Jeremiah Masanja ametoa maoni na mtazamo wake juu ya hali ya CHADEMA sasa na wagombea uenyekiti wawili wenye nguvu, Freeman Mbowe na Tundu Lissu...
Anasema wote wawili anawafahamu vizuri sana...
Tundu Lissu amesoma naye darasa moja na Freeman Mbowe amecheza naye muziki ktk klabu mbalimbali ikiwemo ile iliyokuwa maarufu sana enzi hizo, Billcanas...
Amesema haielezeki kirahisi kwa kiongozi wa chama kukaa uongozini miaka 21 lakini akawa hajaandaa succession plan ya uongozi wa chama na taasisi/idara zake ili kujenga sustainability ya chama ktk kutekeleza shughuli na malengo yake hata pale atakapokuwa hayupo...
Huo ni udhaifu mmoja mkubwa wa Freeman Mbowe na udhaifu unathibitishwa na namna anavyowafungia njia wenzake kupata fursa ya kutumia vipawa vyao kukijenga chama. Na sasa, kuna kila sababu kusema kuwa amechokwa na wanataka kumfurusha/kumwondoa kwa nguvu...
Hii kwa lugha yoyote si heshima wala busara kwake kwa kushindwa kusoma majira na alama za nyakati ili kumwezesha kufanya maamuzi sahihi....
Aidha, anasema pia kuwa miaka 10 na pengine chini ya hiyo ilimtosha Freeman Mbowe kukitengeneza chama na kuwaachia wengine. Ingeweza kuwa John Heche, Godbless Lema, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, Tundu Lissu, John Mnyika na wengine wengi tu. Hakufanya hivyo na badala imeleta mtafaruku unaoweza kukidhoofisha chama kwa kiwango kikubwa..
Amemaliza kwa kusema,FREEMAN MBOWE ATALAZIMISHWA KUTOKA CHADEMA whether he like it or not....!
Msikilize ☝🏻☝🏻☝🏻