Jerry Muro ameiaibisha nchi, TFF, Yanga na Wanataaluma..ajiuzuru!

N nimethibitisha we Ni simba,ya muro waachie waajiri wake ,au unataka ajiuzuru ili mite go hicho upewe wewe
 
Kama ni kweli Jerry muro ndio kaipotosha Yanga kwa kutokutimiza wajibu wake vizuri hadi ombi la Yanga likataliwe, ana haki ya kupewa onyo kali sana na kuomba radhi viongozi na mashabiki wake. Otherwise inaweza ikawa ni tatizo la Yanga yote labda walikuwa hawajafanya maamuzi kamili au bosi wao Manji alikuwa hayupo na hajatoa approval.

Kuchelewa huku kwa Yanga na uamuzi wa CAF kunainyima Yanga mapato maana hii mechi ilistahili kujaza uwanja, lkn pia kuharibu ratiba ya kocha.
 
Mkuu tatizo we unajulikana kabisa kuwa ni shabiki la kutupwa la Lunyasi, Kiukweli mkuu Simba inatupa tabu sana huku mtaani.


Anyway utabiri wako wa 7 mtungi naomba sana utimie. Ameeeen

Una uthibitisho wowote ule kuwa Mimi ni " Chura churani? "
 
nyie wamatopeni fuatilieni yakwenu,hayo mambo ya mganga kasema kuna siku sio nzuri ndo yanayowafanya timu lenu likose ubingwa kwa kuendekeza ushirikina,
 

Sasa Mkuu kwa haya maelezo yako Wewe huzioni hapo goli wiki / saba ( 7 ) ? Sijui kwanini Yanga yangu huwa kila mara inaingizwa choo cha Kike na huyu Msemaji wetu. Mwenyekiti wetu tunayekuchaguaga kwa njaa zetu wenyewe Manji huyaoni haya Tajiri?
 
nyie wamatopeni fuatilieni yakwenu,hayo mambo ya mganga kasema kuna siku sio nzuri ndo yanayowafanya timu lenu likose ubingwa kwa kuendekeza ushirikina,

Waambie Simba wenyewe Mkuu kwani Mimi kila mtu humu anajua kuwa ni Mwana Yanga tena wa Kindaki ndaki kabisa japo damu yangu ni Nyekundu ya kutukuka. Sijui tufanyeje sisi Wana Yanga ili tuwaombe msamaha TP Mazembe kwani kila tukichungulia kwa " Babu " tunaziona saba na tisa mara kwa mara.
 
itawezekanaje kufungwa saba nyumbani mkuu? hata simba huyu japokuwa anaumwa zika lakin hawez fungwa saba pale taifa
 
itawezekanaje kufungwa saba nyumbani mkuu? hata simba huyu japokuwa anaumwa zika lakin hawez fungwa saba pale taifa

Sasa Mkuu kwa beki yetu hii ya akina Cannavaro, Yondani na Kamusoko hatutagawana maumivu hiyo Jumanne pale Taifa? Nasikia tumesajili mchezaji anaitwa James Chura vipi ataweza kuruka ruka mbele ya Le Tout Puisant Mazembe?
 
Sasa Mkuu kwa beki yetu hii ya akina Cannavaro, Yondani na Kamusoko hatutagawana maumivu hiyo Jumanne pale Taifa? Nasikia tumesajili mchezaji anaitwa James Chura vipi ataweza kuruka ruka mbele ya Le Tout Puisant Mazembe?
usiogope mkuu kama goli nyingi tungepigwa na mafarao pale misri,acha uoga
 

nakubaliana na wewe kwa 100% - Muro kakosea kweli. kama ulivyopatia kusema, inaonekana anasukumwa zaidi na unazi na si principles za kiuongozi.

but na wewe pia naona umekosea kwani umeongea kinazi zaidi. mambo ya mganga na Yanga yanahusiana vipi na ukakasi ulioupata kwa Muro?

obviously I can smell bitterness kwenye maneno yako. bitterness ya kuona Yanga inafanikiwa zaidi ya wengine (ambao Muro huwaita wa matopeni). hii ya kumnanga Muro ni sideshow tu lakini the crux of the matter ni kuwa una bitterness dhidi ya mafanikio ya Yanga!
 
usiogope mkuu kama goli nyingi tungepigwa na mafarao pale misri,acha uoga

Mafarao na TP Mazembe ni sawa Mkuu? Police na Mwanajeshi wanalingana uwezo japo wote ni wapiganaji au wapambanaji?
 

Hivi kweli Mimi Mwana Yanga naweza kabisa nikawa na uchungu na mafaniko ya timu yangu ya Kimataifa inayokaa katika Jengo chafu na kuu kuu sasa mwaka wa 77 huku kipindi cha masika tunatafutana pale Kaunda? Nitake radhi Mkuu kwani kwa wanaonijua humu Mimi ni Mwana Yanga wa kufa kufa!
 
Mpira wetu bongo ni mpira wa ndani ya mipaka yetu tu, hata Africa Mashariki tu, ni kimbembe, mpira unachezwa zaidi midomoni kupitia vyombo vyetu vya habari, masjabiki tu wameipaisha yanga ila tukija ktk uhalisia, tutaona ktk michezo iliyopo mbele yao.
 
Mambo ya Yanga yanakuhusu nini?

Nikiwa kama Mwanachama wa Yanga nina haki ya kulalamika kwa Kiongozi wetu tuliyemchagua kwa njaa zetu na umasikini wa kiupeo unaotukabili " Gabachori " ili hatua stahiki zichukuliwe. Tena unatakiwa unipongeze Mimi mwana Yanga mwenzio badala ya kunilaumu. Uko wapi Mkuu kwa sasa? Kama vipi tukutane huku Chalinze kwa " Babu " tunapojitahidi kupunguza hizi goli saba au tisa ambazo nimethibitishiwa kuwa ndiyo tutafungwa na TP Mazembe tarehe 28 June 2016. Anahitajika mtu wa kujitoa muhanga ila bahati mbaya kila mtu anapenda bado kuishi.
 
sasa wewe utaiweza nafasi ya jerry muro au unapiga kelele tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…