Jerry Muro amekubali yaishe, arejea mjini na kusema haya

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,440
Reaction score
8,149
-Mkuu wa kitengo cha habari Yanga SC, Ndugu Jerry .C. Murro amelazimika kukatisha likizo yake na kurejea jijini Dar, ambapo hakuwa na maneno mengi zaidi ya kusema. .

" Tulieni wala msijali nimeshafika jijini Dar. Kumbukeni NGARIBA HAOGOPI MKOJO"

======

jerry-muro-768x414.jpg

Kama utakuwa na kumbukumbu vizuri utakumbuka wiki iliyopita Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini ilimkuta na hatia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro na hivyo kumfungia mwaka mmoja kutokujihusisha na soka na kumpiga faini ya shilingi Milioni tatu.

Wakati Yanga ikipambana na Medeama katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), Jerry Muro aliandika Instagram “Tutaishangilia timu yetu mpaka watufungie na uku tu, ila wajue mpira kwetu ni sehemu ya maisha @yangasc”

Maneno ambayo Muro ameyaandika yamepokelewa na mashibiki wa soka kwa mitazamo tofauti wengine wakiona ametumia ujumbe huo kufikisha sehemu ujumbe lakini wengine wakiona ni maneno ya kawaida ila tu akionyesha mapenzi yake kwa Yanga.

13668996_1140485139328236_7011643253947783674_n.jpg

Jerry Muro ameamua kukubali hukumu iliyotolewa dhidi yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayomtaka kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja
 
Jerry kwa mipasho hajambo. Angefaa zaidi kuwa msemaji wa kundi la taarabu au bendi yoyote maarufu maana maneno yake yanawafaa zaidi kuliko medani ya soka.
 
Huyu mpuuuzi ale kitanzi tu,anaufanya ushabiki wa mpira uwe uadui,Simba/Yanga zipo muda mrefu na watu wanataniana na maisha yanasonga,..
 
Mourinho alipotua England nakuendeleza mipasho lakini pia teknikalitiz ndani ya pitch ligi ya epl ilichangamka sana na kuanza kushuhudia uwekezaji mkubwa katika vilabu ambavyo hapo awali hapakuwa na mpango wa waarabu na matajiri Wengine kutoka Asia kama vile Thailand kuweza kuwekeza. Binafsi namuunga mkono Jerry kwani TFF hii bila mipasho na kusemwa haiwezi kusimamia mchezo huu vizuri. Zipo changamoto zao marefarii, upangaji wa matokeo, vingilio na mgawanyo wa pesa. Muro huwa hafumbii macho madudu hayo. Kwa hiyo wapenda michezo wote bila kujali timu zetu na tofauti zetu Tumuungeni mkono. Huwezi kuwawekea utaratibu wa kukaa washabiki wa yanga kwenye mechi ya waarabu wa Tunis as if mechi inayochezwa ni ya DAR derby. Siku ya watani wajadi tuwekeeni utaratibu huo na ulishazoeleka. Ifike mahali haki na usawa katika soka la TZ vitawale mchezo huu.
 
Na mechi inayofuata ni free kama kawaida
 
Unataka kusema watu au wawekezaji waliwekeza kwenye EPL kwa sababu au moja ya sababu ikiwa ni mipasho ya Mourinho?????Mmmmmmmhhh????
 
Huyu mpuuuzi ale kitanzi tu,anaufanya ushabiki wa mpira uwe uadui,Simba/Yanga zipo muda mrefu na watu wanataniana na maisha yanasonga,..
Wewe ndio umefanya uadui..wengine tunaona ananogesha utani wa jadi!
 
Ameandika haya instagram
b624e571573be2f4d2647111be9e58bd.jpg

Kila nikifikiria figisu za soka la Bongo aisee nachoka kabisa, let me walk away for a while though I will be missing my fans and my people wa kimataifa but I must walk away for a while,”
 
afadhali aende tena siyo for a while ila jumla, nilimwona wa ovyo alipomtukana yule mwandishi wa kike aliyetaka habari za kocha na yeye kumjibu eti "unamwulizia kocha na mapumziko yake, unataka ukapumzike naye"...utumbo no.1
 
My funs! Nyie mlikuwa kichekesho kwake si ndio? Ama grammatical errors?
 
afadhali aende tena siyo for a while ila jumla, nilimwona wa ovyo alipomtukana yule mwandishi wa kike aliyetaka habari za kocha na yeye kumjibu eti "unamwulizia kocha na mapumziko yake, unataka ukapumzike naye"...utumbo no.1
Duh me nlijua ni mpuuzi tu, kumbe ni mpuuzi wa wapuuzi...... Tena kubwa lao!
 
Mkosi wa kumtukana yule binti mwandishi wa habari naona unamuandama. Alikua na kiburi sana tangu apate ile kazi. Let him go away forever.
 
Huyu jamaaa ni mseeeeeeeee.... dah cyber crime law inazinguaaaaa
 
Back
Top Bottom